Mahakamani: Hatma maelezo ya mke wa Bilionea Msuya kujulikana leo Februari 21, 2022

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Hatima ya maelezo ya onyo yanayodaiwa kutolewa na mke wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu wa madini, marehemu Erasto Msuya maarufu kama Bilionea Msuya, Miriamu Mrita itajulikana leo Jumatatu Februari 21, 2022 wakati Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam itakapotoa uamuzi wake.

Miriam ambaye anakabiliwa na kesi ya mauaji ya wifi yake, Aneth Msuya, yeye pamoja na mwenzake, mfanyabiashara Revocatus Muyella, anapinga mahakama hiyo isiyapokee maelezo hayo ambayo anadaiwa kukiri makosa, kama upande wa mashtaka ulivyoomba, akidai kuwa hayakukidhi matakwa ya kisheria.

Hivyo, mahakama katika uamuzi wake itaamua kama maelezo hayo yamechukuliwa kwa mujibu wa matakwa ya kisheria au la.

Ikiwa mahakama itakubaliana na upande wa mashtaka basi itayapokea maelezo hayo na kuwa kielelezo cha ushahidi wa upande wa mashtaka, ambayo inaweza kuyatumia kumtia hatiani.

Lakini kama itakubaliana na hoja za pingamizi la upande wa utetezi, kuwa yamechukuliwa kinyume cha matakwa ya kisheria, basi itayakataa.

Miriam na Muyella wanadaiwa kumuua Aneth kwa makusudi kwa kumchinja nyumbani kwake, maeneo ya Kibada Kigamboni, Dar es Salaam, Mei 25, 2016.

Kesi hiyo namba103 ya mwaka 2018 iko katika hatua ya usikilizwaji wa ushahidi na upande wa mashtaka kupitia kwa shahidi wake wa kwanza uliomba mahakama hiyo kupokea maelezo yaliyotolewa na mshtakiwa huyo ambapo anadaiwa kukiri makosa, ili yawe kielelezo cha ushahidi wake.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo anayewakilishwa na wakiki wa kujitegemea, Peter Kibatala alipinga kupokewa kwa maelezo hayo ya onyo akitoa sababu tatu ikiwemo, kuteswa, akidai kuwa hakuyatoa kwa hiyari yake bali aliyatoa kutokana na mateso kutoka kwa askari Polisi.

Pia alidai kuwa maelezo hayo yalichukuliwa nje ya muda wa saa nne zinazoelekezwa kwa mujibubwa sheria, baada ya kutiwa mbaroni na kwamba

hakupewa haki zake za msingi wakati wa kuandika maelezo hayo.

Kutokana na pingamizi hilo, Jaji Edwin Kakolaki anayesikiliza kesi hiyo alilazimika kusimamisha kesi ya msingi na kusikiliza kwanza kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi ili kujiridhisha na uhalali wa uchukuaji maelezo hayo kama umekidhi matakwa ya kisheria.

Upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili Mwandamizi Erick Tesha akishirikiana na Gloria Mwenda na Caroline Matemo uliwaita mashshidi watatu akiwemo WP 4707 Sajenti Mwajuma (42), aliyeandika maelezo hayo ambaye pia shahidi wa kwanza katika kesi ya msingi.

Upande wa utetezi pia uliwaita mashahidi watatu akiwemo mshtakiwa wa kwanza mwenyewe, Miriam na mdogo wake, Mbaazi Mrita na askari wa magereza ambaye pia ni daktari wa zahanati ya gereza la.Segerea,Pembe Zuberi.

Dk Zuberi ambaye ndiye alifunga ushahidi wa upande wa utetezi katika ushahidi wake aliieleza mahakama jiyo kuwa alimtibia mshtakiwa huyo kidonda kilichokuwepo juu ya mguu wake wa kushoto karibu na kidole chake cha mwisho.

Alieleza kuwa Agosti 24, 2016 akiwa katika gereza la Segerea wakati wakihakiki washtakiwa wapya waliofikishwa katika gereza hilo alimuona Mrita akiwa na kidonda ambacho hakijafanyiwa usafi kilichokuwepo juu ya mguu wake wa kushoto karibu na kidole chake cha mwisho.

Alidai kutokana na jeraha hilo kilisababisaha mguu huo kuvimba na kwamba hivyo alimfanyia matibabu ikiwemo kumsafisha kidonda hicho,kumchoma sindano ya kutuliza maumivu na kuua bacteria pamoja na vidonge.

"Sijajua kidonda hicho kilisababishwa na kitu gani kwa jinsi kilivyokuwa kidonda chake kichafu inawezekana alijigonga, kujichoma na mwiba au kujimwagia na maji ya Moto," alidai Dk Zuberi.

Alieleza kuwa baada ya kumtimia alijaza jina la mshtakiwa huyo kwenye kitabu cha wagongwa wa gereza hilo ambacho hajakipeleka mahakamani hapo kutokana na utaratibu wao hauruhusu.

Alidai sheria ya magereza inasema mganga mkuu wa hospitali ya magereza hatihusiwi kutoa kitabu chochote cha hospitali hadi apate ruhusa kutoka kwa Mkuu wa gereza husika.

Baada ya maelezo hayo ndipo Jaji Kakolaki alipopanga kutoa uamuzi.

Source: Mwananchi

bilionea-pic-data.jpg
 
View attachment 2125663
Huyo mama anaroho ngumu kuliko shetani
 
Dah! Kuna umuhimu wa kutengeneza mazingira mazuri ya wosia kwa ajili ya wapendwa wetu, kabla ya kuondoka hapa duniani.

Ona sasa mke wa marehemu anateseka gerezani kwa kushutumiwa kumuua kikatili wifi yake! Familia itakuwa imeparanganyika! Kisa mali!
 
Ndio maana ni mara chache sana mwanaume ukiwa na hela mke wako kupendwa na ndugu zako hasa wazazi kwasababu wanajua tu una mlia timing mtoto wao ila sisi wanaume hatusikii tukishapenda.
 
Ndugu wa mume sio wa kuletea nao mazoea kabisa,ukijichanganya kidogo inakula kwako mazima
 
Dah! Kuna umuhimu wa kutengeneza mazingira mazuri ya wosia kwa ajili ya wapendwa wetu, kabla ya kuondoka hapa duniani.

Ona sasa mke wa marehemu anateseka gerezani kwa kushutumiwa kumuua kikatili wifi yake! Familia itakuwa imeparanganyika! Kisa mali!
Aliyeuliwa alikuwa ni dada mmoja mzuri na mrembo mno Tena mno mie iliniuma Sana jamani. Yaani wanaume tumepunguziwa utamu
 
Back
Top Bottom