Mahita ajitosa ubunge Moro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahita ajitosa ubunge Moro

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Josh Michael, Oct 4, 2009.

 1. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  JOTO la kuwania nafasi ya ubunge ndani la Jimbo la Morogoro Mjini limezidi kupanda, baada ya kuwapo habari za kuaminika kuwa zaidi ya watu wanne wamejitokeza kutaka kuchukua fomu katika uchaguzi mkuu ujao.

  Walioamua kujitosa kwenye kinyang'anyiro hicho kukabiliana na Mbunge wa jimbo hilo, Omari Mzeru, ni pamoja na aliyewahi kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali mstaafu, Omari Mahita, Aziz Abood, Profesa Ishengoma na mwanahabari Amina Said, ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya Morogoro Mjini.

  Kwa mujibu wa taarifa za ndani za kuaminika, kila mmoja anajigamba kupata nafasi hiyo ndani ya kura za maoni kupitia CCM, hali ambayo inaonyesha kuwapo upinzani mkubwa.

  Kwa muda sasa, jimbo hilo limeonyesha kuwa na upinzani mkubwa wa vyama vya CCM na Chama cha Wananchi (CUF), ambapo kwa upande wa CUF, Mkurugenzi wa Siasa wa chama hicho, Mbalare Maharagande, ametangaza jana nia ya kugombea tena nafasi hiyo.

  Akizungumza katika mkutano wa hadhara jana wakati wa mwendelezo wa mikutano ya chama hicho iliyopewa jina la Operesheni Zinduka kwenye viwanja vya Soko la Mawenzi, alisema dalili za kujitokeza kwa wagombea zaidi ya wawili ndani ya CCM kunaonyesha wazi mbunge aliyeko madarakani ameshindwa kuwatumikia wananchi wake.

  Alisema kuwa wananchi wamechoshwa na umaskini uliopo kwa sasa ingawa Morogoro ndicho kituo kikuu cha kati cha biashara, lakini hakuna hata mapato yanayoweza kusimamiwa na kuwafaidisha wananchi. Katika kadi zilizorudishwa, kulikuwa na wenyeviti wawili wa serikali za mitaa kutoka CCM, Kulwa Shaaban na Jamponi Gaston waliojiunga na CUF.
   
 2. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mahita si ndiye huyu aliyemkataa mtoto wake mwenyewe? Sasa ndio anaenda kugombea ubunge na ku adopt an entire constituency?

  Jamaa hana aibu!
   
 3. B

  Bao3 JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2009
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 318
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Inawezekana Morogoro hawajui hilo. Anajaribu bahati yake.
   
 4. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo una m support? Na unaandika kabisa "anajaribu bahati yake" unamaana unaamini uwakilishi wa watu uende kwa kufuatana na bahati?

  Attitudes kama hizi ndizo zinatupa viongozi tulionao, halafu wakiboronga tutalalamika?
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,389
  Likes Received: 5,670
  Trophy Points: 280
  Jamani hii inawezekana ikawa ni kichekesho kama kweli nimesikia jamaa anataka kugombania ubunge ameshindwa mtoto aliekamua kiunoni mwake huku jasho likimtoka ataweza wana morogoro zaiidi laki kadhaa???
   
 6. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #6
  Oct 4, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kazi kubwa sana, sisi kama wadau tutaona mambo mengi sana katk kuelekea uchaguzi mkuu mwakani
   
 7. M

  Mayolela JF-Expert Member

  #7
  Oct 4, 2009
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kukataa mtoto na ubunge ni vitu viwiwli visivyo na uhuhusiano kabisa.kama mtanzania na katiba inamruhusu atumie nafasi hiyo.
  kweli wenye visa watu.
   
 8. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #8
  Oct 4, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Tanzania hata uweke jiwe linaweza kutuongoza mradi lipitishwe na sisiem!
   
 9. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #9
  Oct 4, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  I beg to differ,

  Kukataa mtoto ni irresponsibility ya hali ya juu ambayo mwanadamu anaweza kuifanya.Hata baadhi ya wanyama wanaosemwa kutokuwa na akili kama binadamu wanajua kutunza watoto. Waswahili wanasema damu nzito kuliko maji, sasa huyu aliyeshindwa kuitunza damu (mtoto wake mwenyewe) ataweza kuwaenzi watu baki (maji) ?

  Fikra kama hizi za "kukataa mtoto na uongozi ni vitu tofauti" ndizo zinatupa viongozi kama kina Pinda na Kikwete.

  Kama mtu hana discipline kiasi cha kufanya rape (mahakama iangalie kama anaweza kushtakiwa kwa statutory rape) tena kwa mfanyakazi wake wa ndani, unafikiri akipata nafasi ya kuwa rape wananchi wa Morogoro katika ufisadi atakuwa na discipline ya ku resist?

  Sija question kama anaweza au hawezi kugombea, certainly this is a straight provision of his civil rights.What I am questioning is his ability to lead.These are two different things and should not be confused as one.
   
  Last edited by a moderator: Oct 5, 2009
 10. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #10
  Oct 4, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ivi kuwa mbunge ndo dili lililobaki bongo? Yani Mahita anataka ku-move kutoka IGP to mbunge? Is that psychologically possible? Hii ni kudanganya wananchi sasa! Upuzi mtupu! Ni sawa na Mrema kutaka urais...hahahaha
   
 11. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #11
  Oct 4, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Alaa,Mahita kajihukumu mwenyewe kuwa siku zile alipokuwa IGP, akidaiwa kuwa ana mahaba makubwa na CCM kiasi cha kuwa tayari kutumia wadhifa wake kukisaidia chama hicho kupata ushindi wa kishindo. Kiasi ya kutumia "ngunguri" kuwashughulikia wafuasi wa upinzani au wale waliothubutu, na kufikia hata kusababisha mauwaji ya kutisha kwa wananchi bila ya sababu. Nionavyo,hafai kuwa hata VEO,kutokana na rekodi mbaya ya utendaji wake kazi kama kiongozi wa chombo cha kusimama ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao kadhalika kama mwanajamii kwa kuwa na rekodi mbovu ya uongozi wa familia.
   
 12. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #12
  Oct 4, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Vyombo vya Dola vyote vinashabikia CCM hivyo kumbe Mahita wakati yupo katika Polisi alikuwa shabiki mkubwa sana wa CCM ndio maana alikuwa anawapa kipigo vyama vya upinzani
   
 13. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #13
  Oct 4, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Katika hao wote ni afadhali Mstahiki Meya Prof. Ishengoma.
   
 14. M

  Magezi JF-Expert Member

  #14
  Oct 4, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mahita amekuwa rafiki sana wa majambazi wa kutumia silaha wakati akiwa IGP sijui hana hata aibu? Hivi CCM huwa hawajui kwamba mtu akiwa mhalifu hafai kuwa kiongozi?? Naanza kuamini kwamba CCM hutumia pesa za ujambazi kujiimarisha pia kisiasa.
   
 15. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #15
  Oct 4, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  kumbe kisa chote cha mahita kumkataa mtoto ilikuwa kwa ajili ya manufaa yake ya baadae kama kugombea ubunge? nawashauri asichaguliwe kabisa kwani kashaonea udhaifu mkubwa sana kwenye huaminifu kutokana na kumchezea mchezo mchafu mke wake.namshangaa hata kua na moyo kiasi hiki cha kutaka kugombea ubunge baada ya kashfa nzito.kama ni kweli anataka kugombania ubunge.
   
 16. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #16
  Oct 4, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  CCM haina ubavu wa kupambana na CUF hapa Tanzania ikiwa uchaguzi utakuwa wa haki na usawa na ulio huru kabisa.
  CCM wanalielewa hilo ,kule kusema CUF ni Zanzibar tu ,ni kutafuta ahuweni na kupata kupumua ,lakini ukweli haujifichi,siku zote ukweli unakuwepo juu ya uongo ,mstari wa kiswahili unasema ,Ukweli ukidhihiri uongo hujitenga ,Tumeona CUF ilivyoitikisa Dar ,sio mchezo polisi wenyewe natumai wametambua kuwa CUF ni Chama kinachoishikilia amani ya Nchi hii na wakijifanya wao ni ngunguri watashindwa kuzuia vurugu yeyote ile itakayoamuliwa na CUF katika kudai haki inafuatwa.
  Morogoro ,nani asiejua kama Morogoro ni CUF watupu ? Ndio maana imekuwa ikipuuzwa katika kupatiwa maendeleo.
  Ila safari hii nchi imekalia vibaya sana ,Serikali na CCM yake wasipoangalia wataipeleka Nchi katika mapambano ,jambo ambalo Mheshimiwa Mwema amesikika akisema itawawia vigumu kuirudisha nchi katika amani ikiwa itavurugika.

  Hapo ndipo yeye Said Mwema ajue ni nini la kufanya ,afanye kazi yake kama chombo ambacho kinatakiwa kisifungamane na upande wowote ule ,sio CUF wala CCM wala Chadema wala wengine. Lakini akijidai kupokea au kutoa rushwa ili mapolisi watumike na kukubali kutumiliwa basi ajue kuwa yeye atakuwa wa mwanzo kubeba lawama ,akina Kikwete na Karume watamruka vibaya sana ,wakidai dhamana yote ni yake kama polisi waliuwa walinajisi kwa chochote watakachokifanya naamini kabisa yeye Said Mwema atakuwa mshitakiwa nambari one. Kama Arusha au Jiniva.
   
 17. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #17
  Oct 4, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kuna haja ya kuwa na watu walio kuwa huru kuliko kuwa nusu nusu kama hivi, mara wanashabikia CCM mara hawana chama kabisa
   
 18. M

  Magezi JF-Expert Member

  #18
  Oct 4, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Hivi niulize CCM hakuna watu wengine? Kila kona ni wazee wastaafu, mtu amekuwa IGP, amepora maeneo ya watu, ameshirikiana na majambazi mpaka akastaafishwa kabla ya muda, bado tu yumo.

  Ameua watu zanzibar!! halafu hata wanaharakati wa haki za binadamu tanzania nadhani hawako serious, kwa nini wasimshitaki mahita kwa mauaji ya zanzibar??
   
 19. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #19
  Oct 4, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Kama una historia ya wizi, mauaji, uzinzi, uwongo, unyanyasaji na kiburi, ingia CCM na gombea ubunge kwa tiketi ya CCM, mambo yako yatakunyokea. Mafisadi wa CCM hulindana kwani nje ya CCM hawana usalama. Siri ya mafanikio katika maisha kwa watu waovu ni maisha ndani ya CCM. Mkuu wa majeshi mstaafu alitaka ubunge, mkuu wa polisi mstaafu anataka ubunge na mkuu wa usalama mstaafu atataka ubunge - wooote hao kupitia CCM. Hatutashtuka kumsikia mkuu wa nchi mstaafu akiutafuta ubunge - akiupata tu dhambi zake zote zitasamehewa.
  Naipenda Tanzania :confused:
   
 20. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #20
  Oct 4, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mstaafu Rais Moi wa Kenya enzi za ubabe wa KANU akisema kuwaambia Wakenya kuwa "...bila ya KANU hakuna maendeleo, bila ya KANU askari hawalipwi mishahara...bila ya KANU..." ilimradi bila ya KANU kila kitu hakuna,baadhi ya askari Kenya waliamini kabisa kuwa kweli wafanye kila wanaloambiwa na kuagiwa na wakubwa wao kuilindan KANU ibaki madarakani... leo wapi KANU haipo na wao wanaendelea na serikali ya chama chengine kutoka upinzani, askari wetu wajifunze hapa kuwa chama chochote kinaweza kuwa 'bosi wao', leo kama wanaona raha kutandika wapinzani virungu wajuwe kesho wapinzani hao hao wanachukua hatamu za nchi watakuja watazama kwa jicho gani?
   
Loading...