Maharamia wakamatwa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maharamia wakamatwa Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 15, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  WATU sita wenye asili ya Somalia wanaotuhumiwa kuwa maharamia wamekamatwa mkoani Pwani na kukutwa wakiwa na silaha kali za kivita na mabaki ya risasi zilizotumika.

  Miongoni mwa silaha hizo ni magazini moja iliyokuwa na risasi za moto 21 pamoja na maganda mawili ya risasi za SMG na SAR, yaliyotumika.

  Watu hao walikamatwa mara baada ya wananchi waliowaona ufukweni kutoa taarifa ambapo walitiwa nguvuni na Polisi majira ya saa moja usiku wa kuamkia jana katika kijiji cha Kirongwe kata ya Kirongwe wilayani humo.

  Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, wanakijiji wa Kifinge kata ya Baleni, watu hao walionekana majira ya asubuhi kwenye ufukwe wa bahari wa kijiji hicho.

  Walisema hali zao zilionekana kudhoofu kutokana na kukaa muda mrefu bila kula na hata kuashiria kuwa na matatizo ya kiafya.

  "Walionekana wakiwa kwenye boti aina ya Fiber yenye injini ya nyuma huku wakiwa hoi wanaomba msaada wa chakula kwa kuonyesha ishara," alisema mmoja wa wakazi hao kwa sharti la kutotajwa jina gazetini.

  Taarifa hizo zimeeleza kuwa wakati wakiomba msada huo wa chakula, wasomali hao waliiacha fiber Boat yao majini na wote sita walichukuliwa na wanakijiji hadi kwenye zahanati ya Kijiji cha Kirongwe ambapo walipewa huduma ya kwanza pamoja na uji kutoka kwa wasamaria wema.

  Kutokana na hali yao kuonekana kuchoka na kulalamika kuwa wana njaa, wanakijiji hao waliwakirimia chakula lakini wakawa na wasiwasi nao hivyo kulazimika kutoa taarifa polisi ambao waliwatia mbaroni.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Absaloom Mwakyoma, alithibitisha tukio hilo na kuwataja wasomali hao kuwa ni Mohamed Hassan (26), Mohamed Abubakari (19), Mohamed Abdulkarim(21),Abdallah Halid (23), Gibril Abdul(26) na Nuru Ally(19).

  Pamoja na takrima walizofanyiwa na hata polisi kuwatia mbaroni kuilaini, tatizo lililijiyokeza ni lugha ya mawasiliano.

  Watuhumiwa walionekana kutojua Kiswahili wala Kiingireza, hivyo kulipa wakati mgumu jeshi la polisi la kuchukua maelezo yao.

  Alisema baada ya kuwakamata watuhumiwa hao waliwachukua na kwenda nao hadi eneo ilipokuwa fiber Boat na kuanza kufanya upekuzi ambapo katika ukaguzi huo ndani yake walikuta mkoba unaovaliwa kiunoni wenye uwezo wa kubeba magazine tatu za bunduki na ndani yake pia kulikutwa magazine moja ikiwa na risasi za moto 21 ambazo hazijajulikana ni za bunduki gani.

  Alisema aina ya magazine iliyopatikana imeandikwa kwenye kitako Adventure line MFG,Co-Ing Persons, KS, USA na pia katika upekuzi huo walifanikiwa kukuta maganda mawili ya risasi za SMG/SAR.

  Upelelezi wa awali wa polisi, alielezea Kamanda kuwa imeonyesha kuwa watu hao wana dalili zote za kuwa ni maharamia ambao wamekuwa wakiteka meli na kuziachia baada ya kulipwa kiwango kikubwa cha fedha.

  "Sisi tumebaini hawa ni maharamia ingawa kwa mahojiano ya taabu wao wamedai walitokea Mogadishu wakaenda Mombasa kwa lengo la kwenda Afrika Kusini kutafuta maisha, wakipitia Msumbiji," alisema Mwakyoma.

  Hata hivyo Kamanda huyo alisema walipowabana zaidi watuhumiwa hao walidai kuwa awali walikuwa 11 katika Fiber boat mbili ambapo wenzao watano katika boti ya pili walizama baharini na kati yao wawili walipona na watatu walipotea na hawajajua kama wapo hai ama la.

  Kwa mujibu wa Mwakyoma,watuhumiwa hao waliendelea kudai kuwa katika boti iliyozama ndiyo iliyokua imebeba vifaa vyao vyote ambavyo vimepotea na baada ya kuokolewa wenzao wawili walirudi Mombasa na boat yao.

  "Hawa watu tumewabana kweli kweli na ndipo walipotueleza hayo yote na hili la kukaa baharini siku nne bila kula chakula na ndiyo sababu wamelazimika kujisalimisha katika kisiwa cha Mafia," alisema na kuongeza:

  "Napenda kusema kuwa hili bado ni tete hasa kwa kukamatwa na magazine na risasi zote hizo, maganda ya risasi zilizotumika ndani ya boti yao hiyo, inatia shaka kuwa hawa ni maharamia," alisema Mwakyoma.

  Watuhumiwa wote sita na vielelezo vyao hivyo vinashikiliwa na kwamba Polisi bado wanaendelea na upelelezi.

  Tukio hilo limetokea wakati juhudi mbalimbali za kimataifa za kukabiliana nao katika ukanda wa Bahari ya Hindi ukiendelea.

  Pamoja na kuwepo kwa jeshi la umoja wa mataifa katika eneo hilo la pwani ya Afrika, inayopakana na bahari ya hindi, bado maharamia hao wa kisomali wameendelea kuteka meli na kulipwa mabilioni ya fedha ili kuziachia.

  Hali hiyo imevuruga kwa kiwango kikubwa safari za meli kupitia ukanda huo wa bahari kuingia au kutoka pwani ya Afrika Mashariki.
   
 2. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #2
  Jan 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  haba na haba hujaza kibaba ndio wameanza taratibu baadae wakiongezeka amani itatoweka bongo
   
 3. Ikimita

  Ikimita JF-Expert Member

  #3
  Jan 15, 2011
  Joined: Oct 23, 2010
  Messages: 302
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hawa sio watu wa kuonea huruma. Inabidi wapewe sifongo badala ya chakula!!
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Jan 15, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,496
  Likes Received: 19,900
  Trophy Points: 280
  akili kumkichwa
   
 5. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #5
  Jan 16, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  kwangu imegoma kuchakachua....hebu nichakachulie
   
 6. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #6
  Jan 16, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Ni wale wale wa ile deen ya upendo na amani.
   
 7. Mauza uza

  Mauza uza JF-Expert Member

  #7
  Jan 16, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 2,068
  Likes Received: 785
  Trophy Points: 280
  Hebu acha ujinga ..hivi huwezi kukaa kimya zaidi ya kutukana dini ya watu??FYI Somalia ni muslim country 150%.Hovyooooo.
   
 8. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #8
  Jan 16, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160

  Haya majina nikuyaogopa km ukoma
   
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  Jan 16, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,496
  Likes Received: 19,900
  Trophy Points: 280
  mmm!! Dear mary ..majina sio kitu kwa sababu wengi ni wazuri zaidi ya % 99 ni wazuri na tunaishi wote , labda kama unafanya kazi kwenye embassy ya USA
   
 10. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #10
  Jan 16, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Lazima hawa wanajuwana na Mh Kinana!
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  Jan 16, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,496
  Likes Received: 19,900
  Trophy Points: 280
  ahahha !! wajomba zake
   
 12. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #12
  Jan 16, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  walikuwa wanakuja kuajiriwa paradise hotel,city garden na tansoma hotel
   
 13. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #13
  Jan 16, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,496
  Likes Received: 19,900
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 14. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #14
  Jan 16, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  wa tz, safari ya kufika kwenye uelewa na uhodari ktk upelelezi bado ni ndefu, nikawaida kila unapokutana na wanauslama wetu there is no qn wewe tayari ni mharifu na unaanza kupata mukwaju. Ni vema tukaelewa kuwa Kwa msomali awe mwema au mharifu kutembea na ak47 ni sawa na masai kutembea na sime. Kutangaza kuwa hawa waliokamatwa ni maharamia baada ya mahojiano mafupi inaonyesha ni kiasi tuanadhani kila msomali ni mteka mali. Ni vema tukajua kuwa pirates wa kisomali ni matajiri sana hivyo hawawezi kukosa chakula baharini.
   
Loading...