Mahakama yatupilia mbali ombi la Afande Fatma kusomewa mashtaka popote alipo

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
1,105
2,637
Kesi inayomkabili 'Afande' Fatma Kigondo, anayeshtakiwa kwa kuratibu ubakaji na ulawiti wa kundi dhidi ya binti wa Yombo, Dovya jijini Dar es Salaam, imeendelea Oktoba 18, 2024, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma.

Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Nyamburi Tungaraja, ametupilia mbali maombi ya upande wa mlalamikaji yaliyotaka mshtakiwa asomewe mashtaka popote alipo, akisema maombi hayo hayajakidhi vigezo vya kisheria.

Maamuzi hayo yamekuja baada ya Jumatano, Oktoba 16, 2024, upande wa mlalamikaji kuwasilisha ombi hilo, ambapo Hakimu Tungaraja aliahidi kupitia sheria kabla ya kutoa maamuzi ya kusaini au kutosaini hati ya mashtaka kama ilivyoombwa.

Kigondo, anayekabiliwa na kesi hiyo nzito, amekuwa akishindwa kufika mahakamani mara kadhaa kwa sababu zinazodaiwa kuwa za kiafya.
Pia, Soma:

 
Kesi inayomkabili 'Afande' Fatma Kigondo, anayeshtakiwa kwa kuratibu ubakaji na ulawiti wa kundi dhidi ya binti wa Yombo, Dovya jijini Dar es Salaam, imeendelea Oktoba 18, 2024, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma...
Kumbe mahakama zetu zinaweza kuwa za kishenzi namna hii? This is to the extreme. Huyu ksho unamkuta High court akiwa Judge!
 
Taarifa zaidi hizi hapa

Screenshot_2024-10-18-13-07-13-1.png
Screenshot_2024-10-18-13-25-18-1.png

Swali letu ni hili, Je Ubakaji ule ulikuwa na Baraka kutoka Juu, Kwanini?
 
Back
Top Bottom