Maharage Chande: 2 Februari 2022 Transforma mpya inayofungwa katika kituo cha kupooza umeme cha Kunduchi kuwashwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,969
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika Shirika la Umeme Tanzania TANESCO , Maharage Chande amesema Februari 2 mwaka huu wanatarajia kuanza kuiwasha Transforma mpya inayofungwa katika kituo cha kupooza umeme cha Kunduchi baada ya kukamilisha matengenezo yake

Akizungumza leo Januari 31,2022,baada ya kutembelea kituo hicho amesema Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limefunga Transfoma hiyo ili kuondoa baadhi ya changamoto zilizokuwa zinajitokeza kwa wateja kupata usumbufu wa kukatikakatika kwa umeme
20220131_174153.jpg
20220131_174156.jpg
20220131_175342.jpg
20220131_183418.jpg

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika Shirika la Umeme Tanzania TANESCO ,Maharage Chande akizungumza na waandishi wa habari katika kituo cha kupozea umeme cha Kunduchi mara baada ya kukagua ufungaji wa transformer unaoendelea kituoni hapo
 
Kichwa cha habari kinasema "transfoma mpya inayofungwa", lakini habari yenyewe inasema "baada ya kukamilika matengenezo yake" sasa hiyo transfoma ni "mpya" ya aina gani?!

Hebu tulieni huko Tanesco mfanye mambo yenu kwa utulivu, naona mna pressure sana.
 
Sasa hyo transfoma n mpya au n ya zaman imefanyiwa repair

Mbona mnatuona watanzania Kama mabwege Sana tusiojua kusoma

SWALI hyo transfoma n mpya au ya zaman?

Kama mpya matengenzo n ya nini?

Bwana NJEGERE CHANDE shirika litakushinda hili

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Kichwa cha habari kinasema "transfoma mpya inayofungwa", lakini habari yenyewe inasema "baada ya kukamilika matengenezo yake" sasa hiyo transfoma ni "mpya" ya aina gani?!

Hebu tulieni huko Tanesco mfanye mambo yenu kwa utulivu, naona mna pressure sana.
Hawajui wanachofanya wapo hapo kubangaiza na kusuka hujuma kwa Taifa.
Nani alimfanyia usairi wa hiyo nafasi huyo Maharage? Kurusha vipindi vya tv DSTV mpaka kuongoza shirika kubwa kama TANESCO wapi na wapi?
Kumuajiri bila ushindani kunaonesha wazi kuwa ameletwa hapo kwa lengo maalum!!
 
HII NCHI INA watu ndezi kweli......ngoja tusikilizie.....MIHEMKO...
 
Back
Top Bottom