MAHANGA umewafanyia nini jimbo lako la Ukonga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MAHANGA umewafanyia nini jimbo lako la Ukonga

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by HM Hafif, May 17, 2010.

 1. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2010
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Leo asubuhi 17 may 2010 nilitoka nyumbani kwangu kariakoo saa 12.10 kuelekea tabata Segerea kumpeleka mtoto wangu shule ya Tusiime iliyoko Sanene Segerea mara baada ya kuchwa na gari la shule.


  Nilitumia kiasi cha dkk 45 tu kufika huko. Lakini nilipoanza safari ya kurudi mjini tena ilinitumia zaidi ya masaa mawili kufika kariakoo.

  Nimesikitika sana kuona jimbo hilo la aliyewahi kuwa NAIBU WAZIRI MIUNDOMBINU kuwa na miundo mbinu mibovu sana na hata kusababisha foleni kubwa sana kuanzia eneo la tabata Posta mpaka kufika barabara ya mandela.

  Sasa najiuliza Je mbunge huyu anaishi huko Segerea?
  Je anatoka saa ngapi kwenda kazini?
  Jitihada gani kama mbunge na zaidi naibu waziri anazozichukua kuepusha faleni hizo?
   
 2. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #2
  May 17, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mahanga hana historia yeyote ya utendaji na kwa bahati mbaya anatarajia kugombea na kuchaguliwa tena kuwa mbunge wa segerea (jimbo jipya ).

  Kama mkazi wa Tabata naomba tuchague mabadiliko kwa sasa. tuwapime wagombeaa kutokana na rekodi yao ya utendaji kuanziaa wanapoomba kugombeaa kwenye vyama vyao mpaka uchaguzii kwa wananchi..

  MABADILIKOO UBUNGE SEGEREA/UKONGA KWA MASILAHII YA MAENDELEO.
   
 3. k

  kisikichampingo Senior Member

  #3
  May 17, 2010
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 129
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kama wana-Segerea/Ukonga mnataka mabadiliko. Msipige kura zenu halafu mkatokomea kwenda ulevini. Kaeni vituoni mlinde kura zenu ili Sisiem wasiibe. Fanyeni kama wana Tarime walivyowadhibiti akina Makamba kwa kulinda kura zao hadi mwisho
   
 4. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #4
  May 17, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Bora nyie mmeliona hilo. Hofu yangu ni je? wananchi wengi wanajua hilooo. Au wanafurahia kupewa kanga ,kofia na Tshirts tu na kubaki wakishangilia na kupoteza kura zao kwa kuchagua watu wasiofaa.
   
 5. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #5
  May 17, 2010
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wananchi lazima wajue umuhimu wa kura zao
   
 6. H

  HusseinMgumba New Member

  #6
  May 17, 2010
  Joined: May 17, 2010
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dah,afu huyo mjamaa ni Waziri......na eti inasemekana ni mshkaji wake jamaa na alikuwa akimtafutia vidosho basi ndo akapewa ka jift box hako...ka u waziri.
  kazi kwenu wana ukonga/segera......................
   
 7. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #7
  May 17, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Jamani mnaniumiza sana maana Makongoro ni Tapeli wala sio uongo sasa hivi ameshaanza kukutana na wazee wa serikali za mitaa ndio approach yake kila kipindi kuwaomba msamaha wale na kupitisha grader kwenye bara bara. Yule jamaa bungeni kazi yake ni kutetea mafisadi tu. Mimi nakaa ukonga na nimejiandikisha ili nimnyime kula yangu tu. Fisadi wa elimu yule harafu atakuwa anatudharau ngoja ashangae mwaka huu.
  Ni muongo akiwadanganya watu wanaelewa alikuja siku moja anawaambia watu wa Mombasa kuwa bara bara hii inatengenezwa kwa kiwango cha lami baadae kasema watu wa barabarani wamekataa kujenga hizi pesa nimepeleka banana kujenga bara bara ya kule. Mimi nikajiuliza kwanza hivi vitu vilikuwa discussed wapi, kama ni bungeni yeye hana uwezo wa kubadili mpaka bunge lijadili tena na sio sababu mtu wa bara barani kukataa. serikali imevunja kipawa ije ishindwe nyumba mbili mombasa??
   
 8. Kabuche1977

  Kabuche1977 JF-Expert Member

  #8
  May 17, 2010
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Duh!!! ahaaaaaaaaa, juzi juzi nilimuliza brother angu anakaa ukonga kuhusu huyo jamaa, toka amechaguliwa hajawahi hata kwenda kuwasabahi wanacommunity ya ukonga, wala hajui kama kuna matatizo ya barabara, kama we mkazi wa huko angalia barabara toka mombasa kwenda moshi bar mpaka kule chini wanakuita kwa diwani---ukiwa na saloon car huwezi pita, sasa hiyo Dar mikoani je?? watu kama akina mahanga ni kuwatosa tu, hatufai hata kidogo kwenye kizazi hiki cha nguvu kazi na maendeleo-------wakati wao umepita, sometimes old is not Gold------------inakuwa nikel au lead.
   
 9. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #9
  May 17, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  John Second Hongera kwa uamuzi wako wakishujaa
   
 10. D

  Dina JF-Expert Member

  #10
  May 17, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Nasikia ametangaza/onyesha nia ya kugombea tena! Hivi anagombea jimbo la zamani au jipya? Manake upande wa hilo jipya alishasema hatahangaika na huko (kabla ya kumegwa) kwa kuwa chaguzi zilizopita hawakumpa kura (kwa sababu hakutimiza ahadi zake hasa barabara ya mombasa - moshi bar)! sasa atakuwa na ujasiri (mmh ila huwa hawaukosi) wa kurudi kuomba kura tena?
   
 11. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #11
  May 17, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Tatizo ni maswahiba wa Kikwete wote upupu, sasa kaona jamaa ana hali mbaya kagawa yamekuwa majimbo mawili ili amnusuru waendelee na ka biashara kao alikosema HusseinMgumba.
   
 12. d

  damn JF-Expert Member

  #12
  May 17, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 585
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  FISADI MMOJA MIAKA YA 1980s ALIWAHI KUSEMA, MIAKA MITANO YA KWANZA HUWA YA MBUNGE, MITANO INAYOFUATA NI KWA AJILI YA KULISHA WAPAMBE NA WANAOMWEZESHA KUWA MBUNGE, MITANO YA KIPINDI CHA TATU NDIYO WANANCHI HUANZA KUFIKIRIWA. SASA WANA UKONGA WACALCULATE WENYEWE....NA UKIZINGATIA NI TAPELI MAHANGA. KAZI IPO!!!
   
 13. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #13
  May 18, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Huyu ni Mjaluo fake !Sijaona Mjaluo anafake Phd kama huyu!Kwa sababu Tanzania ni mambumbu wengi,huyu atapita tu!May be 98 % ya wapiga kura wa jimboni hawajui hata Phd fake nini.
   
 14. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #14
  May 19, 2010
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha sana. Poleni sana wa jimbo lake ila mnatakiwa mjue HATIMA YAKE YA KURUDI TENA BUNGENI IPO MIKONONI MWENU. Jitokezeni, jiandikisheni na nendeni mkapige kura kutimiza haki yenu ya kidemokrasia ya kuchagua viongozi wenu.
   
 15. masharubu

  masharubu Senior Member

  #15
  May 19, 2010
  Joined: May 5, 2010
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wana JF haya ni malamiko niliyadokoa sehemu ya wakazi wa ukonga ambako MAKONGORO ndie mbunge wao, hivi hata pesa za kuweka mafuta greda la manispaa hakuna? Pesa wanazokusanya ushuru ktk maziziz wanapeleka wapi? sehemu ya dakika 5 unatembea nusu saa, si diwani si mbunge anaejali,ama kweli CCM ina wenyewe


  TUNAMUOMBA MUNGU AWAPE MIOYO YA HURUMA VIONGOZI WA MANISPAA YA ILALA na MAHANGA.

  Ninaandika kwako kutoa dukuduku langu kwa viongozi wetu wa Manispaa ya Ilala. Mimi ni mmoja wapo wa wakazi wa Ukonga Mombasa.

  Ni muda mrefu sana tumekua na kilio cha ubovu wa barabara yetu ambayo kwa muda mrefu imeachwa kama motto yatima wakati barabara nyingine pacha kama za Kitunda na Kinyelezi aidha zimetengenezwa kwa kiasi Fulani cha lami au zimekua zikichongwa na kuwekewa vifusi mara kwa mara.

  Tunamuomba Mwenyeezi Mungu awape mioyo ya huruma viongozi wetu watukufu nikianzia na Katibu mtendaji wa kata, Diwani, Meya, Mbunge, Mkurugenzi wa Manispaa, Mhandisi wa Manispaa na viongozi wote wanaohusika katika ufatiliaji na ukarabati wa barabara husika.

  Hivi ni kweli hata kupitisha tingatinga inashindikana? Ni vipi wananchi hatuelezwi hatua yeyote kuhusiana na ukarabati wa barabara hiyo? Chakusikitisha ni kwamba mnamo tarehe 02 mwezi wa Tisa 2007 walikuja watumishi wa Kampuni ya ujenzi ya KAJIMA na kijiko cha kuchimbia mashimo ambacho walitumia kukwangulia barabara kipande cha urefu meta takiribani mia na hamsini tu na hakuna kilichofanyika zaidi ya kuzidi kuiharibu, au waliku wana msafishia njia Mheshimiwa mmoja Mtumishi wa Wizara ya Miundo mbinu ambae anakaa meta chache kutoka barabara kubwa? Hii sio rushwa?

  Ni kweli bajeti ya kukarabati barabara hii ya ukonga mazizini haijatengewa pesa kwa kipindi cha miaka mitano sasa? Naona umefika wakati kwa wazee wa TAKUKURU watutetee wanyonge sie walau kwa kwenda kuchungulia na kukagua vitabu vya mahesabu ya Manispaa ya Ilala kujua kama kweli bajeti ya barabara hiyo haijatengwa, na iweje itengwe ya kukarabati kinyelezi mara kwa mara na huku isiwepo wakati wote tupo jimbo moja, ama ni kwa sababu Mheshimiwa Mbunge ndiko kwenye makazi yake? Na kama kuna mis allocation of fund, tunaomba tuelezwe ni vipi pesa hizo zipelekwe katika sehemu nyingine ilihali nasie ni walipa kodi na tuna hitaji kugawana hako ka SUNGURA kwa kuletewa maendeleo.

  Kwa kifupi barabara hii ni moja wapo ya barabara ambazo waheshimiwa hao naona wanampango wa kuja kuigeuza shamba la migomba, haya na waje maana mashimo yapo ya kutosha. Ni mwaka umepita sasa tokea Mheshimiwa Makongoro Mahanga (MB) alipotamka ya kuwa barabara hiyo itatengenezwa karibuni. Tunakuomba Mheshimiwa uachane na ziara za Mikoani kwenye zomeazomea na uje walau uone kwa macho yako na utueleze kinachoendelea kwa watendaji wako.

  Tulipokea habari hizo kwa shingo upande kwani si maneno ya leo huwa mara kwa mara tunaambiwa vivyo, pamoja na hayo cha kujiuliza hivi ni kweli barabara hiyo haijapangiwa pesa ya kukarabatiwa kwa mwaka wa tano sasa? Cha aibu ni pale mwaka juzi kipindi cha kampeni waheshimiwa hao walikwenda Uwanja wa ndege na kuchukua lami iliyotolewa katika barabara ya kukimbilia ndege na kuja kuiweka katika maeneo machache hata hivyo ni aibu kwani walichofanya ni kama wamechukua limao na kusafishia shaba katu haiwi dhahabu. Diwani wetu upo wapi?Meya wa Manispaa ya Ilala upo wapi? Ahadi zenu tamtam zipo wapi?Tumechoka kutoa pesa za kusomesha watoto kwa kutengeneza magari.

  Hivi ni kweli hakuna hata greda la kuja kuchonga hii barabara wakati tukisubiri hayo matengenezo makubwa? Mbona ya kuvunja vibanda vya walalahoi yapo?hata mgonjwa wakati anasubiri upasuaji mkubwa hupewa panadol ili apunguziwe maumivu.

  Namalizia tena kumuomba bwana Mungu alie hai awape mioyo ya huruma na mtutengenezee barabara hiyo.
   
 16. Homo Habilis

  Homo Habilis Senior Member

  #16
  May 19, 2010
  Joined: Jul 2, 2009
  Messages: 189
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mmeumia.!
  huyo aliahidi kujenga daraja maeneo yetu lakini alipopata ubunge mpaka leo hii hakuna cha daraja wala mataruma ya kuvukia.!
  nakusaushi tu kama mkiwa jumuiya moja jipangeni kwa kaya mjitengenezee hiyo barabara mkisubiri huyo muhanga hawezi kujitoa muhanga.
  viongozi kama hawa wabinafsi sio wa kuwapa madaraka kabisa yaani uchaguzi ujao fagieni hizo taka taka zote mzichome moto msije mkapaka chokaa msimu wamvua itatiririka na maji yooote kisha ubakie uchafu usiopendeza machoni.
   
 17. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #17
  May 19, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  haya kila mahali ni kilio. havi nyie mafisadi mnafikiri mungu yuko usingizini.mwaka huu lazima kieleweke .wanaukonga hata aende jimbo gani fagieni
   
 18. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #18
  May 19, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  huyoo Mahanga jamanii hana jipyaa kwanii hana rekodii yan utendaji zaidi ya utapelii, wizi, na ubadhirifuuu uliokithiriiii..jamaa kwa kweli hana hata heshima ya kuwa kiongozii wa jamii achiliaa mbali uwezo wake mdogoo wa utendajii..

  Mimi kama mdau wa ukonga/segerea naomba tujadilii kama kuna wagombeaa imara wanaowezaa kutuvushaa katika bunge lijalo kutoka chama chochotee..

  Vipi yule Kessy wa Tabata ameonyeshaa nia ya kugombeaa?? nakumbuka alipambana na mahanga vipindi vilivypita ila huangushwaa na rushwaa inayotolewa na mahanga na wapambe wake (dk masaburi) na viongozii wa ccm wilaya ya ilala ambao ni vibaraka wa Mahanga..
   
 19. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #19
  May 25, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nyi pigeni kelele sisi huki huy jamaa yumo katika list ya watu ambao tutahakikisha kuwa hapiti sio kwa kuandika humu ila kwa vitendo. Huyu alishaapa kuwa watu wa segerea na kinyerezi kuwa hatawaletea kitu akiwa anategemea kupata kupitia wale watu wa mayai. sasa cha ajabu ni kuwa amewatosa na kuja huku nadhani amekata tamaa.Huku apati labda aje aokolewe na CCJ
   
 20. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #20
  May 25, 2010
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  kaiz kwenu kwani KURA ZENU NDIO JBU LA YOTE
   
Loading...