Mahakama Yetu Ianze na Yaliyo bayana

1954tanu

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
1,038
487
Katika bunge linaloendelea serikali iliwasilisha mswada wa kuanzisha mahakama ya kushughulikia kesi za ufisadi.

Mahakama hii ianze na tuhuma zilizobayana, mfano, Ununuzi wa Rada; Tegeta Escrow Account, Lugumi, UDA, Richmond nk. Isije ikaanza na kesi viini macho kama za kumshitaki sungura kwa kula majani ya mbuzi, yaani, kesi za alijilipa milioni 40 akaishi kama malaika; ama eti Afisa Utumishi alipokea mshahara wa marehemu. Kama Mahakama ya Mafisadi itaanza na vikesi kiini macho basi huo utakuwa ni utani tena utakuwa ni ubaradhuli.
 
Tunataka tuanze na Richmond. Mbona unaikimbia hiyo. Au kwa sababu ni boss wako?
 
Unayoyasema ni sahihi sana lakini kusema ukweli upo wasiwasi mkubwa kama kweli hiyo mahakama italeta kizimbani hizo kesi kubwa zote. Hii ni kwa sababu haki haitatendeka, kwa mfano vipi ushahidi ukimnyooshea kidole moja kwa moja kiongozi yeyote wa zamani ambaye juzi tu Magufuli tayari ameshawalinda? Je, itakuwa haki kuwatia hatiani wahalifu wengine ambao walifanya ubadhirifu kwa kushirikiana na kiongozi huyo huku yeye akiendelea kuishi kifalme?
Kimsingi katiba ingerekebishwa sambamba na utungwaji wa sheria hiyo ili haki itendeke.
 
Tunataka tuanze na Richmond. Mbona unaikimbia hiyo. Au kwa sababu ni boss wako?
Mkuu tafakari hii ya Richmond kwani itaibua wasiyotaka kuyaibua. Kwa nini unafikiri magamba walishindwa kuyavua hata kama walisema wanayajua. Hebu muulize waziri msomi yale ambayo alisema aliyamezea ni yapi? Lakini pia Richmond siyo ya kwanza kuna msururu mrefu. Sisi tunasubiri tuone mambo yatakuaje wakiwaweza wa richmondi sawa, ya meremeta sawa, ya deep green sawa, escrow sawa, epa sawa, mabehewa mabovu sawa, etc.
 
Katika bunge linaloendelea serikali iliwasilisha mswada wa kuanzisha mahakama ya kushughulikia kesi za ufisadi.

Mahakama hii ianze na tuhuma zilizobayana, mfano, Ununuzi wa Rada; Tegeta Escrow Account, Lugumi, UDA, Richmond nk. Isije ikaanza na kesi viini macho kama za kumshitaki sungura kwa kula majani ya mbuzi, yaani, kesi za alijilipa milioni 40 akaishi kama malaika; ama eti Afisa Utumishi alipokea mshahara wa marehemu. Kama Mahakama ya Mafisadi itaanza na vikesi kiini macho basi huo utakuwa ni utani tena utakuwa ni ubaradhuli.
Comrade, hilo halipo kwa tuhuma ulizozitaja. These are few blessed ones!. Nashukuru umeliona hilo, maana mrengo wa upande mwingine hayo si rahisi kuonekana- Lugumi for example inapigwa dana dana
 
Katika bunge linaloendelea serikali iliwasilisha mswada wa kuanzisha mahakama ya kushughulikia kesi za ufisadi.

Mahakama hii ianze na tuhuma zilizobayana, mfano, Ununuzi wa Rada; Tegeta Escrow Account, Lugumi, UDA, Richmond nk. Isije ikaanza na kesi viini macho kama za kumshitaki sungura kwa kula majani ya mbuzi, yaani, kesi za alijilipa milioni 40 akaishi kama malaika; ama eti Afisa Utumishi alipokea mshahara wa marehemu. Kama Mahakama ya Mafisadi itaanza na vikesi kiini macho basi huo utakuwa ni utani tena utakuwa ni ubaradhuli.
Hata kuanzishwa kwake ni dalili za ujinga. Nchi inahitaji mahakama maalum itakayoshughulikia makosa yasiyoruhusiwa dhamana pamoja na watuhumiwa walionyimwa dhamana katika makosa yanayoruhusiwa dhamana. Hasara ya mahakama hii ya kutafutia sifa itaonekana mapema tu. Tatizo la mtu kufungwa mahabusu kwa miaka mingi kisha akaachiwa kwa kukosekana ushahidi linaonekana la kawaida kwa CCM.
 
Tena ni ujinga wa kutosha kwa maana ya kawaida kabisa SHETANI HATOI SHETANI
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom