Mahakamani: Msaidizi wa Sabaya amkaanga ile mbaya, adai ni mtu hatari sana

Alidai Sabaya na walinzi wake walikuja Arusha na yeye aliitwa na mshitakiwa wa tano katika kesi hiyo,Silverster Nyengu{26} kuwa Sabaya anamwita katika hotel ya Point Zone na alifanya hivyo baada ya nusu saa lakini alikutana getini na msafara wa magari yakiwa yanatoka na aliambiwa apande gari ya nyuma aina ya VX Masai na kujikuta akiwekwa chini ya ulinzi kwa madai kuwa amechelewesha msafara.
🦮
 
Alidai kabla ya kumaliza Ushahidi wake alimwomba Hakimu Kisinda na Mahakama yake kumpa ulinzi yeye akiwa gerezani kwani Sabaya ni mtu hatari sana ombi ambalo Hakimu alitoa maelekezo kwa Askari Magereza kuhakikisha hilo linafikishwa kwa Mkuu wa gereza Kisongo Arusha ili utekelezaji uweze kufanyika.
Mlinzi wake kamlipua sasa anaponaje?
 
Kwenye Magenge ya kihuni na ujambazi ukisikia mtu akisema "Mtoe wenge" adhabu ndogo kabisa unayopewa ni kupigwa bapa la panga kichwani mithiri ya kukua. Na kweli Wenge linakutoka.🤣🤣
Chuga kutolewa wenge unazabwa makofi kwenye masikio yote mawili kwa wakati mmoja huwa wanaita 'headphone'

Nilikamatwa maskani nikawa mzito kutoa rushwa polisi mmoja akazunguka kwa nyuma akanipiga hiyo headphone nikabaki nasikia zzzzzzzzzzzzzzzzz

Hili ndiyo wenge alilotolewa huyu shahidi kwa maelekezo ya general sabaya.
 
Mwahomange alidai kuwa Sabaya alimwambia ni kwa nini anaitwa haendi kwa muda muafaka na anaenda kwa muda anaotaka na baada ya hapo aliwakabidhi walinzi na kutolewa wenge{kipigo} na kufungwa pingu
Duh..
NI kama kichaa kakabidhiwa shoka!
 
Jamaa ameumiza sn watu.Wengine wamekatwa masikio,vidole n.k.

Et alikuwa anatumia makonda style of leadership!
Na kwa vile Sabaya alitamka kwa mdomo wake kuwa anatumia MAKONDA STYLE basi ni wazi haya yote aliyotuhumiwa na mengine kuhukumiwa Sabaya basi Makonda kesha fanya sana.

Jee kwa nini hadi leo Makonda hajachunguzwa na kupelekwa sheriani? Ni aibu kwa DPP na Takukuru kubambika watu kesi na kesi za kweli wanakaa kimya hadi wananchi kama Kubenea wanatumia Private prosecutor kumshtaki Makonda.

Au yasemwayo kuhusu mahusiano yake Makonda binafsi yana ukweli?
 
"Kutolewa wenge" naona sasa ni zamu yake Sabaya kutolewa wenge.

Ajabu mtu huyu licha ya kukutwa na hatia na kufungwa lakini bado kuna vichaa wanamtetea bila aibu.
Sabaya aliumiza wengi ambao ni Chadema, kwa hiyo wenye chuki na Chadema kwao Sabaya ni shujaa wao kulingana na fikra zao za kijinga
 
Magufuri alipenda watu dizaini ya sabaya
Ndio maisha yake huyo jamaa yalivyokuwa.
Ndio maana hata wakati mnaenda kukumbuka mwaka mmoja toka aende zake ona wife alivyo nawiri! Ndio wenye akili wanajiuliza iweje mume aondoke na ndani ya mwaka mke shavu dodo? Lazima atakuwa alikuwa katika maisha ya mateso na hudhuni sasa yuko huru na furaha.
 
Kuna mtu kule kibaha anaitwa Capt Dickson Linje. Huyu KAZI yake ilikuwa kuwabambikia watu kesi za kumtukana Magufuri.

Nadhani muda mfupi ujao tutashuhudia visasi vyao
Alikuwa nani hapo Kibaha? Watu wanamna hii ni kuweka details zao hadharani kila mtu amjue
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom