Mahesabu msiyopenda kusikia kuhusu Makamu mpya wa Rais

Yaani Chadema bwana wakati huo huo hawaitaki CCM na wakati huo huo wanawataka watu fulani wa CCM.
So pathetic
Kikatiba uchaguzi mwingine utafanyika 2025. Kwa sasa yeyote asiyependa CCM analazimika kuishi na CCM hadi 2025 atakapopata nafasi nyingine ya kujaribu tena.
 
Ili afanikiwe na chama chake kisirudi ktk zama za kutumia pesa kushinda uchaguzi inabidi apate mtu asie wa makundi.

Mtu anaweka maslahi ya nchi mbele kuliko maslahi yake binafsi au ya kundi lake.

JPM hakuingia na kundi so hakuwa na muda wa kurudisha fadhila kwa mtu yoyote.
Mzee Kayanza Peter Pinda atafaa sana kwa hii transition
 
Hakuna kitu kama hicho kitatokea,jeshi liko nyuma ya Raisi Samia suluhu Hassan.Unafikiri rahisi kihivyoo eeeh.
Rejea hotuba ya General Mabeyo jana.
Jeshi limesha ona likifuata hawa wanasiasa watapoteza nchi maana wote wana maslahi yao binafsi
 
Ndio mana nasema mama afumue mizizi yote ya JPM apange safu yake haraka na kuwaweka kando ya mfumo hawa wapambe wa JPM mana kivyovyote hataweza kuwaridhisha mana walishalamba Uhuru na Ukwasi mkubwa sana, Mama aje na safu yake ambayo itakuwa loyal kwake
Lakini pia hawa Walio achwa na Mzee nataka niwatahazarishe kuwa Amiri Jeshi Mkuu ni mtu mwenye Nguvu sana sana Wasijaribu kufanya lolote wataumia tu, Na hili mzee Magu ali prove kuwa Rais ni Mhimili uliojichimbia ndio maana tumeshuhudia watu kama kina kinana wana surrender, Hata Mkwere anafahamu fika power ya Rais achana na porojo za kitaa sijui kuungwa mkono, Rais anahitaji Inner circle ndogo sana ya kumsupport tena iwe loyal haswa the rest waweza kushugulikiwa wakati wowote na saa yoyote
 
Baada ya kuapisha VP, Rais atavunja baraza la mawaziri asubuhi na mida ya mchana atapeleka jina la PM (Majaliwa) bungeni na kesho yake bunge litamthibitisha.

Hapa Rais atakuwa ameondoa minong'ono ya kwamba amevunja katiba ya kuendelea na baraza lile lile la Magufuli

Mawaziri wa sasa walio wengi watarudi na baadhi yao watabadilishwa wizara.

Mwana mpotevu a.k.a mtabiri atapelekwa ofisi ya VP kama kifuta machozi akashughulike na mazingira ambako sauti yake itakuwa ikisikika kwa nadra!
Rais halazimiki kuvunja baraza la mawaziri. Ni hiari yake kufanya hivyo, katiba haijamlazimisha. Hivyo akiamua kuendelea na baraza hilohilo ni sawa tu, hatakuwa amevunja katiba popote.
Kumbuka hii ni serikali inayoendelea, ya awamu ya 5, siyo serikali mpya.
 
Kama ulimsikia kiongozi mmoja wakati anatoa salamu za kumuaga JPM akitamka mwaka 2022, ilihali akizungumzia tukio la mwaka 2020 hebu na anyooshe mkono.
Niliwaza sana kauli ile ya JK ni kuwa aliteleza au Ndio mambo ya Long term plan
 
Awaache mpaka wampigie kura ya kutokuwa na imani naye? Yeye mjinga wakati ana mamlaka makubwasana kuwazuia .
 
Japokuwa sijui siasa... Ila Aise msimsahau RC Anthony Mtaka ... Anafaa kabisa kuwa makamu wa rais... Ni maoni tu..
 
Wapinzani katika ubora wenu mmeanza tena kutuletea ramli zenu chonganishi!!!

FYI utabiri wako will never come to pass - Serikali ya CHAMA tawala na Wabunge wake hawawezi kuruhusu mpasuko wowote ndani ya Serikali na kwenye CHAMA,wana inbuilt mechanisms za kuhakikisha hilo halitokei hasilani - kama ulisikiliza vizuri rai ya CDF jana kuna kitu alipaswa kujifunza i.e ungefikiri mara mbili kabla hujatuletea bandiko lako hapa. Good day.
Ni uhuru wa mawazo na wa kujieleza. Hayo ni mawazo yako, na wengine pia wana mawazo yao. Karibu.
 
Sequence of events:
  1. Suppose Kundi mojawapo katika wanaotaka nafasi hiyo wana mshikamano na Spika.
  2. Halafu mtu wao anateuliwa kuwa makamu wa rais.
  3. Bunge linampitisha kwa kauli moja, anaapishwa kuwa makamu wa rais
  4. Baada ya miezi michache wabunge wanaanza kuhoji ufanisi wa rais.
  5. Hoja ya kutokuwa na imani na rais inaletwa kwa mujibu wa ibara ya 46 ya katiba, spika anakubali ijadiliwe, na inapita kwa kauli moja na azimio la bunge kuwa limekosa imani na rais.
  6. Katiba inafuatwa tena, makamu huyo anakuwa rais, anaapishwa, duara linarudi lilipoanzia.
Nyie bisheni.
Spika mwenyewe wakati wa kutoa rambirambi, nilishindwa kumuelewa ni kama mtu aliyestukizwa!
Aliyoyayongea hayakuwa na mwelekeo au utashi wa Spika, Nahisi tunahitaji spika mwingine anaejitambua.
 
Sequence of events:
  1. Suppose Kundi mojawapo katika wanaotaka nafasi hiyo wana mshikamano na Spika.
  2. Halafu mtu wao anateuliwa kuwa makamu wa rais.
  3. Bunge linampitisha kwa kauli moja, anaapishwa kuwa makamu wa rais
  4. Baada ya miezi michache wabunge wanaanza kuhoji ufanisi wa rais.
  5. Hoja ya kutokuwa na imani na rais inaletwa kwa mujibu wa ibara ya 46 ya katiba, spika anakubali ijadiliwe, na inapita kwa kauli moja na azimio la bunge kuwa limekosa imani na rais.
  6. Katiba inafuatwa tena, makamu huyo anakuwa rais, anaapishwa, duara linarudi lilipoanzia.
Nyie bisheni.
Bunge hili kutokuwa na imani na Rais!!! hakuna kitu hicho kutokea karibuni...kumbuka wabunge hawa wengi wameingi bungeni kwa "fadhila" ya alieondoka...
 
Kwahiyo unadhani kutokuwa na imani na Rais ni kwamba makamu ndio atakuwa Rais?

Hakuna kitu kama hicho. Soma katiba vizuri.

Kuna mazingira ambayo makamu anaweza kuwa Rais kwenye Ibara ya 37 ya katiba yetu.
Mkimuondoa kwa kura ya kutokuwa na imani anakuja na kulivunja bunge na tunarejea kwenye uchaguzi.
 
Kwahiyo unadhani kutokuwa na imani na Rais ni kwamba makamu ndio atakuwa Rais?

Hakuna kitu kama hicho. Soma katiba vizuri.

Kuna mazingira ambayo makamu anaweza kuwa Rais kwenye Ibara ya 37 ya katiba yetu.
Mkimuondoa kwa kura ya kutokuwa na imani anakuja na kulivunja bunge na tunarejea kwenye uchaguzi.
Weka vifungu mkubwa. Ibara ya ngapi hiyo?
 
Back
Top Bottom