Mahesabu ya Zitto na wapambe wake yamekwenda kombo -- namsikitikia sana!

Mwanza wamewapiga marufuku mbowe na slaa mpaka wamrudishie zitto uongozi.. Wamepewa cku ine tu la sivyo maandamano yanakuja
Mkuu unaiongerea Mwanza ipi? Unaweza kunitajia mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa kwa wanamwanza? Ulimola?
 
Leo ni takriban siku ya 12 tangu Zitto na wenzake wavuliwe uongozi Chadema kutokana na usaliti walioukiri.

Hadi leo sijaona mtikisiko wowote (nasema mtikisiko) kwa chama hicho nchini kuhusu kupinga hatua hii ya kamati kuu ya CDM, zaidi ya kelele na matusi humu JF, kelele ambazo naamini kwamba kwa asilimia kubwa zatoka CCM., pamoja na kutoka kwa akina Fyonza na wasaliti wenzake.

Support kubwa anayopata Zitto ni katika magazeti ya Uhuru, Habari Leo na Daily News, kitu ambacho ilimpaswa kujiuliza vipi?

Nilitarajia katika siku hizo 11 yafuatayo yangetokea:

1. Maandamano makubwa ya wana CDM - hata katika asilimia 40 ya mikoa yote (au aslimia 40 ya wilaya zote) kumsupport Zitto. Hilo halijatokea., na pia Zitto ajiulize kwa nini.

2. Mlolongo wa kujiuzulu kwa viongozi wakuu wa CDM – hata kwa silimia 20 tu (kamati kuu, wenyeviti mikoa etc). Hilo pia halijatokea na Zitto inapaswa ajiulize kwa nini.

Ama kweli Zitto kwishney – mahesabu yake yamemuumbua sana! Na wanaomtetea CCM wamepatikana kwa hili kwani ‘watu wao’ katika CDM wametimuliwa na ndiyo maana wanasononeka sana.

___
Umeanza kwa kukemea matusi halafu ukarudi kwenye matusi! FYONZA naamini ni Shonza,lakini huyu ni mzazi wa Juliana Shonza. Tuwatendee haki wazazi. "waheshimu baba na mama upate miaka mingi na heri duniani". Huyu dada makosa yake yasihusishwe na mzazi wake.
 
hiyo ni hatua ya kwanza bado! bado chama kitachukua hatua stahiki hivi karibuni hatutaki wanachama wanafiki wasio na uchungu wa nchi bali wa kwao na kakundi kenye maslahi binafsi. atanyooka na atajutia mikakati ya kuliangusha taifa na harakati za kujikomboa
 
Kweli huyu zitto ni msaliti toka long na ni fisadi kama magamba wengne na ndo kapunguzaga zile kelele zake kwa magamba wenzake siku hizi..
 
Asilimia kubwa ya wanaolalamikia suala kuvuliwa uongozi ZITTO KABWE na wenzake kwa USALITI nia yao kubwa ni kuona chama hiki kinasambaratika katika ulimwengu wa siasa. Kwa bahati nzuri mbinu zao zinagundulika mapema kabla hata ya robo ya mipango yao kuanza kutekelezwa.
 
Mie nashangaa kwqa nini hafukuzwi haraka uanachama - akawe Mbunge wa Mahakama. Ni nyoka kabisa kuwa naye katika kundi lenye malengo mema. Kwanza hashangai makada wa CCM - Nape na Nchemba ndiyo wanamuonea huruma -- inawahusu nini wao. Si wanataka CDM ipasuke? Wanafiki tu!
 
Asilimia kubwa ya wanaolalamikia suala kuvuliwa uongozi ZITTO KABWE na wenzake kwa USALITI nia yao kubwa ni kuona chama hiki kinasambaratika katika ulimwengu wa siasa. Kwa bahati nzuri mbinu zao zinagundulika mapema kabla hata ya robo ya mipango yao kuanza kutekelezwa.

hii si comment tu ambayo ungeweza kuiweka kwenye thread nyingi zilizomo humu-kwani kulikuw na haja hadi uanzishe thread yako? ama kweli.
 
Asilimia kubwa ya wanaolalamikia suala kuvuliwa uongozi ZITTO KABWE na wenzake kwa USALITI nia yao kubwa ni kuona chama hiki kinasambaratika katika ulimwengu wa siasa. Kwa bahati nzuri mbinu zao zinagundulika mapema kabla hata ya robo ya mipango yao kuanza kutekelezwa.
Ndugu yangu umesema kweli tena unaona mbali utakuta hata wanachama wa ccm wanashabikia hapo ndipo utaona kuwa kuna njama chafu.watanzania tuamke
 
Back
Top Bottom