Mahali popote! RUKSA?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahali popote! RUKSA??

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by OkSIR, Jul 17, 2009.

 1. O

  OkSIR Senior Member

  #1
  Jul 17, 2009
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 108
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mahali popote!  Hata njia za train wengine wametumia[​IMG] Swali:
  Tuna miaka mitano (5) katika ndoa yetu na siku zote tumekuwa tunafanya tendo la ndoa kitandani tu, je ni sehemu zingine zipi zinaweza kutumika kwa wanandoa kufurahia kuwa mwili mmoja?
  Jibu:
  Ni kweli kitandani ndiyo sehemu ambayo ni rahisi (convenient), inayofaaa, inayotoa fursa na maalumu kwa wanandoa wengi kufurahia kufanya mapenzi (sex) au kuwa mwili mmoja. Hata hivyo si sehemu ambayo wengi hutumia kufanya mapenzi.
  Takwimu zinaonesha kwamba asilimia 90 ya wanandoa wanaofanya mapenzi huwa kitandani wapo wanandoa hutafuta sehemu zingine kutokana na mood au pale wanataka kitu kipya.

  Ni busara na hekima sana kuwa creative na kufanya kitu kipya hasa wawili wakikubaliana na ikiwa tu hakuna tatizo litakalotokea kuharibu privacy yenu, kukamatwa, kudakwa au hata kushitakiwa kwani kuna sehemu watu hawaruhusiwi hata kama ni mke na mume.

  "So, Sex is everywhere"

  Hapa si suala tu la kuwa na sehemu tofauti za wawili kuwa na faragha bali aina za milalo na pia ubunifu kuhakikisha kwamba shughuli nzima ya kuwa mwili mmoja haiwi na utaratibu unaojirudia miaka nenda rudi.

  Naamini hata wewe unayesoma hapa sasa hivi inawezekana umewahi tumia sehemu ambayo ukikumbuka unaishia kucheka hata hivyo ilikuwa ni kumbukumbu nzuri ndiyo maana umeishia kutabasamu.

  Baadhi ya sehemu ni:
  Kwenye shamba la mahindi, msituni, jikoni, bafuni, sebuleni, sakafuni, mezani, kwenye backyard huku kukiwa na nyota angani, kwenye gari, kwenye boat, chumba chochote kwenye nyumba yako, swimming pool, mlimani, kwenye mvua, beach nk.
  Naamini wapo ambao wamewahi tumia sehemu zingine zaidi ya hizo.

  Zifuatazo ni sehemu hatari kabisa kwa wawili kuwa mwili mmoja.
  Beach
  – kujisahau huweza kusababisha kubebwa na mawimbi, kumbuka ile issue ya tsunami.
  Ofisini – kama ni ofisi yako au ofisi yenu na mke wako au mume wako it is ok, ila kama ni vinginevyo utaacha evidence ambayo lazima utafukuzwa kazi.
  Makaburini (graveyard)- hata haielewiki watu wapoje, lazima akili iwe inaenda mwelekeo tofauti na binadamu wengine, hata hivyo tumeyasikia.
  Kanisani – ni aibu na kukosa maadili hata hivyo tumesikia watu wanaenda church pews kutimiza haja zao za kimwili.
  Kitandani au chumbani kwa wazazi wako – subiri ukamatwe ndo utajua kuwa ni risk kiasi gani.
  Kwenye reli – mahaba yakinoga mnaweza kusagwa na train.

  Pia ulimwengu wa sasa security Camera zinawekwa kila sehemu hivyo bila kuwa makini unaweza kushangaa issue zako zipo hewani bila kujua.
   
Loading...