Mahiga: Serikali inajua matukio ya utesaji wapinzani inafuatilia, wanaulizwa na Jumuiya za Kimataifa

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Agustino Mahiga, amesema matukio ya utesaji ya wapinzani na uvunjifu wa amani pamoja na madai ya wapinzani ni miongoni mwa mambo yanayoulizwa na Jumuiya za Kimataifa na serikali inaendelea kuyafuatilia.

mahigaa.jpg

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Agustino Mahiga

Waziri Mahiga ametoa kauli hiyo Bungeni jijini Dodoma katika muendelezo wa vikao vya Bunge baada ya kuulizwa swali na Mbunge wa CUF Ali Saleh, ambaye alihoji juu ya uwepo wa matukio hayo na kueleza ni uvunjaji wa haki za binadamu.
Akijibu swali Waziri Mahiga ameeleza kuwa "kuhusu matukio ya utesaji wa wapinzani na uvunjaji wa haki za binadamu, matukio yanajulikana serikalini na vyombo vya usalama vinafuatilia."

"Mara nyingi tunapata taarifa na majibu yanaridhisha, kazi ya upelelezi inaweza kuchukua muda, maswali haya yanaulizwa na wananchi, yanaulizwa kimataifa, tupo tayari kutoa taarifa sahihi uchunguzi ukikamilika" ameongeza Mahiga

Kwa sasa Bunge linaendelea jijini Dodoma, ambapo Mawaziri mbalimbali wameendelea kuwasilisha makadirio yao ya bajeti na wakiomba ridhaa ya kupitishwa na wabunge.

Chanzo: EATV
 
Siku itakayo tokea kwa mjukuu wa huyu waziri kutekwa,ninamtegemea atatoa jibu kama hili,ndio maana Bunge letu linafanana na old homeage ,watu kama hawa ilitakiwa wawe wameshastaafu long time ago na kuwaachia vijana kuzifanya kazi hizi kwa makini zaidi.
 
Inamaanisha hatupo salama kwa majibu kama haya. Miaka miwili inaenda sasa, alzory, Ben na huyo Lisu. Kwahiyo wateswe tu, wapotee tu, waumie tu... Eti serikalini inakuja na majibu.

Hivi hawa wasomi kweli? Hawajajifunza kukaa kimwa kuficha udhaifu kama huu?
 
Serikali inafanya jambo muhimu sana ili kuona kama hayo madai yana uhalali na pia ni muhimu wakiyatolea ufafanuzi, baada ya huo uchunguzi kukamilika.
 
Mkuu are you serious na haki ya KILA mTanzania kuishi na kuwa huru? Kwamba inawezekana ni uongo na/au madai haya si halali?
 
Jibu la Mahiga limekwenda shule sana, inahitaji akili kulielewa.

Kwanza amekili hayo mambo yapo na Jumuiya za kimataifa zinafuatilia kwa karibu.

Hili jibu sidhani kama linatampendeza Magufuli.

Ila sipati picha hilo swali angeulizwa Lugola jibu lake lingekuwaje.
 
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Agustino Mahiga, amesema matukio ya utesaji ya wapinzani na uvunjifu wa amani pamoja na madai ya wapinzani ni miongoni mwa mambo yanayoulizwa na Jumuiya za Kimataifa na serikali inaendelea kuyafuatilia.

mahigaa.jpg

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Agustino Mahiga

Waziri Mahiga ametoa kauli hiyo Bungeni jijini Dodoma katika muendelezo wa vikao vya Bunge baada ya kuulizwa swali na Mbunge wa CUF Ali Saleh, ambaye alihoji juu ya uwepo wa matukio hayo na kueleza ni uvunjaji wa haki za binadamu.
Akijibu swali Waziri Mahiga ameeleza kuwa "kuhusu matukio ya utesaji wa wapinzani na uvunjaji wa haki za binadamu, matukio yanajulikana serikalini na vyombo vya usalama vinafuatilia."

"Mara nyingi tunapata taarifa na majibu yanaridhisha, kazi ya upelelezi inaweza kuchukua muda, maswali haya yanaulizwa na wananchi, yanaulizwa kimataifa, tupo tayari kutoa taarifa sahihi uchunguzi ukikamilika" ameongeza Mahiga

Kwa sasa Bunge linaendelea jijini Dodoma, ambapo Mawaziri mbalimbali wameendelea kuwasilisha makadirio yao ya bajeti na wakiomba ridhaa ya kupitishwa na wabunge.

Chanzo: EATV
- KumbukiziMTAFUTANO.jpg

uchunguzi upi anaousema huyu mzee ?
 
Kama umeisoma zaidi ya mara tatu na haujaelewa basi achana nayo haikuhusu.
Mhmmm inanihusu mkuu maana hutesaji ambao serikali unakiri kuujua na kukosa majibu si salama kwa watanzania wote achilia mbali kupin point wapinzani!!!!
 
Back
Top Bottom