Mahakama yawafutia dhamana M/kiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko

Ungejua maana na masharti ya dhaman usingetoka povu. Ni Mara nyingi Mbowe hakufika mahakamani kwa sababu nyepesi tu na aliachwa. Hata hii ya mwisho kuwa kaugua gafla na kukimbizwa SA ulikuwa usanii tu. Yaani augue, hakuna taarifa ya Chama kama kaugua Mpaka inaenda kutolewa mahakaman? Haileti maana hiyo. Sometimes yote hayo yanatendwa ili kuifanya mahakama ionekane kuwa inawaonea na ni maagizo ya juu. Mbona we zake Mbowe wamekuwa wakienda Mahakaman na hawajapelekwa Segerea?
Acha mahakama itende yale wayapendayo.
 
Taarifa za uhakika kutoka mahakamani.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewafutia dhamana Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime mjini Esther Matiko hivyo kuanzia sasa watarudishwa Rumande mpaka pale kesi itakavyoisha

Uamuzi huo unatokana na maombi yaliyotolewa na upande wa mashtaka Novemba 12, uliodai washtakiwa hao wamekiuka masharti ya dhamana kwa kusafiri nje ya nchi bila kibali cha mahakama na kushindwa kuripoti katika kituo cha Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala.

Upande wa mashtaka ulifikia hatua hiyo baada ya Mbowe kushindwa kufika mahakamani, Novemba Mosi na 8 na Matiko kushindwa kufika Novemba 8, kwa ajili ya usikilizwaji wa awali wa kesi inayowakabili.

Mbowe, Matiko na wenzao saba wanakabiliwa na kesi ya jinai mahakamani hapo yenye jumla ya mashtaka 8 yakiwemo ya uchochezi na uchochezi wa uasi.

Habari zaidi, soma=>Mbowe na viongozi 6 wa CHADEMA wafikishwa Mahakamani Kisutu, wasomewa mashitaka 8, wanyimwa dhamana hadi Machi 29 - JamiiForums
Sheria inayohusu dhamana inaeleweka ila wanasiasa wanapenda kuchanganya watu.
Jamaa wanafanya makusudi kwa kucheza mchezo wa paka na panya wakiachiwa nni kama wanaogopwa na wanapochukuliwa hatua stahiki wanaonewa.
 
Back
Top Bottom