thread critic
Member
- Jul 17, 2012
- 71
- 14
kweli
kama unanjaa utaonewa kila kukicha
kama unanjaa utaonewa kila kukicha
Sasa ushauri huwa wanaomba wa nn kama hawawezi kuufuata.
kilimo bila viwanda na miundombinu ni kazi bure..
wtf dude??Jamani mtoto wa masikini kama mimi naruhusiwa kugombea urais? Nina talent ya kiongozi ila siko kwenye system
mi nafikiri mtu mwene njaa ndio kichwa chake kinachangamka zaidi...Tungekula tukashiba, lazima tunge pata akili ya viwanda na mambo mengine, Jmaa aligundua AKILKI HATUNA kwa sababu ya NJAA!
huu ndio mfumo kristo
Mahathir Muhammad aliyekuwa Rais wa Malaysia na ambaye sera zake zimeifanya Malaysia kuendelea vilivyo aliombwa ushauri na Rais Mkapa (alipokuwa Rais) juu ya siri ya Malaysia kuendelea ili na sisi tupewe hiyo dawa waliyotumia Malaysia.
Jibu la Mhathir lilikuwa very simple: ''Anzisha sera inayoeleweka ya kilimo, Lisha raia wako na muwe na reserve kubwa ya Chakula kwanza kisha mengine yatafuata''

Mpaka ngano tunaagiza toka nje.
Namheshimu sana Mahathir kwa kuwa kiongozi wa aina ya Nyerere katika kuwa na mapenzi makubwa na nchi yake na kuifikisha mbali sana kiuchumi.
Lakini lazima tukiri kwamba kugundulika kwa mafuta Malaysia kulichangia sana kuiinua nchi hiyo kiuchumi, kwa kuwa Mahathir alikuwa kiongozi makini. Leo hii Petronas, kampuni ya taifa ya mafuta Malaysia, ni mojawapo ya makampuni makubwa ya mafuta duniani. Si kweli kwamba kilimo pekee ndio kiliinua Malaysia.
Kwa hiyo Mahathir alipaswa kumwambia Mkapa ahakikishe anatumia rasilimali za nchi, dhahabu, Tanzanite, almasi, mbuga za wanyama nk, kwa kuifaidisha Tanzania, sio kuwafaidisha wawekezaji.
Kwa nchi kama Tanzania, tunapaswa kuyafanya madini yetu kama ndio mafuta yetu, na kuhakikisha kampuni ya madini ya taifa, STAMICO, ndio inasimamia mambo yote ya madini pamoja na utoaji wa leseni za exploration na uchimbaji, na kungia kitu inaitwa "Production Sharing Agreement, PSA" na wawekezaji wote wa madini nchini, wa ndani na wa nje.
Inabidi tutumie formula ya PSA ya mafuta kwa madini yetu, na kuifanya STAMICO kama vile Petronas ya Malaysia au STATOIL ya Norway.
huu ndio mfumo kristo