Mahakama yatupilia mbali pingamizi la Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mahakama Kuu Division ya Makosa ya Uhujumu Uchumi na Rushwa Leo Septemba Mosi, 2021 imetupilia mbali pingamizi lililowasilishwa na Mawakili wa upande wa utetezi, juu ya Mahakama hiyo kuwa na uwezo wa kusikiliza kesi ya Ugaidi.

Usikilizwaji wa kesi hiyo unaendelea.

=====

1630498645882.png


Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, maarufu kama Mahakama ya Mafisadi, imetupilia mbali pingamizi ililowasilisha na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu la kwamba mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi zenye mashtaka ya Ugaidi.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatano Septemba Mosi, 2021 na Jaji Elinazer Luvanda, baada ya kupitia hoja za pande mbili.

Jaji Luvanda amesema mahakama hiyo ina mamlaka ya kusikiliza mashauri ya ugaidi na kwamba pingamizi lililowasilishwa na upande wa utetezi halina mashiko na hakubaliani nalo.

"Kwa maoni yangu, sitaweza kukubaliana na hoja zilizowasilishwa na upande wa utetezi," amesema Jaji Luvanda na kuongeza

"Baada ya kupitia hoja za pande zote, mahakama hii inayo mamlaka ya kusikiliza mashauri ya ugaidi na hoja zilizowasilishwa na upande wa utetezi hazina mashiko," amesema Jaji Luvanda.

Jana Agosti 31, 2021 Mbowe na wenzake waliwasilisha pingamizi mahakamani hapo wakipinga mahakama hiyo kuwa haina mamlaka ya kusikiliza kesi yao kwa mashtaka ya ugaidi na kwamba kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia Ugaidi kesi yao inapaswa kusikilizwa na Mahakama Kuu ya kawaida na si hiyo ambayo ni Divisheni Maalum.

Baada ya washtakiwa hao kuwasilisha pingamizi hilo, Serikali imepinga hoja hizo ikidai kuwa kwa mujibu wa marekebisho ya sheria mbalimbali namba 3 ya mwaka 2016 makosa yaliyoko kwenye Sheria ya Ugaidi yaliwekwa kwenye Sheria ya Uhujumu Uchumi na kwamba kwa hali hiyo mahakama hiyo ya ufisadi ina mamlaka ya kusikiliza mashtaka yao.

Baada ya Jaji Luvanda kutoa uamuzi huo, upande wa mashtaka waliomba kuwasomea maelezo ya awali (PH) washtakiwa hao.

Hata hivyo kabla ya kuwasomea maelezo kufanya, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando anayewasilisha jopo la mawakili watano wa upande wa mashtaka, ameniomba mahakama hiyo, kufanya marekebisho katika hati ya mashtaka kwa kuieleza mahakama hiyo kuwa Hoteli ya Aishi ipo wilayani Hai na sio wilayani Moshi kama ilivyoandika katika hati ya mahstaka.

Wakili Kadando baada ya kueleza hayo, Wakili wa utetezi Peter Kibatala amewasilisha pingamizi mahakamani hapo akipinga hati ya mashtaka ina makosa.

Kutokana na hali hiyo, Jaji Luvanda aliahirisha kesi hiyo kwa dakika 15 ili upande wa utetezi uweze kuja kuwasilisha hoja kuhusu pingamizi hilo huku upande wa mashtaka nao watatakiwa kujibu hoja hizo.

Chanzo: Mwananchi
 

Attachments

  • R Vs Freeman Mbowe and 3 others Ruling(1).pdf
    1.9 MB · Views: 5
Ulikuwa upuuzi mtupu.
ujuwaji mwingiiii!!
mnawachosha mabalozi wa watu bureee mwisho wapate korona!!!
Mbowe anavuna alicho kipanda.
eti anachagua Mahakama ya kusikiliza kesi yake!!
mwishowe atachagua na gereza la kutumikia kifungo chake!!
 
Ulikuwa upuuzi mtupu.
ujuwaji mwingiiii!!
mnawachosha mabalozi wa watu bureee mwisho wapate korona!!!
Mbowe anavuna alicho kipanda.
eti anachagua Mahakama ya kusikiliza kesi yake!!
mwishowe atachagua na gereza la kutumikia kifungo chake!!
Huko nyumbani kwako wanaona unafundisha nini ?

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
Achana na huyo . Pingamizi zipo kisheria . Hata kumkataa Jaji kupo kisheria . Hilo lijamaa la hovyo
 
Mahakama Kuu Division ya Makosa ya Uhujumu Uchumi na Rushwa Leo Septemba Mosi, 2021 imetupilia mbali pingamizi lililowasilishwa na Mawakili wa upande wa utetezi, juu ya Mahakama hiyo kuwa na uwezo wa kusikiliza kesi ya Ugaidi.

Usikilizwaji wa kesi hiyo unaendelea.
Ni jambo jema.Naaamini kila mtu ana hamu ya kuona mwisho wa kesi hii.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom