Mahakama zetu ni PUBLIC ENEMY Number One katika vita dhidi ya Ufisadi, Wizi wa mali umma.

M_kara

JF-Expert Member
Jan 9, 2016
385
293
Katika hotuba mbali mbali Mh. Rais amekuwa akiwambia watanzania kumwombea kwa Mungu katika azima yake ya kutumbua majipu. Watanzania tunaelewa kwamba vita dhidi ya madawa ya kulevya, ufisadi na wizi wa mali ya umma ni ngumu na hatarishi. Na kwamba vita hii si ya Mh. Rais peke yake. Ni vita ya watu wote wapenda maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Sehemu muhimu katika vita hii ni mahakama zetu, ambazo mwisho wa siku ndo tunazitemegemea kutoa tafasiri na hukumu ya kisheria kwa makosa mbali mbali ya watu ambao, wananchi kupitia serikali yao, wanawatuhumu katika hujuma kwa taifa hili. Naamini, ndiyo maana kiasi cha mwezi mmoja uliopita Mh. Rais alielekeza taasisi ya mahakama ipewe haraka bilioni 2 ili kuboresha mazingira ya shughuli zake za kutoa haki. Kwa bahati mbaya sana, ni taasisi hii hii ambayo inaonekana kuwa PUBLIC ENEMY Number One katika vita hii ya kuondokana (kama siyo kupunguza) na vitendo vya rushwa, ufisadi na wizi wa mali umma.

Tanzania ina wanasheria ambao wengi wao wamepata elimu yao bure kwa pesa za walipa kodi. Inasikitisha kuona ni wanasheria hao hao walio katika ajira za serikali kwa nyazifa zao kama majaji, mahakimu, n.k. ambao wamegeuka kuwa ndio defense attorneys wa mafisadi wakijitahidi kutumia na kupenyeza vifungu vya sheria kila panapo wezekana kudhoofisha hoja za waleta mashitaka upande wa serikali, hasa kwenye high profile cases. Sisi ambao ni laymen katika taaluma ya sheria tunafahamu kwamba sheria haiwezi kwenda kinyume na common sense. Haiwezekani mahakama ipate kifungu cha sheria cha kumtia hatiani na kumpeleka jela mtu anaye shitakiwa kwa kosa la matumizi ya mtandao (kwa mfano) halafu sheria ile ile ikamwachia huru mtuhumiwa anaye shitakiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka, wizi wa mali ya umma, ufisadi n.k. kwa visingizio vya kukosa ushahidi wa kutosha. Haiwezekani sheria ikamtia hatiani mbakaji anayekana kosa lake, na wakati huo huo ikamwachia huru mpokea rushwa ambaye taasisi makini za upepelezi za kimataifa kama FBI au UK Serious Fraud Office ya uingereza inao ushahidi wa kutosha kuhusu mtuhumiwa.

Kampeni ya Mh. Rais inayoendelea ya kutumbua majipu ina viashiria vya kuwa 'wakati wa mavuno' kwa baadhi ya wafanyakazi wa mahakama. Badala ya kutenda haki, wenzetu wa mahakamani wanaona huu ni wakati wa kutafuta vifungu vya sheria (wakishirikiana na wanasheria wa watuhumiwa) ambavyo vinatoa loopholes za kuwaachia huru watuhumiwa kulingana na fungu la rushwa lililokubalika. Haingii akilini kwamba vitapatikana vifungu vya sheria vya kuwatia hatiani watuhumiwa waliokuwa wanafaidika na mitandao ya wafanyakazi hewa, wachuuzi wa madawa ya kulevya, na wngine wenye makosa ya aina hiyo. Lakini hatutashangaa kusikia kuachiwa huru kwa watuhumiwa walio jimilikisha tenda kubwa za kazi kwa wake zao, manunuzi au matumizi ya pesa yasiyo fuata utaritibu, wizi wa waziwazi wa mali ya umma, umiliki wa maekalu na mali zisizo kuwa na maelezo ya vyanzo vya kipato, n.k. kwa visingizio vya kukosa ushahidi. Kwa mwenendo huu wa kimahakama tunajua Lugumi haitawajibishwa, Tegeta Escrow & Co. hawatawahi kuspend a night jela, NSSF ndo haswa wao ni untouchables, na wote wale ambao kesi zao tayari ziko mahakamani wataachiwa huru au kupewa adhabu ya kusafisha soko la samaki feri kwa siku kadhaa. Rai yangu ni kwamba wananchi wanapofikia kiasi hiki cha kutokuwa na imani ya mahakama, then we are doomed as a nation.

Biblia inasema yafuatayo kuhusu wanasheria na majaji:

Isaiah 59:4 - No one enters suit justly; no one goes to law honestly; they rely on empty pleas, they speak lies, they conceive mischief and give birth to iniquity.

Jude 1:16 - These are grumblers, malcontents, following their own sinful desires; they are loud-mouthed boasters, showing favoritism to gain advantage
 
Hapo umenena mkuu kwa kweli mahakama zetu ni tatizo sana na zinarudisha nyuma juhudi ya mheshimiwa Rais ya kupambana na mafisadi . kwa kweli inabidi mahakama zetu ziangaliwe upya ingawa na mhimili unaojitegemea lakini unatakiwa upangwe upya . Kwani mafisadi nwengi ni watu wenye fedha za kutosha hivyoi kuwarubuni kwa kitita cha fedha za kutosha mahakimu ni jambo lakawaida .
 
Jana nilileta uzi kama juu hapa japo ulikua mfupi lakini nikarushiwa mawe na baadhi ya watanzania humu humu! Nilisikitika sana.
 
Jana nilileta Uzi jama huu humu wenye title "Nani wa kuwafunga mafisadi" lakini nikarushiwa mawe na baadhi ya wanzania wenzangu humu humu.
 
Tatizo pia ni sheria, watu wana tumia loopholes (mianya) kuponyoka, nadhani kazi ya kubadilisha sheria hasa za rushwa inatakiwa ipewe kipaumbele, na kesi nyingi sana serikali ita shndwa kwa kweli
 
Katika hotuba mbali mbali Mh. Rais amekuwa akiwambia watanzania kumwombea kwa Mungu katika azima yake ya kutumbua majipu. Watanzania tunaelewa kwamba vita dhidi ya madawa ya kulevya, ufisadi na wizi wa mali ya umma ni ngumu na hatarishi. Na kwamba vita hii si ya Mh. Rais peke yake. Ni vita ya watu wote wapenda maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Sehemu muhimu katika vita hii ni mahakama zetu, ambazo mwisho wa siku ndo tunazitemegemea kutoa tafasiri na hukumu ya kisheria kwa makosa mbali mbali ya watu ambao, wananchi kupitia serikali yao, wanawatuhumu katika hujuma kwa taifa hili. Naamini, ndiyo maana kiasi cha mwezi mmoja uliopita Mh. Rais alielekeza taasisi ya mahakama ipewe haraka bilioni 2 ili kuboresha mazingira ya shughuli zake za kutoa haki. Kwa bahati mbaya sana, ni taasisi hii hii ambayo inaonekana kuwa PUBLIC ENEMY Number One katika vita hii ya kuondokana (kama siyo kupunguza) na vitendo vya rushwa, ufisadi na wizi wa mali umma.

Tanzania ina wanasheria ambao wengi wao wamepata elimu yao bure kwa pesa za walipa kodi. Inasikitisha kuona ni wanasheria hao hao walio katika ajira za serikali kwa nyazifa zao kama majaji, mahakimu, n.k. ambao wamegeuka kuwa ndio defense attorneys wa mafisadi wakijitahidi kutumia na kupenyeza vifungu vya sheria kila panapo wezekana kudhoofisha hoja za waleta mashitaka upande wa serikali, hasa kwenye high profile cases. Sisi ambao ni laymen katika taaluma ya sheria tunafahamu kwamba sheria haiwezi kwenda kinyume na common sense. Haiwezekani mahakama ipate kifungu cha sheria cha kumtia hatiani na kumpeleka jela mtu anaye shitakiwa kwa kosa la matumizi ya mtandao (kwa mfano) halafu sheria ile ile ikamwachia huru mtuhumiwa anaye shitakiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka, wizi wa mali ya umma, ufisadi n.k. kwa visingizio vya kukosa ushahidi wa kutosha. Haiwezekani sheria ikamtia hatiani mbakaji anayekana kosa lake, na wakati huo huo ikamwachia huru mpokea rushwa ambaye taasisi makini za upepelezi za kimataifa kama FBI au UK Serious Fraud Office ya uingereza inao ushahidi wa kutosha kuhusu mtuhumiwa.

Kampeni ya Mh. Rais inayoendelea ya kutumbua majipu ina viashiria vya kuwa 'wakati wa mavuno' kwa baadhi ya wafanyakazi wa mahakama. Badala ya kutenda haki, wenzetu wa mahakamani wanaona huu ni wakati wa kutafuta vifungu vya sheria (wakishirikiana na wanasheria wa watuhumiwa) ambavyo vinatoa loopholes za kuwaachia huru watuhumiwa kulingana na fungu la rushwa lililokubalika. Haingii akilini kwamba vitapatikana vifungu vya sheria vya kuwatia hatiani watuhumiwa waliokuwa wanafaidika na mitandao ya wafanyakazi hewa, wachuuzi wa madawa ya kulevya, na wngine wenye makosa ya aina hiyo. Lakini hatutashangaa kusikia kuachiwa huru kwa watuhumiwa walio jimilikisha tenda kubwa za kazi kwa wake zao, manunuzi au matumizi ya pesa yasiyo fuata utaritibu, wizi wa waziwazi wa mali ya umma, umiliki wa maekalu na mali zisizo kuwa na maelezo ya vyanzo vya kipato, n.k. kwa visingizio vya kukosa ushahidi. Kwa mwenendo huu wa kimahakama tunajua Lugumi haitawajibishwa, Tegeta Escrow & Co. hawatawahi kuspend a night jela, NSSF ndo haswa wao ni untouchables, na wote wale ambao kesi zao tayari ziko mahakamani wataachiwa huru au kupewa adhabu ya kusafisha soko la samaki feri kwa siku kadhaa. Rai yangu ni kwamba wananchi wanapofikia kiasi hiki cha kutokuwa na imani ya mahakama, then we are doomed as a nation.

Biblia inasema yafuatayo kuhusu wanasheria na majaji:

Isaiah 59:4 - No one enters suit justly; no one goes to law honestly; they rely on empty pleas, they speak lies, they conceive mischief and give birth to iniquity.

Jude 1:16 - These are grumblers, malcontents, following their own sinful desires; they are loud-mouthed boasters, showing favoritism to gain advantage
Wewe hujaenda shule katu kwa uandishi huo au umetumwa na mabwana zako
 
Mkuu, umeongea kweli kabisa. Eti mwizi wa kuku anahukumiwa miaka 5 Jela. Aliyeiba billion zaidi ya 30 anaafungwa kifungo Cha kufagia hospital!!.loh
 
Wewe hujaenda shule katu kwa uandishi huo au umetumwa na mabwana zako
Mabwana zake? ameolewa au? fungua macho, habari ya shule imetokea wapi tena,hao wanaotuibia si wengi wao ni DR sasa hapo kisomo kinasaidia nini? UTASHI wa kuwaletea WANANCHI MAENDELEO ndicho cha muhimu
 
Hapo umenena mkuu kwa kweli mahakama zetu ni tatizo sana na zinarudisha nyuma juhudi ya mheshimiwa Rais ya kupambana na mafisadi . kwa kweli inabidi mahakama zetu ziangaliwe upya ingawa na mhimili unaojitegemea lakini unatakiwa upangwe upya . Kwani mafisadi nwengi ni watu wenye fedha za kutosha hivyoi kuwarubuni kwa kitita cha fedha za kutosha mahakimu ni jambo lakawaida

Ingawa watu wengi tunamuunga mkono mheshimiwa Magufuli katika jitihada zake za kupambana na maovu katika jamii yetu, vita hii itakuwa ni ngumu sana kushinda iwapo ataendelea kupigana kama LONE RANGER!!

Ishara zimeishaanza kuonekana kuwa hawa mafisadi na wauza madawa ya kulevya wameishagundua kuwa njia moja wapo ya kudhoofisha vita dhidi yao ni kutumia mwanya wa kuwahonga mahakimu na majaji wa mahakama zetu!! Ili kuweza kuwakabili wahalifu hawa mbinu anazotumia mheshimiwa Rais ni kama za ZIMA MOTO yaani zitafanya kazi kwa muda mfupi [ waswahili mtaani wanaita NGUVU ZA SODA] na hivyo muda si mrefu mafisadi watarudi tena kwa nguvu zaidi; kuwa na mapambano endelevu dhidi ya hawa maadui wa jamii yetu ni lazima kuwa na TAASISI zenye nguvu kwa mfano kuwa na mahakama yenye mahakimu na majaji waadilifu na hawa watapatikana tu iwapo tutakuwa na KATIBA ambayo itaelekeza jinsi ya uendeshaji wa mahakama hizi na jinsi ya kuwapata watumishi mahili wa mahakama wenye maadili!! Magufuli kuwashinda mafisadi anahitaji VERY STRONG INSTITUTIONS ENSHRINED IN A LEGITIMATE CONSTITUTION!!!! Bila kuwa na taasisi zenye nguvu atakuwa anatwanga maji kwemye kinu!!!
 
Mahakama siutumia vifungu vya sheria mfano mita mia mbili ccm siwalifurahia. Sheria ni msumeno wanasiasa hukurupuka ndo mana wanagarangwaza kisa ujinga hafu mzisingie tena.public enemy ni wanasiasa
 
Jana nilileta Uzi jama huu humu wenye title "Nani wa kuwafunga mafisadi" lakini nikarushiwa mawe na baadhi ya wanzania wenzangu humu humu.
usikate tamaa mahakama kuna majipu kuliko popote. ndio yanahamaki na wateja wao mafisadi kwa hofu. lazima umma wa wananchi waungane kwa kutumbua wanasheria wanaofanya biashara ya kuuza haki
 
Jana nilileta Uzi jama huu humu wenye title "Nani wa kuwafunga mafisadi" lakini nikarushiwa mawe na baadhi ya wanzania wenzangu humu humu.
Ndugu yangu, tayari kuna mtu hapa JF anadai sikwenda shule au nimetumwa. Sitaki hata kuwa katika majibizano naye kwa sababu he is a moron. Nina elimu kutosha na labda hata kumzidi. Watanzania tuamke kutokubali fikra za kipuuzi.
 
Back
Top Bottom