Mahakamani kuna nini?

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
4,080
5,058
Kuna mambo yalitokea wakati wa mwanzo wa kesi ya Lema na leo hii yametokea kwenye kesi ya Melo.
Kwa Lema ilikuwa hakimu amekubali dhamana na akavunja mahakama kwa muda na watu walitegemea akirudi atoe masharti ya dhamana lakini alipoitisha mahakama tena akawa amefuta kauli yake ya mwanzo.
Leo mshtakiwa mmoja akiwa na mashtaka matatu kila shtaka limesomwa kwa hakimu tofauti.
Inawezekana ni utaratibu wa kimahakama ambao hatuujui lakini ni bora wananchi tuelimishwe kwani watu wenye nia mbaya wanaweza kupotosha jamii na kufanya mahakama isiaminike kwa wananchi.
Nawasilisha ila tuchangie kwa ustaarabu wa hali ya juu.
 
Haki na sheria, au unazungumzia mahakama za hapa tu tz? Zenyewe zina vitu vingi!
 
Bwana Maagizo kutoka juu, ndo anatesa watu atakavyo na hata Mahakama inamgwaya
 
Watanzania tunakosa umoja, kila kundi linakaa kulalamika lenyewe. Hata kutokea mahakamani kwa wingi leo tumeshindwa... Leo ilitakiwa iwe mafuriko ya watu mahakamani na hadi Sizonje apelekewe habari.

Nafikiri ni Kweli Mwenge ni uchawi na watanzania tumekuwa mazuzu.....it is Satan...
Viongozi wa dini wafanye maombi

Kuna masuala mengi yamepita kwa urahisi na ni ya kidhalimu.

-Mswada wa habari
-Mikopo ya wanafunzi
-FAO La Kujitoa
-Sheria ya mtandao
-Jamii forum Director (tumeshindwa kwenda mahakamani kwa wingi)
 
tatizo ni nyie mlioko Dar watu wadaresalamu mnaongea kuliko vitendo njoo A town.

swissme
 
Ndipo tulipofika baada ya kuambiwa kuna mhimili umerefuka kwenda chini
 
Hebu wataalam wa sheria watuelimishe sababu ya mtu kushtakiwa kwa makosa matatu na kila kosa kupewa hakimu wake.

Huu ni utaratibu wa kawaida au ni utaratibu uliobuniwa kwa ajili ya hii kesi?
 
Anastaafu karibuni anajiandaa kugombea urais kupitia CCM,hivyo hataki kuwaudhi makada wenzake.Aibu ya mahakama za Tanzania.Bora ziitwe matawi ya CCM.
 
Back
Top Bottom