real G
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 5,227
- 5,287
MAHAKAMANI KISUTU: Puto la Boss wa IPTL tumboni limeisha muda wake, linaweza kugeuka sumu
Wakili wa mmiliki wa IPTL, Harbinder Singh Sethi ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Puto lililopo tumboni mwa Seth limeisha muda wake na asipobadilishwa litamsababishia kifo.
Katika kesi hiyo, mbali na Sethi mshtakiwa mwingine ni James Rugemarila ambao wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi na kutakatisha fedha.
Hayo yameelezwa na wakili wa Seth, Alex Balomi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leornad Swai kueleza upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na wanaomba iahirishwe.
Baada ya kueleza hayo, Wakili Balomi amedai kwa mujibu amri ya Mahakama mteja wake Seth alipelekwa kufanyiwa vipimo Hospitali ya Taifa Muhimbili, lakini hadi leo hajapatiwa majibu ya vipimo wala kupatiwa matibabu.
Amedai kuwa mshtakiwa huyo ana Puto tumboni na limeisha muda wake, hivyo linapaswa kubadilishwa mwishoni mwa mwezi October.
>>>"Kama hilo balloon halitabadilishwa linaweza kugeuka sumu na kuondoa uhai wake, hivyo daktari aliyechukua vipimo anapaswa kumpatia."
Aidha, amedai kuwa wanaomba upelelezi ukamilike kwani upande wa mashtaka unaonekana umezembea sana na watuhumiwa wanateseka jela bila sababu.
Hata hivyo, Wakili Swai amedai kuwa Seth alipelekwa Hospitali October 13, 2017 na alipokea matibabu kutokana na vipimo vya daktari, lakini majibu ni siri ya Daktari na mshtakiwa, sio vya kuongelea Mahakamani.
Kuhusu suala la upelelezi wanaendelea kufanyia kazi.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Shaidi amesema Mahakama ilitoa amri kwamba Seth apelekwe Hospital na amepelekwa, hivyo daktari amekamilisha kazi yake, Mawakili wanaweza kwenda kuulizia kuhusu vipimo vyake akisema upande wa mashtaka ufanye unavyoweza kuhakikisha upelelezi unakamilika na kuahirisha kesi hadi November 10, 2017.
Chanzo: Millard Ayo