Maharagande: Naibu Waziri TAMISEMI Ajiuzulu

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
608
1,540
Utata kifo cha Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM); Naibu Waziri-OR TAMISEMI ajiuzulu kupisha uchunguzi.

Utangulizi
Chama cha ACT Wazalendo kimepokea kwa masikitiko makubwa juu ya kifo chenye utata cha aliyekuwa Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma akisomea shahada ya kwanza ya Sanaa katika Elimu (BA.Ed) Nusura Hassan Abdallah. Utata wa kifo cha Nusra unatokana na taarifa zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii zikihusianisha kifo hicho na ajali iliyotokea Dodoma tarehe 26 April 2023 ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Baada ya mjadala wa siku zaidi ya wiki moja, juzi tarehe 05, Mei 2023 taarifa ya Uongozi wa Chuo cha Dodoma ilithibitisha kifo hiko na kuelezea kuwa Nusra amefariki akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Faraja iliyopo Kilimanjaro.

ACT Wazalendo tunaona wazi kuna utata juu ya chanzo cha kifo hiko; hasa taarifa zake zimekuwa na mkanganyiko mkubwa na wenye sura mbili; Mosi, kuwa kifo hiko kimetokea pamoja na ajali iliyomkuta Waziri wa TAMISEMI Dkt. Festo John Dugange (Mb) usiku wa kuamkia tarehe 26 April 2023. Ambapo awali kabisa taarifa katika mitandao ya kijamii zilieleza kuwa katika ajali hiyo pamoja na Waziri huyo kulitokea kifo cha mwanamke aliyekuwa ndani ya gari ya Waziri lakini taarifa za mwanamke huyo hazikufahamika.

Baada ya siku tatu, Jeshi la Polisi kupitia kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno (ACP) alieleza kuwa kwenye ajali hiyo hakukuwa na kifo chochote zaidi ya majeruhi ambaye ni Dkt. Dugange.

Pili, taarifa zinaonyesha kuwa kifo hiko kimetokea Kilimanjaro na kutaja chanzo cha kifo ni ugomvi wa kimapenzi. Sura hii ya pili inaonyesha kuwa ni hoja zinazotumika kuficha ukweli baada ya msukumo mkubwa wa watu kuulizia ukweli wa kifo hiko.

Kwasababu inaacha maswali megi sana, haiwezekani kwa Chuo kuchelewa kwa muda wa wiki nzima kupata taarifa za kifo cha mwanafunzi wake. Aidha, kitendo cha Jeshi la Polisi Dodoma kukaa muda wa siku tatu bila ya kutoa maelezo ya ajali ya Naibu Waziri TAMISEMI inaonyesha kuna usiri mkubwa. Vilevile, taarifa ya Uongozi (Menejimenti) wa UDOM inachukua upande mmoja unaojaribu kuonyesha kuwa kifo hiko kimetokea Kilimanjaro.

Sisi ACT Wazalendo kutokana na utata wa chanzo cha kifo cha Nusra Hasan Abdallah na ushiriki wa baadhi taasisi (Jeshi la Polisi, Chuo Kikuu cha Dodoma na Wizara) kwenye kuzalisha taarifa zenye mkanganyiko zaidi. Tunataka hatua zifuatazo zichukuliwe;

i) Tunamtaka Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Festo John Dugange ajiuzulu kupisha uchunguzi.

ii) Serikali iunde Tume huru ya kuchunguza suala hili kwakuwa uchunguzi utakaofanywa na Jeshi la Polisi umeshakuwa na doa kutokana na ushiriki wao kwenye hatua za awali za kuficha ukweli wa taarrifa za kifo hiko.

iii) Tunataka hatua zichukuliwe kwa wahusika wote ikibainika kuna jitihada za kuficha ukweli.

Imetolewa na;
Ndg. Mbarala Abdallah Maharagande
Twitter: @Mbaralagande
Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani.
ACT Wazalendo.
07 Mei, 2023
 
Utata kifo cha Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM); Naibu Waziri-OR TAMISEMI ajiuzulu kupisha uchunguzi.

Utangulizi
Chama cha ACT Wazalendo kimepokea kwa masikitiko makubwa juu ya kifo chenye utata cha aliyekuwa Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma akisomea shahada ya kwanza ya Sanaa katika Elimu (BA.Ed) Nusura Hassan Abdallah. Utata wa
ACT Wazalendo.
07 Mei, 2023
Taarifa mbona haina utata vyombo vyote vilivyotakiwa kutoa taarifa vimetoa taarifa.Hizi taarifa za mitandaoni ndo zina utata
 
ii) Serikali iunde Tume huru ya kuchunguza suala hili kwakuwa uchunguzi utakaofanywa na Jeshi la Polisi umeshakuwa na doa kutokana na ushiriki wao kwenye hatua za awali za kuficha ukweli wa taarrifa za kifo hiko.
Tayari inajijua
 
Baada ya mjadala wa siku zaidi ya wiki moja, juzi tarehe 05, Mei 2023 taarifa ya Uongozi wa Chuo cha Dodoma ilithibitisha kifo hiko na kuelezea kuwa Nusra amefariki akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Faraja iliyopo Kilimanjaro.
Tena kwa kupigwa na mpenzi wake ambaye jina lake halikutajwa wala kujulikana ni wa wapi
 
Waziri ajiuzuru kwanini kwasababu mtu kafa mbona kilasiku watu wanakufa hoja nini
 
Back
Top Bottom