Vawulence
JF-Expert Member
- Jan 4, 2009
- 1,931
- 2,114
Mkazi mmoja wa wilayani Kwimba jijini Mwanza leo tarehe 5 November 2010 amefikishwa katika mahakama ya mwanzo ya Hungumalwa kwa kosa la kumtapeli bibi mzee fisi wake.
Akitoa maelezo yake bibi aliyetapeliwa aliieleza mahakama kuwa mtuhumiwa alhmuazima fisi huyo dume kwa lengo la kwenda kuwazalisha fisi wake majike. Hata hivyo baada ya mtuhumiwa kuona fisi yule ana nguvu sana aliingiwa na tamaa ya kummiliki. Kuhakikisha anammiliki fisi yule,mtuhumiwa alimuahidi bibi sh.laki tatu ambazo alizikataa.
Habari zaidi zinadai kuwa baada ya bibi kukataa malipo mtuhumiwa aliamua kumchukua fisi kimya kimya akiamini bibi angeona aibu kuweka jambo hilo hadharani. Pasipo kutarajia mtuhumiwa alijikuta mahakamani na bibi akaeleza kila kitu bila chembe ya aibu. Na hadi sasa bibi ameshikilia msimamo wa kurejeshewa fisi wake na si malipo ya fedha.
Hakimu wa mahakama hiyo alipata wakati mgumu ikabidi awaamuru kurudi kwa mwenyekiti wao wa kitongoji kwanza na kujaribu kusuluhisha tatizo lao.
Habari hii ni ya kweli kabisa na si utani.Nimeiweka hapa kwani sikuona pengine pa kuiweka.Kama una mtu anayeishi Kwimba anaweza kukuelezea kwa uzuri zaidi.