Mahalu aibwaga serikali kortini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahalu aibwaga serikali kortini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kaa la Moto, Oct 5, 2010.

 1. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  na Happiness Katabazi

  MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, imetamka kuwa kifungu cha 36(4)(e) sura ya 200 cha Sheria ya Uhujumu Uchumi kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, ni kinyume cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Sambamba na hiyo, mahakama hiyo, imetoa maelekezo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ndani ya mwaka mmoja kuanzia jana, awe amefanyia marekebisho kifungu hicho.

  Hukumu hiyo ya Kesi ya Kikatiba ya mwaka 2008, iliyofunguliwa mahakamani hapo na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ilitolewa jana na jopo la majaji watatu lililokuwa likiongozwa na Jaji Kiongozi, Fakhi Jundu, aliyekuwa akisaidiwa na Jaji Agustine Mwarija na Projest Rugazia ambaye hakuwepo mahakamani hapo wakati hukumu hiyo ikisomwa.

  Akisoma hukumu hiyo, Jaji Jundu alisema kimsingi Mahakama Kuu inakubalina na hoja za mawakili wa mlalamikaji (Mahalu), aliyekuwa akitetewa na mawakili wa kujitegema, Alex Mgongolwa na Cuthbert Tenga kwamba kifungu hicho cha 36 (4)(e) sura ya 200 cha Sheria ya Uhujumu Uchumi, kinakwenda kinyume na Katiba ya nchi na kinaleta ubaguzi.

  Alisema wanakubaliana na hoja za mawakili wa Mahalu, kwamba uwepo wa kifungu hicho unafanya mshtakiwa mwenye fedha ndiye apate dhamana na mshtakiwa ambaye hana fedha hawezi kutimiza masharti hayo ya dhamana hivyo kuishia kusota gerezani.

  Hata hivyo, Jaji Jundu alisema kwa mujibu wa Ibara ya 30 (5) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mahakama Kuu inapoona kifungu chochote cha sheria kinakiuka ibara za Katiba , ina mamlaka ya kutoa maelekezo kwa Mwanasheria Mkuu kukifanyia marekebisho kifungu hicho.

  Hii ni kesi ya pili ya Kikatiba kufunguliwa na wananchi katika mahakama hiyo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na mwisho wa siku, wanashinda tangu serikali ya awamu ya nne iingie madarakani.

  Mahalu alilazimika kufungua kesi ya Kikatiba Mahakama Kuu, ikiwa ni muda mfupi baada ya mwaka 2006, kufikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi ya sh bil. 3.
   
 2. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ndiyo kawaida ya serikali ya awamu ya nne inabwagwa kila sehemu. Tatizo ni kuwa kila jambo inafanya pupa tu kwa lengo la ku-win mass kwamba inapelekwa hata vigogo mahakamani kama jk anavyozungumza majukwaani.

  Hata suala la mgombea binafsi lilifanywa kwa jazba tu. JK afahamu kuwa uongozi wake una dalili zote za kupwaya angeachia ngazi mapema huenda tungempatia heshima kubwa kuliko hivi sasa. Dr. Slaa akishinda urais, tumtarushia JK vilago vyake aende Chalinze.
   
 3. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #3
  Oct 5, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Si ndio utendaji haki jamani? Hii sio kesi ya msingi bali ni suala la dhamana ambalo linaonekana kuleta ubaguzi kwa washtakiwa wenye fedha na wasio na fedha!

  Sasa pupa ya serikali iko wapi hapa?
   
 4. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2010
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ... pupa ipo kwa UONEVU na KUTAKA KUKOMOA watu kwa kuwaninginiza mahakamani wakiwa hawana hatia. Sakata lote hili tunalijua. Hakuna LIRA iliyowekwa mfukoni na Profesa Mahalu. Narudia hakuna! Kesi iliyopo Kusutu ni ya kisiasa na players wote wanajulikana.

  WAKWAPUAJI wa pesa ya UMMA, pesa zetu tunawajua. Hawa bado ni un-touchables. Sina nia ya kutaja mtu hapa, ila INAKERA sana watu wanaona sawa tu kutumia mihela kibao kugharimia prosecution ya watu ambao ni innocent, licha ya HAKI zao kukiukwa kwa kiwango cha hali ya juu ili mradi tu MIJITU flani ina POWERS.

  The end is around the corner. Piga ua. Hata yule kibosile bwana mamvi mshika hatamu katika uonevu huu, utastaafu tu karibuni. Nashangaa hukuendeleza tena harakati zako kusaka UBUNGE katika jimbo flani mkoani kwetu.
   
 5. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2010
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hivi sheria hii ilitungwa ama kurekebishwa na serikali ya awamu ya nne.

  Hivi maamuzi kama haya sio kuwa ni dalili ama ushahidi kuwa serikali hii imeweza kuacha asasi na mihimili ya dola kukuwa na kuweza kufanya maamuzi bila ya kuingiliwa.

  Kuhusu suala la mgombea binafsi, hivi hadi leo bado hamtaki kuelewa kuwa kesi ile haikuwa ya mgombea binafsi bali ilikuwa ya majukumu ya mahakama dhidi ya bunge????

  Acheni huu utamaduni wa kuchakachua masuala muhimu na uhalali wa asasi nyeti kwa faida ya matakwa yenu.....
   
 6. minda

  minda JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  inafurahisha kwamba checks and balance inaonekana kuwepo katika masuala ambayo hayana maslahi kwa chama tawala tofauti na ile kesi ya mch mtikila ambapo jaji mkuu na jopo lake walikwepa kutoa maamuzi mwafaka.
   
 7. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #7
  Oct 5, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Mbona lile la mgombea binafsi walishindwa kuliamua ilhali lilikuwa ni wazi kabisa linamanyima haki raia anayetaka kugombea urais au ubunge lakini akawa hakubaliani na itikadi za vyama vilivyopo.
   
 8. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #8
  Oct 5, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,495
  Likes Received: 2,739
  Trophy Points: 280
  Hapa nashindwa kiielewa mahakama. Mbona kwenye kesi ya mgombea binafsi hawakutoa uamuzi kama huo!!!?
   
 9. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,838
  Likes Received: 468
  Trophy Points: 180
  Kesi hii ilifunguliwa kwa shinikizo la kikwete kutaka kumkomoa mzee huyu aliyekuwa mwadilifu katika utumishi wake akiwa balozi italy.Walitaka kumuingiza katika ufisadi wa kutafuta pesa za kampeni 2005 akawatolea nje. Wakaamua kumkomoa lakini mwisho wa siku serikali hoi.Ndugu zake wasukuma wanahasira sana na mkwere watammalizia kwenye sanduku la kura mwaka huu.
   
 10. M

  Msengapavi JF-Expert Member

  #10
  Oct 5, 2010
  Joined: Oct 23, 2008
  Messages: 4,802
  Likes Received: 2,748
  Trophy Points: 280
  Katiba yetu ina mapungufu mengi sana. Inevitably, lazima ipitiwe upya na kuwa kurekebishwa. October 31, 2010, Vote for Change bretheren!
   
 11. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #11
  Oct 5, 2010
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ... anaye uwezo wa kukomoa ni MUNGU pekee. Watu flani wanaumbuka na wataumbuka sana katika swala hili. Nguvu za ukandamizaji na wizi wa haki za watu zanashindwa kama zinavyoshindwa NGUVU za kiza. Si mnaona hayo?

  Kwa watuhumiwa wa kesi za uhujumu uchumi HUKUMU hii itasaidia sana. Kumbambikiza mtu likesi la uhujumu uchumi wa mabilioni kadhaa ili ashindwe pata dhamana SIYO rahisi tena.
  Leo hii HUKUMU hii inasakwa kwa udi na uvumba na mawakili kadhaa. Sijui kama baada ya kusomwa nakala tayari zapatikana.
   
 12. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #12
  Oct 5, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Aiseee.......mmmh!
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Oct 5, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Ukisoma hukumu ya suala la wagombea binafsi endapo mabadiliko ya Katiba yamepitishwa kihalali na Bunge yanaweza vipi kuwa kinyume cha Katiba? Kwa sababu majaji wa rufaa walichosema ni kuwa sehemu ya Katiba itakuwa kinyume cha Katiba endapo kimepitishwa kinyume cha utaratibu wa kufanyia mabadiliko ya Katiba.
   
 14. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #14
  Oct 5, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,936
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Jaji Brigedia General Agustino Ramadhani alishindwa nini kutoa hukumu kama hii kwenye kesi ya Mgombea binafsi?
   
 15. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #15
  Oct 5, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mwanakijiji,

  Kinachonittiza mimi ni kwamba katiba hapa ndio inaonekana shida. Tuna lidude linaitwa katiba ambalo ni shida tupu katika kutoa haki kwenye nchi yetu na sehemu nyingi tu zinapingana katika katiba hii.

  Lakini zaidi ya hayo nikiangalia hapa hukumu hii na hukumu ile ya mahakama ya rufani ya mchungaji Mtikila naona ingawa zote zina point kwenye katiba kuwa ina matatizo lakini humu hizo mbili zinakuwa na tofauti.

  Utaona hukumu hii inamuagiza mwanasheria wa serikali katika mwaka mmoja awe amepeleka mswada bungeni kubadilisha vifungu vinavyokinzana wakati hukumu ile ya mahama ya rufani ya mchungaji Mtikila inasema kwenye jambo hilo hilo kuwa mahakama ilikosea kuliagiza bunge kubadilisha kifungu cha katiba. Ikiwa na maana bunge lenyewe ndilo lenye uamuzi wa kubadilisha likipenda tena bila kulazimishwa na mahakama.

  Najiuliza kuwa kama hukumu ya mahakama ya rufaa iliona kuwa mahakama ilikosea kuliagiza bunge (kwa kumuagiza mwanasheria wa serikali ni sawa na kuliagiza bunge kwa kuwa naye ni mbunge kwa mujibu wa katiba) sasa hii hukumu si bado ni kama inakinzana na hukumu ya mahakama ya rufani?

  Haiwezi kuwa ile hukumu ya mahakama ya rufani litolewa na watu hawakwenda shule kiasi kwamba hata majaji wa mahakama za chini bado hawataki kuiangalia kama reference?
   
 16. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #16
  Oct 5, 2010
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,739
  Likes Received: 537
  Trophy Points: 280
  Nadhani muwalaumu wawakilishi(wabunge) wabovu wanaolala usingizi na kushindwa kujadili miswada,matokeo yake ndo kupitishwa kwa sheria kandamizi.Msifanye kosa sasa,chagueni wawakilishi makini.
   
 17. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #17
  Oct 5, 2010
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  HAWALAZIMISHWA WATOE HUKUMU WANAYOTAKA JAMAA FLANI. Upo hapoo? Hii haikupindishwa. Jee ile ya Katiba ilipindishwa? Akili kichwani!!
   
 18. NG'OTIMBEBEDZU

  NG'OTIMBEBEDZU JF-Expert Member

  #18
  Oct 5, 2010
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Halafu kuna watu(hapa Njb Kaskazini) wanataka eti wachague mtu aliyeishia darasa la nne(ingawa anatudanganya kafika la saba) awe mbunge wasijue kabisa kuwa hatakuwa na mchango wowote zaidi ya kupigia kura miswada kwa minajili ya kuvutia upande wao.
  Kukiwa na wabunge mambumbumbu watawezaje kujadili miswada nyeti kama hii wakati wengine hawajui kusoma wala kuandika,na wengine wanaingizwa bungeni ili kulinda maslahi ya chama,na hawathubutu kujikita kwenye kujadili mambo yenye manufaa kitaifa.
   
 19. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #19
  Oct 5, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,239
  Likes Received: 414,667
  Trophy Points: 280
  Kichwa cha habari kilinipa matumaini ya kuwa Prof. Mahalu ameishinda serikali katika kesi ya kimsingi kumbe ni suala la mdhamana tu. Ni vyema ukaboresha kichwa cha habarisiku za usoni ili kiende sambamba na habari yenyewe.
   
 20. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #20
  Oct 5, 2010
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Hivi huyu mzee aliwakosea nini mpaka wakaamua kumfanya hivi?
  Ni nani atamsafishia jina mzee huyu baada ya kuwa amechafuka kwa miaka yote hii?
  Kwa kumchafua huku kote hivi,serikali itamlipa huyu mzee?
  Hivi mheshimiwa fulani Maembe anajisikiaje baada ya mahakama kutamka?
  Ni watu wangapi kama huyu wananyea debe magerezani kwa kubambikiwa kesi zisizo na kichwa wala miguu?
  Pole sana mzee Mahalu.
   
Loading...