Maharamia wa wake za watu tuwafanyaje??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maharamia wa wake za watu tuwafanyaje???

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Apr 24, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,272
  Likes Received: 5,635
  Trophy Points: 280
  Jamani kumekuwa na wimbi la ajabu ama laana ama ....mhhhh sijui waua kuamua kutooheshimu kabisa ndoa na kuamua (WANAUME) kullala na wake za watu...wanawake kulala na WAUME za watu....tumekuwa tukiamini maharamia ni wale tu wa somalia baharini lakini ni vyema nguvu tunazozipeleka uko tujaribu kujua jinsi ya kukomesha uharamia wa wake za watu
  yawezekana ni tamaa;Dawa yao tuwafanyaje watu kama hawa????
   
 2. Scientist

  Scientist JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni hoja nzuri sana hii lkn naona ungeiweka kule kunako mapenzi na mahusiano ndio ingekuwa vema zaidi, tuijadili kwa kina.

  MODS mpoo?
   
 3. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Dawa ya mke/mume anaetokatoka nje mpe ruksa aende mojakwa moja. Hakuna haja yakutafuta ugomvi usio na maendeleo.

  ''Mod peleka kuleeee kwenye mahusiano hii''
   
 4. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #4
  Apr 24, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 135
  Mumeo/ mkeo akiamua kugawa nje, kosa sio la mlaji, hadi mwandani wako akubali kugawa nje basi ujue ndani kuna mapungufu na ni juu ya wanandoa kubainisha na kutafutia ufumbuzi mapungufu waliyonayo ili pasiwe na mwingine wa kuingilia mapenzi yao.
   
 5. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #5
  Apr 25, 2009
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,043
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Kana Ka Nsungu,
  Unadhani inawezekana kweli hapa duniani kumwambia mwenzi wako, baada ya wewe kutoka nje na yeye kujua, kwamba - unajua kuna mapungufu fulani unayo, nadhani tuyaongelee ili mimi nisitoke tena nje ya ndoa.......nk nk nk? Never!
   
 6. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #6
  Apr 25, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 135
  Kama mnaelezana mapungufu yaliyopo bila woga,kutakuwa hakuna sababu ya kutoka nje.
   
 7. S

  Sally Member

  #7
  Apr 28, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ni kweli kabisa mapungufu ndani ya ndoa ndiyo yanayosababisha mke/mume kutoka nje. Unajua kule nje wanakokimbilia dayworker wanakuwa hawana majukumu. Wanazungumzia issue moja tu.Ila nyumbani unakuta kuna issue mara ya watoto mara hivi sasa wanaotoka nje ni kuwa wanajaribu kukwepa na kukubali majukumu yao
  Wanaume
  Tuwapende wake zetu, tuwasaidie, tuwashauri, tuwaite majina mazuri angalau kama tunavyofanya huko nje, tuwasikilize, tuwe na muda wa kuwa na wenzi wetu ( quality time), tutimize wajibu wetu, tuwe wawazi

  Wanawake
  Tuwaheshimu na kuwatii waume zetu, tusiwe na gubu nyumbani, tutimize wajibu wetu, tuwe wawazi
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  Apr 28, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Badili title yako haendani na kiini cha unachotakwa kijadiliwe....Maharamia wa wake za watu tuwafanyaje??? nadhani ungeeleweka vizuri iwapo ungesema maharamia wa ndoa...hapo uko imapartial as if ni tatizo kwa wanaume tu...
   
 9. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #9
  Apr 28, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Hey flag up! mama mia!
   
 10. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #10
  Apr 28, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,272
  Likes Received: 5,635
  Trophy Points: 280
  nafikiri tatizo kubwa sasa hivi watu wengi wanaoa kutokanaa na mawazo tofauti;wapo wanaoooa ama kuoana kutokana na umri kuwa mkubwa...wapo wanaooana kutokana na kweli wote wanapendana vilivyo.,wapo wanaooana just kwa sababu mmoja wao ametoka kwenye frustration za nguvu na kuona soln kuoana....,wapo wanaoooana hawa tunawaita kutokana na upendo wa AGAPE both side...sasa basi unakuta mmoja wao ama wote wakifshafanikisha malengo yao ya kuoana mtu anaamua bull shit ngoja kama kuoa nimeshaoa ama kuolewa ngoja nile maisha...mi nina frame pic ya ndugu yangu mmoja kama sio kumfwata mungu sijui angekuwa wapi......
  huyu aliamua kuoa mwaka 2005 bada ya kuwa na gfrienda wake miaka miwili akapata ujauzito binti kabla ya uja...akabadilika kidogo then wakaitana chini kama mambo ndio haya maisha kusonga mbele kwa nini tusidisaidi mapema....mwanamke akazima simu akabadilisha chipu kila akifwatwa anaambiwa na nduguze hayupo...baadae akaja mwanamke analia sana akaomba msamaha...baada ya wiki kama mjuavyo wanaume walivyo weak kwa madada...akarejesha moyo konde maisha yakaanza baada ya wiki ati ana mimba.....mmmmh???jamaa akacheza nayo ilipofika mwezi akaomba wakapime mimba yao..mwanamke akagoma kabisa kabisa....mpende mamayako kwanza huu ni ujumbe mfupi uletwao kwenu na Mama Mia...then tunaendelea...baada ya mwezi na nusu mwanamke akaamua kuwasha moto kwamba ikifika siku fudenge basi mi ntakuwachia ujue cha kufanya kama utaki tukapime...kumbe yule mwanamke mungu nawaambia ni wa ajabu....akanyanyuka akaenda hospital moja kinondoni...akapima mwenyewe jibu alilopata ni yeye na mungu yake mimba ilikuwa na miezi miwili na nusu...mwanamke akapata mimba ya pili...ya ukichaa..akarudi nyumbani hoi..mwanamme gafla akawa mwanmke akaenda kusachi kwenye pochi...yalaaaaahhhhhhhhhhhhhhhh
  msg ikawa copied kaka wa watu akaamua kuhama siku hiyo na kitanda chake akamwachia mwanamke kila kitu....baadae mwanamke akaenda kutoa ile mimba...jamaa akapata mwanamke mmoja wakiwa harusini kwa wajombweze....wakapendana miezi sita wakaooana harusi kubwaaaa diamond jubilee gafla.......,baada ya mwezi wa tatu binti kaanza kunywa pombe za ajabu...hee jamaa akaona mungu ampendi na kuanza kuomba ushauri jamani nifanyeje....mwanamke akaamua kusafiri kwenda nje ya nchi kumbe anamfwata bwana wake....loh!!!!akatokea msamaria mwema rafiki mkubwa wa huyo mwanamke akamfwata bwanaharusi na kumwambia pole sana we ni kama nduguyangu..., mkeo tuko nae kila siku ana bwana nje anaitwa fulani yuko holland muda wote wanawasiliana si kama marafiki tulimshauri usiolewe kama hujawa tayari......,mungu amrehemu dada yule sasa ni marehemu...alikuwa CELTEL...baadae wakaachana kabisa mahakamani kila mtu akala zake..ndoa ikadumu miezi 3.....kwa hiyo ndoa si ya kukimbilia sababu mnamaisha bora jiulize pesa zikikata pendo litakuwepo....nawachia JF....
   
 11. H

  Haika JF-Expert Member

  #11
  Apr 28, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Maharamia huwezi kuwafanya chochote, we hangaika na ndoa yako.
   
 12. Outlier

  Outlier JF-Expert Member

  #12
  Apr 28, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Maisha ndivyo yalivyo, kubali yaishe - there nothing anybody can do about it. Mnapiga soga tu!
   
 13. S

  Superstar Member

  #13
  May 8, 2009
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pdidy, Thank you for the good message. There are a lot of success and failure stories to be shared in regards to marriage. lakini mimi mwenyewe naona kama sisi wanawake ndani ya ndoa - we are like slaves. Haki ya mungu hata hiyo busu unaweza kukaa hata mwaka hujaipata. Acha busu hata kukuita jina la mapenzi tu - Like Honey, Darling, Sweet heart etc. hakuna. Sasa ukipata mshikaji akakuiita Darling with a kiss so utahamia kabisa. Kutoka nje siyo kosa- kosa ni kufumaniwa! Tunakosa mengi ndani ya ndoa.
   
 14. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #14
  May 8, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  you sound like the haramia.... haha
   
 15. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #15
  May 8, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hili darasa lipo mahali sio pake kwa hiyo wengine tutashindwa kutowa maoni yetu kuna mengi yakuchangia juu ya hili.
   
Loading...