Katika bunge linaloendelea serikali iliwasilisha mswada wa kuanzisha mahakama ya kushughulikia kesi za ufisadi.
Mahakama hii ianze na tuhuma zilizobayana, mfano, Ununuzi wa Rada; Tegeta Escrow Account, Lugumi, UDA, Richmond nk. Isije ikaanza na kesi viini macho kama za kumshitaki sungura kwa kula majani ya mbuzi, yaani, kesi za alijilipa milioni 40 akaishi kama malaika; ama eti Afisa Utumishi alipokea mshahara wa marehemu. Kama Mahakama ya Mafisadi itaanza na vikesi kiini macho basi huo utakuwa ni utani tena utakuwa ni ubaradhuli.