Mahakama za Tanzania ni kwa vibaka na wezi wa kuku lakini kwa mambo ya msingi ni pazia

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
7,252
2,000
Nenda mahakamani sasa hivi utaona jinsi mahakama zetu zinavyo washughulikia vibaka na wezi wa kuku bila huruma hata kama mtuhumiwa ni dhoofu bin hali kwa njaa na umasikini.

Inapokuja suala la kushughulikia mambo ya msingi ya kulinda katiba, sheria za nchi dhidi ya serikali, utawala bora na haki za binadamu, mahakama zetu ni dhaifu hakuna mfano! Mahakama zetu zinashindwa kuchukua nafasi yake ya kulinda wananchi, katiba ya nchi na utawala bora. Mahakama zinajipendekeza kwa wanasiasa na kusahau kuwa ni muhimili huru na unaojitegemea! Hivi sasa mahakama ni mali ya serikali na wanasiasa! Kazi kubwa inayofanywa na mahakama ni kumuapisha Rais na Makamu wake!

Ni bora mahakama hizi zivunjwe na kufutwa kabisa na badala yake tubaki na wenyeviti na watendaji vijiji na vitongoji kusimamia haki na kuhukumu wezi kwa sababu wazifanya kazi hizi kwa ufanisi mkubwa kuzidi mahakama!
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
29,136

Umepitiliza sana. Hawa uliowataja ndio wabovu wa rishwa. Wanakula kitu kidogo usiombe...
Tatizo Majaji hawana sifa wanachaguliwa kwa upendeleo na hivyo hawezi kutenda haki. Unamkumbuka Mashuri aliyewafunga Mbowe akapewa Ujaji? Huyo hawezi kutenda haki katu....
Akina Mugasha wa kesi ya MaDED kusimamia uchaguzi, aliboronga sana huyu mama, hovyo kabisa
 
Ni kweli huenda watendaji na wenyeviti wa vijiji na vitongoji wanakula rushwa sana lakini kuwadhibiti ni rahisi kwa sababu wananchi wana mamlaka ya kuwang'oa madarakani wakati wo wote wakitaka. Lakini hawa majaji wamewekewa kinga kubwa mno hawang'oleki kirahisi mpaka wafe!
 
Uko sahihi, ni rahisi kuwadhibiti, kwa hilo sawa maana tunawafhamu tabia zao, tumeua nao... uko sahihi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom