Mahakama za kadhi afrika mashariki:influence of sultanate of zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahakama za kadhi afrika mashariki:influence of sultanate of zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Phillemon Mikael, May 24, 2010.

 1. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #1
  May 24, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  Leo mahakama kuu ya kenya imetoa hukuma inayozipiga marufuku mahakama za kadhi huko kenya...katika kusoma wa kina nimevutiwa sana na maelezo ya chanzo cha kuwapo mahakama za kadhi ....

  Inaelezwa na wataalamu wa historia kenya kuwa,wakati wa ukoloni sultani wa zanzibar alikuwa akimiliki strip ya maili kumi ya pwani ya afrika mashariki ...kuanzia Kenya hadi MTwara..,baadaye pwani hiyo upande wa Tanganyika ikawa chini ya wajerumani[ikumbukwe sultani alikuja kabla yao].

  Walipokuja watawala wa kiingereza kule kenya sultani wa zanzibar aliamua kuipa mamlaka dola ya ufalme wa uingereza kusimamia masilahi yake Mombasa[ndani ya zile maili kumi]....lakini kwa masharti kuwa asivuruge mfumo wa maisha ya pwani hiyo ..ikiwemo kuzikubali mahakama za kadhi kisheria...ikawa mwanzo wa mahakama za kadhi kuwapo kenya kisheria.

  Ilipofika mwaka 1963 ...wakati dola ya uingereza ilipotaka kutoa uhuru kenya ......iliitisha referendum kwa wakaazi wa pwani ya mombasa ...waamue iwapo wanataka kubakia kwenye serikali mpya ya kenya au warudishwe chini ya mamlaka ya sultani wa zanzibar....maoni yao walitaka wabaki serikali mpya kenya ....lakini sultani ..ndiye alitakiwa kuridhia ...na aliridhia kwa masharti ya awali kuwa mila ,desturi na ilka za zanzibar ..ikiwemo mahakama ya kadhi ziwemo kwenye sheria ya kenya mpya.......na wakatia saini kati ya sultani,kenyata na gavana wa kenya ..shahidi akiwa binti mfalme margareth...

  Nadhani serikali ya Tanganyika haikulazimishwa kuweka mkataba wa kuwa na mahakama ya kadhi na sultani kwa kuwa wajerumani walishavunja .....utaratibu huo na sultani alikuwa na urafiki na muingereza zaidi ...hakuwa na uhusiano mzuri sana na mjerumani..!!...hata baada ya mjerumani kuondoka tanganyika ikawa chini ya umoja wa mataifa ..ni wazi kuwa sultani hakufuatilia tena haki yake ya umiliki wa maili kumi za pwani ya tanganyika!!

  Leo wanasheria kule kenya wanahofia kama baaada ya mahakama hiyo kuifuta makakama ya kadhi ....mkataba kati ya sultani[sasa serikali ya zanzibar]..wanaweza kuwa na haki ya kuingilia kati baada ya masharti ya wao kuwapa kenya kipande cha maili kumi kuvunjwa...au wakaazi wa mombasa ndani ya maili kumi wanaweza kutaka warudi chini ya zanzibar...

  Kwa kifupi hii stori nilikuwa naisikia tu lakini sijapata kuitafakari kwa hisia kama leo....wataalamu wa sheria hapa mnasemaje...je serikali ya mapinduzi zanzibar...ina mamlaka ya kurithi sheria au mikataba aliyoingia sultani ????...kwa kuwa zanzibar haina tena mamlaka ya kuingia mikataba ...je mikataba ya sultani ..inapovunjwa kama hivi nani anaweza kulalamika???? ...nadhani mmeona ,,namna misri inavyooendelea kunufaika na mikataba ya kikoloni hadi leo...???

  Na tafakari nyingine ninayoipata ni influence ya zanzibar kwa ujumla ...si ajabu kama si mapinduzi basi dola ya zanzibar ingekuwa kubwa na muhimu afrika mashariki yote....fikiria ingeendelea kukusanya kodi kwenye pwani ...ya mombasa??? sidhani ingekuwaje kwa pwani ya tanganyika ..kwani inajulikana baada ya wajerumani kuingia hapa ule mkataba haukufuatwa ...[refer six hours war-the world shortest war]...lakini ni wazi kuwa dola la zanzibar lingekuwa kubwa kuliko yote kiuchumi!!

  Nimetafakari na kuona kuwa ni wazi mapinduzi ya zanzibar yamesaidia amani ya kudumu kwenye pwani hii...tuyaangalie kwa jicho hilo......ni wazi kuwa kama sultani bado angekuwa zanziabar angetaka kurudisha Ardhi yake kwenye ndani ya maili kumi za pwani chini ya mamlaka yake....ukizingatia nguvu ambayo ingekuwa nyuma yake...UAE...etc ...ni wazi nguvu za kijeshi zingetumika.......nadhani hapo mtajuwa kiusalama kwanini CIA waliona ni lazima serikali ya sultani ipinduliwe...waliliona hili!!!

  .....ni dhahiri mapinduzi ya zanzibar yameleta faida kwa wazanzibar....lakini yameuwa dola kubwa la zanzibar....laiti mapinduzi yasingetokea ....naona mikataba yote iliyokuwa chini ya sultani ....ingekuwa salama.....na zanzibar wangeweza kudai nafasi yao muhimu kwenye ukanda huuu.......hadi leo sijapata kumsikia mwanasiasa wa zanzibar hasa ccm ...akiongelea influence ya zanzibar kabla ya mapinduzi!!!!!

  references:NATIONS:KADHI COURTS BANNED IN KENYA.

  The judges, sitting as a constitutional court, said the decision to include the Kadhi courts in the country's ultimate law favoured one religion over others.
  However, the judges reserved their decision on whether the provision should be included in the Proposed Constitution, which will be subjected to a referendum on August 4.
  The bench included Justice Joseph Nyamu, Justice Mathew Anyara Emukule and Justice Roselyne Wendoh.

  They also declared that public funds should not be used to run the courts as this would amount to "separate development of one religion and religious practice" contrary to the principle of separation of state and religion.

  In a 114 page ruling, the judges held that the enactment and application of Kadhi's court to areas beyond the ten mile coastal strip specified during their establishment in the colonial times is unconstitutional.

  They further declared that section 66 of the constitution which introduced the Kadhi's court infringes on the constitutional rights of a group of 26 religious leaders who went to court to challenge the inclusion of the Islamic courts.
  The Kadhi courts is one of the issues that have been raised as contentious by a group of political and religious leaders who have come out against Kenya's Proposed Constitution.

  They are meant to apply to Muslims who choose it for application of family law such as inheritance, marriage, divorce and personal status.

  <LI class=g>The Kadhi Courts: How Opportunists Polarize A Nation | tHiNkEr'S rOoM

  14 Apr 2010 ... Here we have a very clever attempt to influence the mind of the reader. ... That having Constitutional Kadhi courts in Kenya is purely for sorting ...... court challenging the legality of the Kadhi court Act, and the ruling ..... of 8th october 1963 between the UK, Kenya and Zanzibar ( at page 3). ...
  www.thinkersroom.com/.../the-kadhi-courts-how-opportunists-polarize-a-nation/ - Cached
  <LI class=g>Kenya: Fw: The Kenya Constitution; KADHI COURTS; the media; at ...

  29 Apr 2010 ... If anyone is in doubt as to the intentions of the Kadhi courts in the Kenya constitution, this article in the Daily Nation ought to be a ...
  blog.jaluo.com/?p=5199 - Cached
  <LI class=g>Why Christians oppose draft law - .: Capital FM Kenya: For ...

  9 Mar 2010 ... Who was the Sultan of Zanzibar? The Sultan was an Arab ruler who colonised ... The reason why I'm scared of Kadhi courts and why Kenyan chrsitian ... they will easily influence adoption of kadhi courts into sharia law. ...
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160

  Mungu ibariki Kenya, Mungu ibariki Afrika.
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  May 25, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Phillemon Mikael,
  Mkuu kwanza umefurahia hukumu ya mahakama ya Kenya kwa sababu ya Udini zaidi ya kueleza mambo muhimu zaidi.. Umeacha kipande hiki muhimu zaidi - However, the judges reserved their decision on whether the provision should be included in the Proposed Constitution, which will be subjected to a referendum on August 4, 2010.
  Kwa hiyo hii ni kama ule ushindi wa Mtikila kwa mgombea binafsi ambao unaweza kuchukua mkondo wowote ule na pia haimaanishi ushindi ni ushindi wa Wakristu dhidi ya Waislaam.. Huu ni ujinga unaozidi kuenezwa na watu wasioweza kutazama upande wa pili wa kila sheria..

  Binafsi pamoja na kuwa sii mwanasheria, sababu za maamuzi ya mahakimu hawa yalikuwa ya kipuuzi kabisa kama vile watu hawakusoma wanapozua infulence ya Sultan na mahakama ya kadhi nchini Kenya lakini wakashindwa kutazama influence ya Malkia na Ukristu ktk sheria zilizopo Kenya. Kama kweli wanataka sheria zao ziwe hazina udini basi kwa kila sheria zilokuwa influenced na Malkia pia ziondolewe zinawalazimu Waislaam kuifuata. In fact Kenyan ultimate law favour one religion (Christianity) over others kutokana na utawala wa Malkia. Toka mavazi, Lugha, sheria, customs, na mengine yote ni kuiga Muingereza kushinda Waingereza wenyewe.

  Mkuu wangu ktk mada zilizopita mimi nimezungumzia uwezekano mdogo wa sheria za kiislaam kutumika kwa Waislaam wa Afrika kutokana na wao kushindwa kufuata ibada za dini zinavyotakiwa badala yake jadi zetu zimechukua nafasi kubwa ya ndoa zetu, watoto na hata mahusiano ya kifamilia kuliko dini inavyowaamrisha kufanya..hivyo kuwahukumu Waislaam ktk mfumo ambao haupo ktk maisha yao ya kila siku na sioo waislaam wa kweli ktk matendo yao ni kulazimisha sheria. Hii pekee ndio sababu nayoweza kuizungumzia lakini sio maswala ya waarabu kutawala hali kuna Wazungu Walio tutawala na tukachukua sheria zao.

  Umeulizia kwa kuhofia hatma ya Kenya kutokana na maamuzi hayo ambayo kisheria Kenya watalazimika kurudisha mkoa wa Mombasa ktk Utawala wa Zanzibar. Labda tu nikufahamishe tu kwamba makubaliano baina ya Kenyatta, Mohamed Shamte, mwakilishi wa Malkia na Jamsheed bin Abdallah ndio yalipelekea Kenya kuchukua Mombasa ktk Uhuru wa nchi hizi mbili uliopangwa kufanyika mwezi Dec 1963.

  Wazanzibar wakubali wasikubali lakini uhuru wa mwaka 1963 ulikuwa Uhuru bandia tu kama ule wa Ian Smith huko Zimbabwe ( Rhodesia), kwani Sultan Jamheed alikuwa bado kiongozi wa nchi (head of State) kulingana na makubaliano haya haya clearly stating that Zanzibar was a consitutional monarchy chini ya utawala wa Sultan Jamheed (head of State) na Waziri mkuu ni Shamte (Chief Minister) jambo ambalo lilipelekea Mapinduzi ya mwaka 1964.

  Maadam Mapinduzi haya ya mwaka 1964 ndiyo yanayohesabika leo na yenye sheria mpya ya utawala mzima wa kimapinduzi Zanzibar sidhani kama makubaliano ya mwaka 1963 will apply hapa. Lakini kama sisi Tanzania na hasa Zanzibar tukiweka madai haya mbele ya sheria inawezekana Kenya wakawa ktk wakati mgumu zaidi kwani maamuzi ya mahakama ya kadhi yanaweza kui cost nchi nzima Pwani yote ya east coast wakawa a land locked country na pengine kutokubali matokeo mwisho kuingia vitani na Tanzania.
  Now U can choose one, either better off let them (muslim) hang themselves na hiyo sheria or forced into a game of Russian roulette!
   
 4. P

  Paul S.S Verified User

  #4
  May 25, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  kwakeli Mungu ibariki afrika mashariki.ni kweli kabisa hii mahakama ilikua ya upande mmoja, hawa ngugu zatu wanapaswa kufahamu hakuna dini inayo weza kuachiwa kufanya kila kitu ipendavyo lazima misingi ya kibinadamu izingatiwe hasa katika nchi zenye dini zaidi yamoja
   
 5. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #5
  May 25, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280

  mkuu naomba uyaangalie mawazo yangu kwenye mtazamo chanya!!!!..futa suala la mimi kufurahi ....sijaandika popote...usinihukumu kwa kanzu yangu niliyovaa au rozari[tasbihi] yangu.....kuacha hilo nimependa sana mawazo yako......naomba pia angalie changamoto nilizoziweka..

  ..je pale zanzibar leo nani anaweza kukumbushia mkataba kati ya sultani na malkia ..ulioipa kenya Mombasa!!!!............................

  unaonaje hila za CIA ...ni wazi kwa kujuwa influence na ukubwa iliyokuwa nao dola la zanzibar.....kupinduliwa kwa sultani ilikuwa afueni kwa wazungu!!!...

  nilijaribu kutafakari....na nimeona kuwa mapinduzi pamoja na faida zaKE pia yalikuwa na hasara ya kuvunjika kwa dola kubwa la zanzibar ...kama vile dola nyingine pwani hii kama kilwa ,sofala etc zilivyoanguka!!!
   
 6. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #6
  May 25, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  ......kumbe wakati wa vurugu za pemba .....wale ndugu zetu waliokimbilia mombasa..kamwe hawakuihitaji kuitwa wakimbizi....kwani bado walikuwa ndani ya eneo lao [kihistoria]......na pia Kenya haingekuwa na uwezo wa kuwarudisha......nadhani wazanzibar hawahitaji passport kuwa mombasa!!!
   
 7. S

  Subira Senior Member

  #7
  May 25, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 162
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  ninachoamini mimi ni kuwa kuna hofu kubwa sana inayowapata upande wa pili wa rosari kuwa waislamu wana udini na wanachodai kitaleta domination,lakini ikumbumbukwe kwamba, wanaodai mahakama hii ni wananchi walio huru ndani ya nchi hizi, swala la kutawaliwa na waarabu au wazungu hapa halipo tena. Imani walionayo wahitaji hawa inatokana na itikadi na wanavyoamini kuwa hivyo ndivyo ilivyo sawa, swali kubwa ni kuwa sheria zote zinazotawala sasa nchi hizi zimetokana na wazungu ambao ni wakiristo je kuna uwezekano wa upande wa pili kuzikataa, hii inahatarisha amani, na pia kuwatoa shaka ni kwamba mahakama hizi hazitoingiliana na sheria za nchi hizi ni kwa wahusika tu, ili waendeleze imani zao za dini yao, nakuapia hata upande wapili watatamani sheria hizi baada ya muda. wapewe haki yao.
   
 8. n

  n'golofu Member

  #8
  May 25, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WAZANZIBARI WANYAMEZE KIMYA KUEPUSHA MIGOGORO ISIYO NA MAANA:target:

  WAPOTOSHAJI KWA UMMA WAMEANZA TENA. NANI KAWAZUIA WAISLAMU KUWA NA MAHAKAMA YAO YA KADHI. HAKUNA BWANA. NANI KAWAZUIA KUFANYA IBADA YAO NJEMA KWAO, JIBU HAKUNA.
  MBONA MAKANISA YANA MAHAKAMA ZAO, ZENYE MAJINA TOFAUTI--FUATILIA UTAJUA HILO.

  TATIZO LINAANZA PALE KUNDI MOJA LINATAKA MAHAKAMA HIZO ZINGHARIMIWE NA GVT , IN THE NAME OF MAHAKAMA YA KADHI. WANARUHUSIWA KUANZISHA ILA SERIKALI ISIHUSIKE KUTOA AJIRA KWA WATUMISHI WA MAHAKAMA HIZO.

  GVT IDEAL NA AFYA, ELIMU, COURT ZAKE TU, ARMY , NK.
   
Loading...