Mahakimu watakiwa kuhakikisha wanatoa hukumu za haki

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma amewataka Mahakimu wakazi nchini kuhakikisha wanatoa hukumu za haki kwa wananchi na kupunguza misongamano ya kesi mahakamani.

Akiwaapisha Mahakimu Wakazi sabini jijini Dar es Salaam pia amewataka wakubali kufanya kazi katika vituo wanavyopangiwa na wasitarajie kupangiwa kazi mijini, kwani maeneo mengi ya vijiji hayana wataalam hao wa sheria.

Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania amesema ongezeko la majaji na Mahakimu wanawake ni ishara ya uzingatiaji wa usawa katika kuwapata watendaji wa vyombo vinavyotoa maamuzi.

Chanzo: ITV
 
Like father like son. Yeye mwenyewe hatoi hukumu za haki, sembuse hawa chekechea.
 
Back
Top Bottom