Mahakimu wazidi kuikimbia kesi ya Mtikila

Ben Saanane

JF-Expert Member
Jan 18, 2007
14,581
18,124
Mahakimu wazidi kuikimbia kesi ya Mtikila
broken-heart.jpg



Tausi Ally
HAKIMU mwingine wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Salome Mwandu amejitoa kusikiliza kesi ya Mchungaji Christopher Mtikila ya kumwita Rais Jakaya Kikwete gaidi.

Hakimu Mwandu alitangaza kujitoa katika kesi hiyo mara baada ya jalada la kesi hiyo kupangwa kwake.

Huyu ni hakimu wa pili kujitoa katika kesi hiyo katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita. Februari 8 mwaka huu hakimu Waliarwande Lema alijitoa baada ya Mtikila kuwasilisha waraka akitaka hakimu huyo ajitoe kusikiliza kesi hiyo akidai kuwa hawezi kutenda haki kwa sababu ameonyesha kuwa na kisirani na ukatili dhidi yake.
Hata hivyo hakimu Mwandu alieleza sababu za kujitoa katika kesi hiyo kuwa ni pamoja na kuwa kesi nyingine ya mshtakiwa huyo kama ataendelea kuisikiliza kesi hii kuna uwezekano wa haki ikaonekana haijatendeka.

“Hivyo kutokana na sababu hiyo najitoa kuisikiliza kesi hii,”alisema Hakimu Mwandu na kuiahirisha kesi hiyo hadi Aprili 7, mwaka huu itakapokuja mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.

Awali Mtikila alieleza kuwa hana imani na hakimu Lema kwa kuwa anamnyanyasa. Alitoa mfano wa manyanyaso hayo, Mtikila alidai kuwa Oktoba 22, 2009 alichelewa kwenda mahakamani hapo na kuwa mara baada ya jalada la kesi yake kuitwa aliamriwa akamatwe, alikamatwa na kupelekwa mbele ya hakimu huyo na kuulizwa sababu ya kuchelewa.

Akifafanua zaidi Mtikila alidai, siku hiyo alieleza kuwa alichelewa kwenda mahakamani kwa sababu wakati akiwa njiani alilazimika kubadili gari eneo la Kamata- Shoprite, kwa bahati mbaya akapasukiwa na suruali yake hivyo ilimlazimu kurudi nyumbani haraka kubadili nguo ili aweze kwenda mahakamani hapo kwa vile mdhamini wake alikuwa Chanika na hakuwa na ufumbuzi mwingine.

“Lakini hata baada ya kuiona dhamira yangu njema na kufuta amri ya kunifutia dhamana, ulitumia muda mwingi kunifokea na kunikamia kwamba ‘ukirudia tena utaniona!’ nikabaki kujiuliza ninachoonywa kutorudia tena ni ajali ya kupasukiwa nguo au kukimbia nyumbani kubadili nguo ili nisije mahakamani uchi kwani nigekuja mahakamani uchi ningedharaulisha heshima ya mahakama na utu wangu mwenyewe,” alisisitiza Mtikila.


Aliongeza kudai kuwa, Novemba Mosi 2010 alipofika mahakamani hapo saa 4:45 asubuhi baada ya kuhangaikia mguu wake uliogongwa na nyoka aina ya Cobra akiwa nchini Zimbabwe kwa sababu ya taabu kubwa aliyoipata usiku, lakini baada ya hekaheka zote alipelekwa mahakamani hapo.

Mchungaji huyo aliendelea kudai kuwa watu wote walihofia athari ya sumu ya yule nyoka kwa sababu wanaogongwa hufa ndani ya saa 24, ingawa yeye bwana Yesu alimtendea muujiza mkubwa sana.

“Lakini wewe ulinifokea kwamba kuhangaikia uhai wangu siyo sababu ya msingi, ukafoka kwamba huna huruma na mimi, ukafuta dhamana yangu huku ukinifokea,” alidai Mchungaji Mtikila katika walaka huo.

Katika kesi hiyo Mtikila anadaiwa kuwa Oktoba 21, mwaka jana maeneo ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Ilala, jijini Dar es Salaam Mtikila alitoa maneno ya uchochezi yenye dharau na kujenga chuki dhidi ya Serikali na Rais.

Ilidaiwa kuwa siku hiyo, Mtikila alitoa maneno mengine ya uchochezi ambayo yalikuwa na chuki na dharau ambayo yangeweza kusababisha watu kukosa imani na serikali yao.
Iliendelea kudaiwa zaidi kwamba Mchungaji Mtikila pia alitoa maneno ya uchochezi kwamba: uteuzi wa "Jakaya Kikwete siku zote unaongozwa na imani yake ya dini kutekeleza malengo yake ya kusilimisha nchi....'' Mtikila alikana mashitaka yote na upande wa mashitaka ulieleza kuwa upelelezi umekamilika.
 
Huyu ndo mtikila. hivi kumbe unaweza kucheza na mahakama hivi.

hahahhahahah kwa kweli hizi sababu zinafurahisha
 
Amalize kesi hii kisha arudie ile kesi ya kupinga Mahakama ya Kadhi!
 
Mtikila alidai, siku hiyo alieleza kuwa alichelewa kwenda mahakamani kwa sababu wakati akiwa njiani alilazimika kubadili gari eneo la Kamata- Shoprite, kwa bahati mbaya akapasukiwa na suruali yake hivyo ilimlazimu kurudi nyumbani haraka kubadili nguo ili aweze kwenda mahakamani hapo kwa vile mdhamini wake alikuwa Chanika na hakuwa na ufumbuzi mwingine.

“Lakini hata baada ya kuiona dhamira yangu njema na kufuta amri ya kunifutia dhamana, ulitumia muda mwingi kunifokea na kunikamia kwamba ‘ukirudia tena utaniona!’ nikabaki kujiuliza ninachoonywa kutorudia tena ni ajali ya kupasukiwa nguo au kukimbia nyumbani kubadili nguo ili nisije mahakamani uchi kwani nigekuja mahakamani uchi ningedharaulisha heshima ya mahakama na utu wangu mwenyewe,QUOTE]

Mtikila u would make a wonderful commedian... ur in the wrong
field/profsn.
 
April 7 ni kumbukumbu ya kifo cha Karume hivi mahakama hawana orodha ya siku za mapumziko ya kitaifa?
 
Back
Top Bottom