Mahakimu watakiwa kutokuhairisha kesi mara kwa mara

pantheraleo

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
691
878
  • Mahakimu wametakiwa kusimamia uendeshaji wa mashauri na kuzuia maahirisho ya mara kwa mara ya kesi bila ya sababu za msingi kwa lengo la kuhakikisha kesizinamalizika kwa wakati Mahakamani.

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amesema hayo wakati wakikao cha majumuisho mara baada ya kumaliza ziara ya kikazi ya siku tano katikamikoa ya Iringa na Njombe aliyoifanya kwa lengo la kukagua shughuli zaMahakama pamoja na kubainisha kwa wadau changamoto zilizoibuliwa wakati wakikao cha Mahakama ya Rufani kilichomalizika leo mjini Iringa.

Jaji Mkuu amewata Mahakimu kutokubali kuahirisha mashauri kwa muda mrefukwa ajili ya kuandaa maamuzi madogo yanayotokana na pingamizi ambazo nyingihutumiwa vibaya kwa lengo la kuchelewesha mashauri.

“Maafisa wote wa Mahakama ni jukumu lenu pia kuzipa nguvu za kimahakamavifungu vya sheria zinazolinda haki ya Mwananchi aliye mahabusu kwakuhakikisha hakuna mwananchi atashikiliwa bila kufikishwa mahakamani ndani yasiku zilizowekwa na sheria”, alisema.

Alitoa rai kwa Mahakimu kutokuwa wepesi kukubali hoja za waendesha mashitakaza kusema kuwa upelelezi bado unaendelea bila ya kufafanua ni kitu gani katikaupelelezi bado kinatafutwa na ni kwa muda gani.

“Ni umakini wa Mahakama ndiyo utahakikisha kuwa shughuli za upelelezi
haziwanyimi wananchi haki yao ya kikatiba ya kutochelewesha haki yao ya
kusikilizwa kesi dhidi yao bila sababu za kimsingi,” alisisitiza Jaji Mkuu.

Akizungumzia dhamana, Jaji Mkuu amesema ni wajibu wa Mahakama kutoa
dhamana kwa makosa yenye dhamana kwa kuwa Mahakama ni msimamizi wahaki ya kila mtu kuwa huru na kuishi kama mtu huru.

Alivitaja vigezo vya kutumiwa katika kutoa dhamana kuwa ni pamoja na
vitambulisho vya Taifa, na vitambulisho vinavyokubalika. Aliongeza kuwa
Mahakama pia ziwaruhusu washtakiwa kujidhamini wenyewe pale Hakimu
anapojiridhisha na utambulisho wao kuwa watahudhuria mahakamani.

“Mashauri ambayo washtakiwa wamekosa dhamana yasikilizwe mfululizo, kwayale makosa yasiyo na dhamana na yako ndani ya mamlaka ya Mahakama,matumizi ya sheria yatumike ili kuyaondosha”, alisema.

Katika kupunguza msongamano magerezani, Jaji Mkuu amesema Maafisa waMahakama hawana budi kutumia adhabu mbadala kwa makosa madogo madogokwa kuzingatia sheria zilizopo.

chanzo:michuzi blog
 
Itakuwa ni Jambo la busara sana kutekeleza aliyoyasema CJ.
 
Hafanyi utafiti kabla hajatoa hoja anajitahidi kulaumu vyombo vingine ili kujisafisha aangalie watu wake ni maagent wazuri wa kujaza mahabusu na wafungwa.Mahabusu walionyimwa dhamana na sheria ni wachache kuliko walionyimwa dhamana na matakwa ya watu wake.

Ni kitu ambacho kwanadhalia inawezekana lakini kwa vitendo ni ngumu kuanzia hoja ya kupeleleza kwanza ndipo muhalifu akamatwe bado siyo jambo linaloendana na mazingira ya nchi yetu lakini pia lazima aangalie kiini cha haya yote na ajue asili ya mambo haya asifikiri kwamba kuna kundi au taasisi yenye lengo la kukomoa mtu bali azingatie job description yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom