Mahakamani kwa kumtukana mwenzake matusi ya nguoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahakamani kwa kumtukana mwenzake matusi ya nguoni

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, Nov 21, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  MWANAMKE Asha Ally [28] mkazi wa Mabibo Jeshini, amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo ya Magomeni kwa kosa la kumtukana mwanamke mwenzake matusi ya nguoni kinyume na sheria. Akisoma hati ya mashitaka Karani Elimina Eligi mbele ya Hakimu Mwanaidi Madeni isilisomeka kuwa Oktoba 23, mwaka huu, majira ya saa 3 usiku huko maeneo ya Mabibo Jeshini mlalamikaji alipokea ujumbe wa matusi kutoka kwenye simu yake ya mkononi kutoka kwa mshitakiwa.


  Ilidaiwa kuwa mshitakiwa alimmiminia matusi ya nguoni mlalamikaji Pendo John kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno [sms].


  Ilidaiwa kuwa mshitakiwa alitumia simu iliyokuwa na namba 0755 691542 na 0752 593940 kupeleka matusi hayo mbalimbali ya uzalilishaji kwenda kwa Pendo na kumpekea hadi akatoe maelezo kituo cha polisi.


  Moja kati ya meseji iliyomuumiza Pendo na kwenda kufungua hati ya mashitaka mahakamani hapo ili haki iweze kutendeka ni “ Muangalie miziwa yake yaani “matiti” kama una tenda ya kunyonyesha watoto yatima Muhimbili na utanikoma mbwa we”


  Na meseji nyingine kedekede ambazo hazifai kuandikwa hapa kwa mila zetu za kitanzania ikiwemo “bwana akutaki we unamng’anga’nia tu”


  Ilidaiwa mahakamani haopo kuwa chanzo cha ugomvi wa akina dada hao ni kugombea mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Bicco ambaye hakuwepo mahakamani na kudai kila mmoja alikuwa akimmiliki yeye.


  Hakimu alimuuliza mshitakiwa ni kweli ulimtukana Pendo alikana shitaka na kudai yeye hakumtukana na kuonyeshwa meseji hizo mbele ya mahakama.


  Hakimu alimuuliza mshitakiwa ina maana mnagombea bwana? mshitakiwa akajibu ndiyo muheshimiwa, hakimu akamuuuliza bwana mwenyewe anaitwa nani Bicco


  Kabla mlalamikaji hajaulizwa alidakia na kujibu Bicco ni mpenzi wangu mimi muheshimiwa!


  Hakimu alimuuliza mlalamikaji na huyo Asha yaani mshitakiwa ni nani? Akajibu huyo ni bwana wake wa zamani alishamuacha kwa sasa yuko na mimi ndio mana ananitukana kila kukicha kwa njia ya meseji alishamuacha


  Hakimu alimuuliza Pendo aliipataje namba yako akajibu kuwa aliiba kutoka kwenye simu ya mpenzi wangu


  Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 25, mwaka huu, itakapoendelea tena.

  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3565838&&Cat=1
   
 2. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #2
  Nov 22, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  wakikua wataacha
   
Loading...