Mahanga kaanza je ndiyo mwanzo wa ukweli kujulikana zaidi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahanga kaanza je ndiyo mwanzo wa ukweli kujulikana zaidi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lunyungu, Oct 26, 2009.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Waziri Mahanga akimbilia mahakamani kudai fidia ya Sh3bilioni

  Na James Magai
  10/26/2009


  NAIBU waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana Dk Makongoro Mahanga amemshtaki mkazi wa jijini, Kainerugaba Msemakweli pamoja na gazeti la Nipashe akidai fidia ya Sh3bilioni kwa madai ya kumkashifu.

  Mbali na Msemakweli ambaye ni mdaiwa wa kwanza na Nipashe (mdaiwa wa tatu), wengine walioshtakiwa katika kesi hiyo ya madai namba 145 ya mwaka 2009 ni mwandishi wa habari wa gazeti hilo Muhibu Said, ambaye ni mdaiwa wa pili na Kampuni ya The Guardian Limited, ambayo ni mdaiwa wa nne.

  Katika hati yake ya madai iliyowasilishwa na wakili wake Kenedy Fungamtama, Mahanga anadai kuwa alikashifiwa na washtakiwa hao kuwa ameghushi vyeti vya shahada ya uzamivu.

  Kwa mujibu wa hati hiyo mdaiwa wa kwanza (Msemakweli) anadaiwa kuitisha mkutano wa waandishi wa habari Oktoba 18 mwaka huu na kutoa taarifa kwamba amefanya uchunguzi na kubaini kuwa Makongoro hajawahi kusoma shahada hiyo wakati wowote na mahali popote duniani.

  Mdaiwa wa pili, wa tatu na wa nne wadaiwa kuandika, kuchapisha uongo na kwa nia mbaya taarifa hiyo iliyotolewa na mdaiwa wa kwanza katika ukurasa wa mbele wa gazeti la Nipashe, toleo la namba 05443 la Oktoba 19, ikiwa na kichwa cha habari "Vyeti vya Elimu: Mawaziri sita wanasa"

  Habari hiyo iliambatana na vichwa vidogo vya habari kuwa vyeti vyao vya elimu vyadaiwa kuwa na mushikeli. Yumo mkuu wa mkoa na wabunge watatu; Orodha yawasilishwa kwa spika wa Bunge.

  Mahanga anadai katika hati hiyo kuwa taarifa hizo zilishusha heshima ya mlalamikaji katika jamii na kwamba kutokana na nafasi yake kama naibu waziri na mbunge imemuathiri kisaikolojia. Mlalamikaji huyo anaiomba mahakama iwakemee wadaiwa kwa hatua hiyo na kuwaamuru wamlipe fidia ya Sh3 bilioni au kiasi ambacho mahakama itaridhika nacho, lakini kisichopungua Sh200,000, gharama zote za kesi, kuwaagiza kuomba radhi kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti hilo, kuzuia wadaiwa na wakala wao kurudia kuchapisha na kusambaza habari hiyo au habari yoyote kuhusiana na mlalamika huyo
  .
   
 2. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  That's what's up!

  Anikeni data tuchambue pumba na mchele.
   
 3. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  How about if its justified truth...Mahanga si utaaibika?
   
 4. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Ndiyo maana sasa nauliza kwamba ndiyo mwanzo na mwisho wa ukweli juu ya watu kughushi ? Je wale ambao walitajwa wamekaa kimya inakuwaje ? nakumbuka rais alisha ambiwa mara nyingi lakini alifikia mahali pa kusema akiwa mwanza kwamba kelele za mlango haziwezi kuizuia CCM means alikubaliana na wenye vyeti vya kuunga unga
   
 5. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tuache sheria ifate mkondo wake. Tutajua mbivu na mbichi.
   
 6. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Atakimbilia kufuta kesi kwa madai kuwa haina manufaa kwa Taifa, si ndiyo zao maji yakiwafika shingoni. Wanabeep wakipigiwa wanazima simu
   
 7. l

  lukule2009 Senior Member

  #7
  Oct 26, 2009
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 132
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wha if he is able to prove his qualifications? si he will up there ?au?
   
 8. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Umesema what if he will be able to prove , let him prove ndiyo tutaanzia hapo . Nimesha wahi sikia kesi za akina RA na Mengi , Mwanahalisi nk zote sijui ziliishia wapi. Mahanga hayuko taabani kweli kule Ukonga ?
   
 9. l

  lukule2009 Senior Member

  #9
  Oct 26, 2009
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 132
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Unajua msingi mmoja muhimu jamani : tusiamini kila tunachoambiwa hadi tupate ushahidi .kwa hiyo mahanga asihukumiwe sasa na hawa jamaa wanaosema ana vyeti fake kazi kwao kuthibitsha.. kwenye maisha dont believe whatever you are being told, search for facts..usiamini kila jambo unaloambiwa,thibitisha.
   
 10. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Mahanga kajitokeza kutetea hadhi ya PhD yake na je wale walioko kimya ni kweli kwamba wana vyeti feki ? Hii isije ikawa ni nguvu ya wana mtandao kupunguzana kasi sasa wanatoleana siri jamani .
   
 11. l

  lukule2009 Senior Member

  #11
  Oct 26, 2009
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 132
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Personally naona he will be very stupid if he got fake PHD and yet he goes to court!!! best alternative kama tuhuma ni za kweli ni kuka kimya.. but I think he is smart enough to know that.. kame ulivyosema tutege masikio tusikilize .. then tutaanzania hapo .. ua right
   
 12. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #12
  Oct 26, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Tatizo hapo sio Ph.D yake kuwa fake bali kuipata chuo ambacho hakitambuliwa na institutions mbalimbali za elimu.

  Toka mwanzoni nilishangaa hiyo confidence ya Msemakweli kwamba hao wana degree fake.

  Labda ana ushahidi zaidi ya ule ambao wengi wetu tumeujadili hapa mara nyingi.

  Hata Mahanga naona kang'ang'ania hapo hapo pa kuwa na degree fake.

  Wizara ya elimu inatakiwa waingilie kati na kutoa mwongozo juu ya vyeti vya elimu ili kama chuo hakitambuliwi na wizara ya elimu ya TZ, iwe ni maruku kutumia title au cheti hicho nchini TZ.
   
 13. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hawa wajinga wanaweza kuispin hii issue iende kwenye hii angle, huyo Msemakweli akaonekana muongo, akalipishwa fidia na kutakiwa kuwaomba radhi hawa vingunge, na diploma mills zitakuwa official bongo.

  A little knowledge is dangerous indeed.
   
 14. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Hii ni vita yetu sote na kwa kuwa long we have been shouting kuhusiana na matukio haya sasa atafutwe msemakweli asaidiwe mawazo pamoja na lwayer wake ili wasije wakapoteza maana tutakuwa tumepoteza pia .Mnasemaje ? If the answer is yes basi wenye contact za msemakweli wampe shout aje hapa jamvini .
   
 15. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #15
  Oct 26, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Bluray,

  Nakubaliana na wewe, tuombee Msemakweli awe na ushaidi zaidi ambao wengine hatuujui, vinginevyo anaweza akajikuta anasaidia kuhalalisha vyeti vya akina Mahanga.

  Mahakama ikitamka cheti chake sio fake, watakuwa wamehalalisha vyeti vingi vya namna hiyo.
   
 16. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #16
  Oct 27, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Mnyonge mnyongeni, hapa waandishi uchwara wamechemsha, hawa viongozi wanazo hizo degree, tatizo tu ni kwamba hizo degree hazikubaliki kwenye standards za kimataifa kielimu na vyuo walivyopatia hizo PhD, havitambuliwi na international community on education kama ni valid as PhDs.

  - Waandishi wameharibu hapo kwa kutoyachuja maneno ya mtaani, badala yake wameyachukua kama yalivyo kwamba hawa viongozi wamefoji vyeti, which is not the case, sasa Nipashe wamuombe huyu fisadi msamaha yaishe mapema, kabla mafisadi wote hawajashuka on them.

  - The lesson hapa ni kwamba hakuna a corrupt leader asiyejua sheria inapoanzia na kuishia, especially mtandao ndio maana husikii tena makelele ya Rostam kisheria dhidi ya Mengi, kama alivyoahidi kule nyuma, ndio maana leo humu humu JF, kuna wanaoshauri kwamba hakuna ushahidi dhidi ya Lowassa na Richimonduli, ni kwa sababu hawa mafisadi they are very good at sheria hasa ya bongo! Waandishi wetu waache hizi tabia za activism journalism, it not worthy a dime wataumia na kutuumiza wananchi wote at large!

  Respect.

  FMEs!
   
 17. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #17
  Oct 27, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Kama sisahau huyo bwana alisema wale aliowataja atakayedhani ameonewa aende mahakamani ili yeye aka prove reseach yake.
  Hapa nadhani ndipo game imeanza. Ebu tusubili. Lakini isije kuwa kama ya Zombe:D
   
 18. m

  mwanamasala JF-Expert Member

  #18
  Oct 27, 2009
  Joined: Jun 20, 2009
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mbunge George Nangale wa EALA,ana Phd ya wapi?
   
 19. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #19
  Oct 27, 2009
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Kuwa na cheti cha digrii na kuwa na digrii ni vitu viwili tofauti. Hawa vihiyo wana vyeti vya digrii lakini hawana hizo digrii. Hawajafoji hivyo vyeti, lakini ni vyeti vinavyosema wana digrii ambazo hawana.


  Nadhani Msemakweli ataweza kuithibitishia mahakama kwamba wahusika wamedanganya kwamba wana PhD wakati hawana. Wana vyeti tu. Ni kama mtu kuwa na cheti kisemacho ana nyumba wakati hana. Ukitangaza hana nyumba utakuwa hujakosea hata kama hakufoji hati miliki yake (ameuziwa na Afisa Ardhi).
   
 20. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #20
  Oct 27, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Well said mkuu Moshi....... Hebu imagine mtu anapata PhD in 6 to 9 months. Chuo kilichotoa hiyo PhD unakuta kina mtuj mmoja tu mwenye PhD na labda tena hatoi lecture za hiyo Kozi ya the so called our doctors. Chuo hakina Campus, wala reliable address. Sasa kwa nini hiyo isiitwe PhD ya mazabe............

  Halafu hivi feki ya kiswahili na fake zina maana sawa????????????? Mfano mtu anaposema mchezo wa jana kati ya Simba na Yanga ulikuwa feki au chakula hiki ni feki ina maana sawa na ile ya kiingereza fake????????? Ntamshangaa sana Dr. Mahanga kama atakomalia haka kaneno feki ambako haiyumkinik na hata yeye anajua si siku zote kwamba ni absolutely equal na fake.

  Anywayz nadhani tutajua mengi sasa!!!!!!!

  Ushauri kwa msemakweli - nenda baraza la kiswahili kaombe upewe tafsiri rasmi ya neno feki.
   
Loading...