Mahindi ya kuchemsha

Mahindi ya mjini mengi yanakuwa ya muda mrefu! We jiulize kwanini hata mahindi ya kuchoma mikoa mingi wanayala hivyo hivyo ila mjini ni hadi tukandikepo ndimu na pilipili ndiyo yanalika maana hivi hivi hayaliki!

Ya mikoani mengi ni fresh sababu mikoa mingi wanalima mahindi ila mjini hakuna mahindi yanayolimwa! Hivyo ni hadi ya mikoani yasafirishwe yakae njiani yafike huku ndiyo yapikwe mengi yanakuwa yashapoteza ladha!
 
Kuna mahindi nimeyapanda karibu na choo cha nje nyumbani kwangu hapa Dar yaani ukichemsha ni matamu ya mikoani yanasubiri
 
Why mahindi ya kuchemsha ya mikoani au vijijini au pembezoni mwa jiji Yana ladha tamu kuliko haya ya mjini?
Shida iko wapi?

Wa mjini wanakosea wapi?

Kutumia gesi? Umeme? Au aina Tu za mahindi?
Ardhi ya Dar es Salaam ina chumvi, kwa hiyo kila kitu kimachotokana na ardhi ya Dar es salaam, kina ladha tofauti na kitu kingine chiochote kile kinacholimwa mikoani, vya mikoani vyote vina ladha, vya Dar es salaam, havina ladha. Ni sababu ya ardhi ya chumvi.

Actually hata nyama ya Dar es Salaam inayotokana na ng'ombe wanaofugwa hapa, ilitakiwa iwe na ladha tofauti na nyama ya ng'ombe wa mikoani, except kwamba nyama huwa tunaweka chumvi, na hivyo effect ya chumvi huwa inashindwa kuonekana sawawa. Hizi nyama mbili zikipikwa bila kuwekewa chumvi, nyama ya Dar es sakaam itaonekana ni tamu kuliko ile ya mikoani kwa sababu ya huku tayari ina chumvi kiasi.

Pia Soda za Mwanza zina ladha tofauti na za Dar es salaam.
Mimi naishi maisha ya shida sana linapkuja swala la chakula kwa sababu niko sensitive sana kwenye ladaha, na sijakulia huku
 
Back
Top Bottom