Mahakamani Kuna Haki Kweli?

Oct 5, 2007
74
1
Nataka mchango wa hali ya juu kweli katika hili, ili nimuandikie Jaji mkuu;

Wapi Tanzania,uliwahi kuona mahakama imetoa hukumu halafu mshtakiwa akakata rufaa kwenye ngazi ya mahakama inayofuata halafu mshtakiwa akishinda kesi hakimu aliyetoa hukumu ya kwanza akihojiwa ni kwanini hakuona makosa waliyoyaona mahakimu ama jaji baada ya rufaa hiyo?

Kifupi naomba msimamo wenu ili nihoji endapo hakimu ama wa mahakama ya mwanzo au wilaya akifululiza kutoa hukumu za upendeleo mfululizo na mahakamani za juu yake kubatiulisha maamuzi yake na ikathibitika kweli alikuwa ameboronga katika hukumu hizo kwa upendeleo ama kutojua sheria anashitakiwa katika mamalaka gani?

Je, ni vema tuachie tu waendelee kuharibu bila hatua?

Nani hajui kwanini kesi nyingi zinakatiwa rufaa kama sio udhaifu wa mahakimu wetu?

Naomba wanasheria mnisaidie sana nami nipambane kwa njia hii tuokoe wananchi wanaofungwa kwa kukosa kukata rufaa!

Najua mpo na tutasogeza.
 
Katika kada niliyotokea kuidharau ni hiyo ingawa ni muhimu Ila %kubwa ni watu wa OVYO sana
 
Wanao amini uwepo wa maisha baada ya kifo wanasema haki ipo mbinguni. Pia elewa sheria hapa duniani ni utaratibu wa kimaandishi ulio idhinishwa katika jamii ili kuwawezesha matajiri kulinda mali zao na maskini kuishia jela.
 
Sheria ziko kwa ajili ya kuwa favor matajiri nchi hii,ukitaka kuamini hivi kwanza ni kwa kiasi gani raia tuna elimu japo ya kawaida ya kisheria? una uhakika katika makampuni mbalimbali ya kibiashara haki za wafanyakazi zinazingatiwa vizuri? ukienda kwenye mahakama zetu wakili anayejuana vizuri na jaji au hakimu ndio mwenye uwezekano mkubwa wa kushinda kesi hata kama hakutakiwa kushinda
 
Mahakama imepoteza heshima kabisa. Kesi za hovyo zimeendelea kurindima nchi na mahakimu na majaji kushindwa kutoa verdict.
 
Back
Top Bottom