Mahari na nafasi yake katika ndoa... Je, utamaduni huu umepitwa na wakati?

Mahari ni ujinga na upumbavu tu. Hazina maana yoyote ile zaidi ya kum-objectify mwanamke.
 
Mi ningekuwa na uwezo ningeabolish hii kitu inaitwa mahari! ndugu zetu Waislam walijua kuna watu watatia ufisadi ndo maana wakasema mahari inatamkwa na mwolewaji tu!

Na muolewaji kwa kuwa anaujua mfuko wa mwenzie basi hatataka kumkomoa kwa kutamka anataka mahari ya milioni sita. Atatamka bei poa tu ili waendelee na maandalizi ya harusi na siyo kuanza kubishana kuhusu ukubwa wa mahari. Mahari ni muhimu kama ahsante kwa mrembo wao, lakini kama inakuwa kubwa kupita kiasi basi hapo mahari inakuwa tena haipendezi.

Wazazi wa mwanaume nao hawastahili 'ahsante' ya kumlea mtoto wao vizuri?
 
...kwa taarifa yenu, heri hao wanaotaka mahari kubwa kubwa, mkishaoana hawawaletei za kuleta. Waogopeni wanaojifanya aarrgghh, "...mahari chochote tu baba, tushakuwa ndugu!"

Utajikuta maisha yako yote unaendelea kutoa 'mahari' -indirectly,...jukumu la kuwasomesha wadogo zake mke, na kuwatimizia haja ndogo ndogo hadi zile kubwa kubwa pamoja na wakwe ndio jukumu la kila siku...
 
Mbu, Usisahau pia manyanyaso atakayoyapata binti aliyetolewa "mahari" ya shilingi milioni sita. Usishangae siku moja anakuja kuwagongea wazazi huku akilia kwa majonzi makubwa sana kwamba "nimechoka kuwa mtumwa naomba mrudishe mahari ya watu mliyopokea maisha ya ndoa yamenishinda."
 
Hivyo mahari ndio inamfanya binti anyanyasike kwa mumewe? Mie nadhani sio mahari, kama ingekuwa mahari ndoa nyingi tu zingekuwa na misuko suko. Asilimia kubwa ya Wanawake wananyanyasika kwa mahari ni wale ambao ni tegemezi kwa mwanaume.
Kama mwanaume una pesa, hata ukipangiwa mahari kubwa mie naona hakuna ubaya, tatizo lipo mtu mwenye kima cha chini kupangiwa mahari kubwa.
Na hawa wazazi/walezi wanaopanga hizi mahari huwa wanafahamu uwezo wa huyo bwana. Kama una dau kubwa na mahari nayo kubwa.
 
Pretty, na kwa nchi yetu hawa wenye kipato kidogo cha kushindwa kumudu mahari ya milioni sita ni wengi sana ukiondoa labda kundi la mafisadi ambao hata wakiwekewa mahari ya milioni 50 wengi hawataiona kama ni mzigo mkubwa
 
Kwa ki-Islam Mahari ni Suna tu sio lazima, hayo nimaelewano baina ya wazazi, wala sio kama ndoa haiwi halali bila ya mahari. Kuna mtu alikwenda kuposa na baada ya wiki alipopewa jibu kua amekubaliwa, akauliza " baba mahari ni kiasi gani?" Baba wa mtoto wa kike akamjibu " mimi simuuzi (not for sale) mtoto wangu" lakini ikiwa unakusudia sunaa tu basi niletee hata kichupa cha mafuta mazuri nikijipaka na nikasikia harufu nzuri basi nitajua hii ni mahari ya mtoto wangu na tuko kwenye Furaha. Jee leo hii kuna wazee wangapi wanafanya hivi?
 
Mahari muhimu lakini kwa kiwango cha 6m jameni! Ni kikubwa sana, inakuwa ni biashara. Hii imenikumbusha kabila fulani kanda ya ziwa, mwanamke akitolewa mahari akaolewa, mfano ng'ombe 20, ikatokea kuna jemba jingine likampenda huyo mama aliyeolewa, basi jemba linarudisha zile ng'ombe 20, na kuongezea za kwake zingine kadhaa, kisha ruksa kumuoa huyo mwanamama! Mila zetu hizo!
 
Wakwe wanataka muoaji aandae send off halafu tena harusi, hilo ndiyo tatizo lako. Mimi nikitoa sana ng'ombe wawili tu wa kawaida, kwanza wadogo..wakikataa tunaondoka hivyohivyo na my mpendwa wangu..
 
Duh!!!! mahari 6,000,000Tsh. halafu bado kwenye harusi yenyewe kama hutaambiwa utoe 10,000,000Tsh kwa ajili ya kamati. Kweli hapa ni kukomoana, sisi ambao bado tupo tupo kwanza sijui kama tutafika.
 
Hivyo mahari ndio inamfanya binti anyanyasike kwa mumewe? Mie nadhani sio mahari, kama ingekuwa mahari ndoa nyingi tu zingekuwa na misuko suko. Asilimia kubwa ya Wanawake wananyanyasika kwa mahari ni wale ambao ni tegemezi kwa mwanaume.
Kama mwanaume una pesa, hata ukipangiwa mahari kubwa mie naona hakuna ubaya, tatizo lipo mtu mwenye kima cha chini kupangiwa mahari kubwa.
Na hawa wazazi/walezi wanaopanga hizi mahari huwa wanafahamu uwezo wa huyo bwana. Kama una dau kubwa na mahari nayo kubwa.

Pretty, hawaaangalii hilo, wengine maadamu binti yao mweupe mfano usukumani mahari inaenda juu! Ndugu yangu mmoja alioa huko alipomaliza tu chuo, mahari aliyoambiwa ilikuwa kasheshe, kama sikosei ilikuwa ng'ombe 70 ambao ilibidi wabadilishwe kuwa fedha ambayo kipindi hicho haikuwa ndogo...hapa nazungumzia miaka mwanzoni mwa muongo huu!
 
Jamani naomba nifafanue kidogo,mimi nimetoka kuoa majuzi tu na hayo yamenikuta. Kotoa mahari ni lazima kwa waislam na dini inasisitiza sana kuwa mahari isiwe kubwa kiasi cha kumfanya mtu asioe.

Lakini ukija katika ukweli halisi wa maisha ya leo mambo yanatafautiana kwa mfano mimi nimeoa kwenye familia yente uwezo wa wastan na nimelipa mil.2 kama mahari. Nilipokaa na mcumba wangu nikamuuliza kulikoni? Akanieleza kuwa kuna vitu vya muhimu vya kununuliwa wakati tunaanza maisha na wazazi wake wasinge afford kughramikia harusi pamoja na mahitaji yake ambayo ni ya lazima wakati mke anapohama kwenye makazi yake mapya na mumewe.

Kwa kweli nikamuelewa na nikaona ni sahihi has kwa mila zetu za kiarabu mwanamke anakuwa na mambo mengi ya kufanya.

Ninachotaka kusema hapa kama familia ya mwanamke ina uwezo wa kutosha itakuwa ufisadi ikidai mahari kubwa kiasi cha kufanya mtu ashindwe kuoa.
 
Hivyo mahari ndio inamfanya binti anyanyasike kwa mumewe? Mie nadhani sio mahari, kama ingekuwa mahari ndoa nyingi tu zingekuwa na misuko suko. Asilimia kubwa ya Wanawake wananyanyasika kwa mahari ni wale ambao ni tegemezi kwa mwanaume.
Kama mwanaume una pesa, hata ukipangiwa mahari kubwa mie naona hakuna ubaya, tatizo lipo mtu mwenye kima cha chini kupangiwa mahari kubwa.
Na hawa wazazi/walezi wanaopanga hizi mahari huwa wanafahamu uwezo wa huyo bwana. Kama una dau kubwa na mahari nayo kubwa.
Pretty, nakubaliana na wewe. Kinachofanya mwanamke anyanyaswe kwa mumewe si mahari, ni tabia mbaya tu ya mume au ndugu wa mume wake. Mwanamke hata kama ataolewa bila mahari kama mume wake ana tabia mbaya atamnyanyasa tu: kwa maneno mabovu na vibao juu, na hata kumwambia "una nini cha pekee wewe, ndiyo maana hata sikutoa kitu kwa wazazi wako".
 
Sasa Braza ulizia kuhusu mahari kwa Wahindi (Hindu sect.)

Kwanza unajua kua mwanamke wa kihindi ndiye anaelazimika kutoa mahari? tena ni hela nyingi pamoja na dhahabu, sasa wengi hua hawa afford na wanataka watoto wao waolewe kwa hivyo hutoa ahadi kua watalipa kwa kipindi fulani, inapofika wakati na wazee wa mtoto wa kike wakashindwa, basi hufika mpaka mtoto wa kike akachomwa moto na wakwe (in laws)zake. Na mambo haya yanaendelea mpala leo.

Masheikh wengi au wote wa ki-Islam wanasisitiza kua mahari ni suna tu na makubaliano ya wazee wawili. Utaona watu wameoana miaka mitatu hawajapata mtoto wakifikiri mahari hata tendo la ndoa hua halina ladha.
 
amani kwenu wana JF..
hivi umewah kutafakari hili suala zima la ulipaji mahari origin yake ni nn?!..na ni vigezo gain vinavyotumika ku evaluate thamani ya huyu mwanamke?. Embu fikiria, kitendo cha mwanaume kulipa mahari kina ulazima gani?, ukiangalia kwa makini ni kama mwanamke ananunuliwa vile!, na mtu akinunua kitu huwa anakitumia atakavyo,simply coz ameingia gharama!..jamani huu utamaduni (hii biashara) si unadhalilisha wanawake?
 
acha ubairi mkuu mahari lazima ila aimaniishi unamnunua wife hapana ni just kujikomiti kiaina tu ila baadhi ya familia wamegeuza biashara
 
nimekusoma kiongozi, bt utatumia vigezo gani kukadiria mahari ya binti yako?.huoni ni kama unapanga bei ya bidhaa?

pamoja!!
 
nimekusoma kiongozi, bt utatumia vigezo gani kukadiria mahari ya binti yako?.huoni ni kama unapanga bei ya bidhaa?

pamoja!!

kwakweli vigezo akuna ndomana baadhi ya makabila yanajua taratibu zao kwa ukitaka kuoa unafanya moja mbili tatu japo sikuizi akuna utandawazi umeingilia kati utakuta wazazi wanakaa na binti wanajadili vp tukimtajia kiasi hiki vp sianauwezo kama binti naye anatamaa imekula kwako ila kamaanakupenda nafuu kwako kwani atakinga kifua kwako
 
Hizi sredi zingine tulikua tunajadili tulipokua form two b, lols.
 
kuna jamaa yangu mmoja alinidokeza kuwa akikumbuka mahari aliyotoa kwa mkewe, humrukia kwa hasira kama simba aliyejeruhiwa kum-do kwa sababbu mahari yake inamuuma sana!!!!!!

nafikiri kwa isingizio hiki, wanawake wengi wenye visirani wamebakwa sana na wame zao!!!!!!!!!!!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom