Mahakama yatupilia mbali mapingamizi ya utetezi, maelezo ya Mohamed Lingw'enya yapokelewa na Mahakama. Kesi kuu kuendelea Des. 15, 2021

Amani ya Nchi ni muhimu zaidi kuliko mwanasiasa yeyote yule.

Kamwe tusijaribu kuchezea au kufanya mchezo na Amani ya Nchi.

Mbowe sio MALAIKA.................................
Narudia tena na tena wewe ni MBWA koko unahitaji kipigo!
 
Tuliaminishwa humu kibatala ndiye wakili bora kabisa hapa nchini kwa sasa?
Mbona anagaragazwa hivi sasa na wakina Wa kili Kidando?

Unaweza kuwa na timu nzuri yenye wachezaji bora lakini refa akiamua kuwabania mfungwe hashindwi. Anachofanya Jaji Tiganga ni kuwapendelea upande was serikali. Jaji akiamua kupendelea hashindwi. Lakini hukumu hii inaeza ikazaa Jambo ambalo hatukulitegemea. Kama vile uchaguzi mkuu ulivyozua msiba mkubwa. Jaji anapingana na nature, na nature huwezi kupigana nayo utashinda. Refer kwa polepole kwa sasa anavyoangahika.
 
Unaweza kuwa na timu nzuri yenye wachezaji bora lakini refa akiamua kuwabania mfungwe hashindwi. Anachofanya Jaji Tiganga ni kuwapendelea upande was serikali. Jaji akiamua kupendelea hashindwi. Lakini hukumu hii inaeza ikazaa Jambo ambalo hatukulitegemea. Kama vile uchaguzi mkuu ulivyozua msiba mkubwa. Jaji anapingana na nature, na nature huwezi kupigana nayo utashinda. Refer kwa polepole kwa sasa anavyoangahika.

Kula tano mwanangu, hilo la kushindana na nature huwa nalisema sana humu. Hata sasa CCM inalazimisha kukaa madarakani lakini nature inakataa. Wanaiba kura ili wakae madarakani, matokeo yake wapinzani wamesusia hizo chaguzi, wapiga kura nao hawajitokezi tena! Huyo Jaji anapoteza muda tu. Hapo mawakili wa utetezi wakijitoa na kusema hawana imani na mahakama, basi mahakama itazidi kupoteza imani kwa umma. Na impact yake itakuwa kubwa.
 
Kweli mawakili wa Gaidi Mbowe na wenzake ni bure kabisa. Wanafanya court battle kwa kutegemea huruma ya akina Mmawia na tindo! Nafikiri ni wakati wa kuanzisha ashtag

#KIBATALA SIO ADVOCATE!!!!

Yaani mnadhani tuna imani na hizi mahakama, hivyo mnaamini tuna ujinga huo kuwa mawakili wa utetezi wanashindwa huko mahakamani. Ni kama box la kura hivi sasa, unaona kabisa wapiga kura hawajafika hata 100, kisha matokeo yakitoka unasikia CCM wamepata kura 500. Tulishaamka muda mrefu, upuuzi uliopo kwenye taasisi nyingi za umma, upo mahakamani pia. Hizo ndio dalili za mwisho za chama kupoteza uhalali wa utawala.

Kinachoendelea mahakamani kwasasa kwa sisi wasoma alama za nyakati, tunajua nini kitaenda kutokea kwenye utawala huu wa CCM.
 
Vipi ile kesi ambayo Mbowe alirudishiwa hela yake? Subiri rufaa,hawa majaji wa michongo na uvccm kuna muda wao
Majaji wanaosikiliza rufaa awachaguliwi na Rais au wao awasikilizi maelekezo toka juu?
 
Usikilizwaji wa Kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu; Halfan Bwire Hassan, Adamu Hassan Kasekwa na Mohammed Ling'wenya inatarajiwa kuendelea leo Desemba 14, 2021

Mahakama inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu pingamizi la Mshitakiwa Mohammed Ling'wenya, aliyepinga Mahakama kupokea kielelezo kinachodaiwa kuwa ni maelezo yake

======

Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake watatu inatarajiwa kuendelea kuunguruma leo huku mahakama ikitarajiwa kutoa uamuzi katika sehemu ya kwanza ya pingamizi la mshtakiwa mwenza na Mbowe.

Leo Jumanne Desemba 14, 2021 Jaji Joachim Tiganga wa Mahakama ya Kuu, Divisheni ya Makosa ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, anatarajia kutoa uamuzi katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi kutokana na upande wa utetezi kuweka pingamizi kuhusiana na malezo ya onyo ya mshtakiwa wa tatu katika kesi hiyo, Mohamed Ling'wenya.

Mawakili hao wa upande wa utetezi walipinga maelezo hayo yaliyotolewa na SP Jumanne yasipokelewe na mahakama kwa sababu mshtakiwa huyo alilazimishwa kusaini na wala hajawahi kufikishwa kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam.

Tayari washtakiwa tayari wameshafikishwa mahakamani kwa ajili ya kuendelea na kesi hiyo.

Pia, awakili wa pande zote mbili nao wameshafika katika Mahakama kwa ajili ya kusikiliza uamuzi katika kesi ndiogo ndani ya kesi ya msingi.

Kwa sasa anayesubiriwa ni Jaji Tiganga kuingia mahakama

Mbowe na wenzake wanakabiliwa na kesi ya uhujumu Uchumi namba 16/2021 yenye mashtaka sita yakiwemo ya kula njama na kufadhili vitendo vya kigaidi.

Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa hayo katika maeneo Moshi, Arusha na Dar es Salaam.

Chanzo: Mwananchi
===

UPDATES

Jaji ameingia Mahakamani Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa.

Wakili wa Serikali Robert Kidando anatambulisha Jopo la Mawakili wa Serikali
1. Pius Hilla
2. Abdallah Chavula
3. Jenitreza Kitali
4. Nassoro Katuga
5. Esther Martin
6. Tulimanywa Majige
7. Ignasi Mwinuka

Wakili Peter Kibatala anatambulisha Jopo la Mawakili wa Utetezi
1. Nashon Nkungu
2. John Malya
3. Fredrick Kihwelo
4. Dickson Matata
5. Seleman Matauka
6. Edward Heche
7. Alex Massaba
8. Gaston Garubindi
9. Sisty Aloyce

Jaji anaita Washtakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani....

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kutolewa Uamuzi tupo tayari Mheshimiwa

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji, Na sisi Pia Kwa Ruhusa yako tupo tayari

- Jaji anaandika Kidogo, Mahakama ipo kimya

Jaji: Shauri hili ni kweli lina kuja kwa ajili ya Uamuzi ambao ulikuwa really served Mahakama ilielekeza Mawakili Walete Hoja zao Kwa Maandishi ambapo wameleta.

Wakati shahidi namba 08 ASP Jumanne Wakati Wa Kutoa Ushahidi Wake alieleza Kwamba alipewa kazi ya Kuandika Maelezo ya Mshitakiwa Wa tatu, Na baada ya Kueleza hivyo aliomba Maelezo hayo ya pokelewa Mahakamani, Ambapo Upande wa Utetezi Walipinga kwa Sababu 9.

Sababu ya Kwanza ni Mshitakiwa namba tatu hakuwa Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam.. Na Haku andika Maelezo yoyote.

Sababu ya Pili Mshitakiwa Wa tatu alilazimishwa Kuweka Sahihi katika Maandishi ambapo pia Pamoja na Kulazimishwa hakupewa nafasi ya Kusoma Maelezo yake.. Alitishwa na Goodluck Minja na ASP Jumanne alimtishia Kwamba Asipoweka atateswa Kama alivyoteswa Moshi.

Sababu ya 3 ni kwamba Maelezo yake yalirekodiwa Nje ya Muda, yalirekodiwa Siku ya Tarehe 09 August 2020 wakati amekamatwa 05 August 2020.

Sababu ya 4 ni kwamba Maelezo ya Onyo yalikuwa a yameandikwa kwa Sheria ya Kifungu 57((1) Ilivyofanyiwa Marejeo 2020 ambapo Sheria hiyo haipo.

Sababu Nyingine NI kwamba alionywa kwa Sheria ya Kuzuia na Kupambama na Ugaidi wakati sheria hiyo haipo.

Sababu Nyingine NI Maelezo ambayo yanalengwa Kutolewa Mahakamani yapo Tofauti na yale Yaliyotolewa wakati wa Commital kwa Kutofautisha Subsection.

Sababu ya Saba Hakuna Kifungu Kinachoonekana Kwamba wamechukua Maelezo na Kushitaki kwa kifungu kipi.

Kutokana na Hoja zote Mbili zilizo letwa zilikuwa zinaangukia katika Sheria ya Ushahidi ambapo ilipelekea Kuwepo Kwa Kesi Ndogo
Kwa hiyo Mapingamizi hayo yalishughulikiwa kwa Njia ya Kuleta Hoja Mahakamani.


Na Kwamba Baada ya Kesi Ndogo Submission ziletwe kwa Kuleta Hoja ya Kuunga Mkono kuhusu Mapingamizi Yanayo angukia Katika Sheria ya Ushahidi.


Jaji: Katika Kesi Ndogo Upande wa Mashtaka wenye Jukumu La Kuleta Mashahidi wa Kuthibitisha.. Walileta Mashahidi wanne..
ASP Jumanne, Goodluck Minja, ISSA Maulid Msemwa na walileta Vielelezo, Barua ya Msajili Kama Kielelezo namba 1, Detention Register kama Kielelezo Namba 2 na Kielelezo namba 3.

Jaji: Kwa Upande wa Utetezi walileta Mashahidi Watatu, Kielelezo Namba Moja Maelezo Ya GOODLUCK Minja, Nakala ya Hati ya Mashtaka , Dispatch Book, Nakala ya Hati ya Mashtaka ya Kesi namba 17/2020, Nakala ya Hati ya Mashtaka Ya Shahidi namba tatu kesi 63/2020 020. Na Kielelezo Kingine ni Diary ambayo Ulichukukiwa wakati WA shahidi Wa Mashtaka Anatoa Ushahidi Wake, Sababu Pande zote hawajazungumzia Kwa Kirefu Kielelezo Hiki basi na Mimi sitoongelea kwa akirefu Kielelezo Hiki, Mahakama haina Nia ya Kurejea Maelezo Ya Ushahidi wote.

Jaji: Suala la Kutafuta Ukweli kwa Hoja namba Moja na Mbili na Hoja namba Tatu Mpaka namba Saba zilikuwa resolved Kwa submission zilizopangiwa parties Mahakamami... Ni Utaratibu wa Kawaida mambo yanayohusu Sheria Kuamuliwa kwanza..

Kwenda Kwenye Hoja za Kisheria si Sawa, Ni Vizuri kwenda Kwenye Hoja za Ushahidi Kwanza, Kwa sababu hiyo Tutaanza Mambo yanayuhusu Ushahidi kabla Mambo ya Kisheria.

Kwa Mujibu wa Sheria ya Ushahidi Sura ya 6 Kifungu 57 (1) pale ambapo Utetezi wa Napinga Maelezo ni Wajibu wa Mashitaka Kuthibitisha, Pasipo Kuacha Shaka.

Kutokana na Ushahidi Wa shahidi namba Moja na Shahidi Nmab tatu ndiyo Waliokwepo Wakati Wa naandika Maelezo, Kwa Mujibu wa Ushahidi Wao walimkamata Mshtakiwa Huko Rau Madukani.

Kwamba Wakati wanawakamata Walikuwa na Mwenzao Moses Lijenje, Na Washitakiwa kwa ridhaa yao Waliongoza Zoezi la Kumtafuta Moses Lijenje Katika Maeneo ya Moshi na Wilaya ya Hai, Kwa amba Baada ya Kushindwa Kumpata Siku ya Tarehe 06 August 2020 Walianza Safari kuja Dar es Salaam.


Jaji: Na wakiwa kabidhi Sehemu ya a Mapokezi na a Ada ya hapo waliondoka Kwenda Kufanya Usafi, Na Kwamba walipokelewa na DC Msemwa.. Na walirudi tena kumuhitaji Mshtakiwa Namba tatu Kuja Kumuandika maelezo kwa ajili ya Kuandika Maelezo yake ya onyo na Kwamba Mshitakiwa Alitoa Maelezo yake kwa hiari yake, Ushahidi Wake uliungwa Mkono na Shahidi namba Mbili, alieleza kwamba aliwapokea baada ya Washtakiwa Kufikishiwa Kwake na Kuwaingiza Kwenye Kumbukumbu ya DETENTION REGISTER..

Kwa Mujibu wa Ushahidi Huo yeye anashuhudia Kwapo Katika Kituo hicho, Anashuhudia kuwa pokea na Kumtoa tena kisha kumpokea tena Mshtakiwa Namba tatu.. Mshtakiwa namba tatu aliporudishwa alikuwa kwenye hali Nzuri. Na Shahidi namba Moja anaendelea Kusema Kwamba Baada ya Kumalizia Kumuandika Maelezo na Kumsomea kisha akamrudisha tena Mahabusu.

Jaji: Ushahidi huu ulipingwa na Upande Wa Utetezi ambapo Mshtakiwa Watatu alitoa Ushahidi Wake Kwamba hajawahi Kufika katika Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam. Walipofikishwa Dar es Salaam Walifikia Kituo cha Polisi Tazara na Kupelekwa Mbweni ambapo alichukuliwa kwenye Chumba alichokuwepo Kupelekwa Chumba Kingine na kisha Kulazimishwa Kusaini Maelezo, Maelezo yoyote yanayosema Kwamba aliyatoa ni ya Uongo.

Akaendelea Kusema Kwamba Upande wa Mashtaka Umeshinda Kuthibitisha kwamba Msemwa alikuwepo Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam Siku hiyo.

Jaji: Hata alipoulizwa alishindwa Kusema aliwapokea zamu yake, Shahidi wa Pili yeye alisema Kwamba alikamatwa huko Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro na Kuletwa Kituo Cha Polisi Oysterbay alimkuta Msemwa. Na Kwamba Kwa Sababu hakuwa amekula alimuagiza Afande Msemwa akamchukulie Chakula na Akaendelea Kuwa Rafiki ya Afande Msemwa.. Na Kwamba hata Baada ya Kupelekwa Mahakamani alirudishwa tena Kituo cha Polisi Oysterbay kwa Siku 19.

Kwa muda wote huo si kweli Kwamba Msemwa alikuwa Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam, Na Kwamba alipokuwa alifuatilia Kesi aligundua Kuwa Msemwa aliongopea Mahakamani Kwamba alikuwa Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam.

Aliwasilina na Wakili Wake kisha anapewa Utaratibu Wa a kupata Nyaraka Kwa ajili ya kuzileta Mahakamani, Alipozileta Upande wa Mashtaka Walipinga lakini Mahakama Inaona ni Busara Kuzipokea.

Jaji: Upande wa Utetezi Wakamleta tena Shahidi Wa tatu, Bwana Mhina ambaye alikamatwa huko Kwao Tabora.. Na wakati wote huko alikuwa anaulizwa kama anamfahamu Mshtakiwa namba Nne na Mshtakiwa Namba tatu.

Ambapo yeye alisema Kwamba alifanya naye kazi wakati fulani, Pamoja na Kuwaeleza Ukweli lakini waliendelea kumshikilia, Na Baadae Kashtakiwa na Kupelekwa Gerezani ambapo Alikutana na Mshtakiwa Namba tatu.

Akasema Kwamba Kwenye Hati ya Mashtaka palikuwa Pameandikwa Majina ya Washitakiwa na pembeni Gereza aliokuwa anashikiliwa.. Yeye alikuwa anashikiliwa na Mshtakiwa Namba tatu Segerea.

Kwa Upande wa Utetezi walionyesha Kwamba Kwa namna gani Mshtakiwa namba tatu hakuwepo Kituo cha Polisi na Upande Wa Mashtaka walikuwa wanaonyesha Kwamba alikuwepo Kituo cha Polisi.

Jaji: Kama nilivyosema Mwanzo Upande wa Mashtaka ndiyo wanalo Jukumu la Kuthibitisha Pasipo Kuacha Shaka, Mzigo Wa uthibitishaji wa Shauri kutoka Upande Wa Mashtaka, Upande wa Utetezi Kazi yake Kubwa ni Kuonyesha mashaka ambayo yanaweza Kuwa Resolved Kwa Favour ya Mshtakiwa.

Hii ni Kwa Sheria Kesi ya JOSEPH Vs JAMHURI Kesi 44 ya 1986, Jambo la Msingi Mshitakiwa Alikuwa wapi, Upande wa Mashtaka Wanasema Mshitakiwa namba tatu alikuwa katika kituoa cha Polisi Kati Dar es Salaam.

Kwa Kuleta Detention Register Kuonyesha alifika a Kituo cha Central Police, Shahidi Namba Mbili anasema Kwamba alimpokea Mshitakiwa na Kumuongoza Kwenye Kielelezo Namba 2 cha Detention Register, Kwa Msingi huo wao Ndiyo Ushahidi Wao.

Jaji: Upande wa Utetezi Wao Wana kana na Ushahidi Wa kukana Umejengwa Kwa a Shahidi Namba Moja na Shahidi namba tatu, Kwamba Ushahidi Waliotoa haujaungwa Mkono na Maelezo yoyote Kwamba Kweli walikuwa Kwenye Kituo Cha Polisi Kati Dar es Salaam.

Kwa upande Wa Utetezi Wa naomba Kwa Mujibu is a PGO namba 284(4,5,6) kwa kusokekana kwa Occurance Book Kuonyesha Ni kweli Kwamba Msemwa Alikwepo kazini Siku hiyo, Hakuna Ushahidi Wa Polisi Incharge pia.

Wakaendelea Kusema hata shahidi namba Mbili alipoulizwa Maswali alishindwa Kuwataja aliwapokea zamu na hata waliompokea, Kinyume na Station Diary ambapo inatakiwa Kuonyesha Matukio yote.

Hata Kielelezo namba 2 kina Mapungufu kwa a Kutolewa kwake Kilipokuwa huko Polisi, Kwa sababu hiyo Mahakama a inatakiwa Ione Mashaka Kwamba hakija kidhi..... Kwa Kesi ya ISAYA Vs JAMHURI 115 ya Mwaka 2019.

Kwa Ushahidi Ulitolewa na Shahidi namba 03, na Kwamba Walipo kutana Mahakamani na Gerezani aliambiwa na Mshitakiwa Namba tatu Kwamba Haku fikishwa Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam Bali Tazara.

Wakati napokea Vielelezo nikisema Mwisho nitaangalia na Kuona Kwamba Vielelezo hivyo ni Relevant, Niliombwa Kuangalia Kielelezo namba Mbili, Mahakama Ichunguze Ione kwamba Hapakuwa na Muunganiko Wa Kielelezo hicho na Swala la Kielelezo Kimetolewaje Mahakamani.

Jaji: Ikumbukwe Kwamba Kielelezo Hiki kilisha pokelewa na Jaji Siyani Na Fikiri siyo Sawa Kuangalia Kielelezo Hicho tena Wakati Kielelezo Hicho Kilishatolewa Uamuzi wa Mahakama.. Kwa sababu hiyo Mahakama inatupilia mbali Hoja hiyo.

Kuhusiana na Hoja namba Tatu Kwamba Mshtakiwa Alikuwepo Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam.. Inahusu Mashahidi Namba Moja na namba Mbili.. Namba Moja anasema Walipo toka Moshi walifika Moja kwa Moja Polisi Kati Dar es Salaam.

Na Wanaonyesha Kwamba jina la Mshtakiwa Namba tatu lipo kwenye Detention Register, Ushahidi Unaonyesha Kwamba Mshtakiwa aliingizwa Kwenye Kituo hicho.. Na Kwamba alitolewa kwa ajili ya Upelelezi.

Jaji: Swali ambalo Mahakama Inajiuliza ni Je ni Ushahidi Wa Kuaminika? Mahakama Inatizama Ushahidi huo kama Ushahidi unapaswa Kuungwa mkono.. Mahakama Katika aina ya Ushahidi unapaswa Kuungwa Mkono, Mahakama Inaona Ushahidi Unatolewa Chini ya Kiapo unapaswa Kuungwa Mkono.

Kwa Mujibu wa Kesi Mvumi Mpenda Vs JAMHURI 327 ya 2016, Na Maelezo ya Marehemu wakati anafariki, Maelezo Ya Mtoto pia.. Sheria Kesi ya Frank Joseph Vs JAMHURI.. Ushahidi ambao imebase kwa Habari ya Kusikia Unatakiwa Kuungwa Mkono.

Ukiangalia aina ya Ushahidi wa a Kuungwa Mkono Utaona Ushahidi Wa Shahidi namba 2 hauangukii katika Miongoni Mwa Ushahidi niliotaja, Kwa maelezo Kwamba alipofika Polisi alimkuta Shahidi Wa Pili.

Mahakama Inaona Kwamba Pamoja na Kwamba Ushahidi Wa shahidi namba Mbili siyo wa Kuungwa Mkono, Basi Ushahidi Wake unaungwa Mkono na Shahidi namba Mbili.

Jaji: Kama ilivyo Kwenye kesi ya Goodluck KYANDO Vs JAMHURI ni Ushahidi ambao Unaaminika.. Kama nilivyosema Kwamba Upande wa Utetezi Jukumu lao ni Kuonyesha mashaka.. Ilikusudi waweze Kuleta Mashaka, Walitakiwa watengeneze Mashaka.

Shahidi Namba 1 Mbaye ni Mshtakiwa namba tatu anapo Sema kwamba Alikuwa Kituo cha Polisi Tazara Ndiyo Mashaka Yenyewe, Mujibu wa Sheria Jukumu la Kuthibitisha Jambo lolote ambalo Mtu a alisema inakuwa Kwake yeye labda Kwa Mujibu wa Sheria it atakiwa itihibitishwe na Mtu Mwingine.

Kwa sababu hiyo Basi Mshtakiwa Alikuwa na Jukumu la Kuonyesha ni Kweli alikuwa Kituo Cha Tazara, Mzigo Huo unakuwa Mwepesi Kwake.. Wakati anapitia Ushahidi Kuhusiana na Jambo hili, Ambapo Mshtakiwa alisema Kwamba alikuwa katika kituo cha Tazara yeye na Mshtakiwa Namba MbiliKumbe alikuwa na Mtu aliyemuona Akiwa Kwenye Kituo cha Tazara lakini Kwa Bahati Mbaya Mshtakiwa namba tatu ameshindwa Kumuita Shahidi huyo Kutoa Ushahidi Wake Mahakamani.

Badala yake alimuita shahidi namba tatu ambaye anasema alipofika Kituo Cha Tazara Hakumkuta Kituo cha Polisi Tazara.. Lakini pia katika Ushahidi Wake Mshtakiwa Namba tatu Haikuelezea.

Jaji: Shahidi namba 3 kwa kutumia Kielelezo ambacho ni Hati ya Mashitaka ambayo inaonyesha Jina Mshtakiwa na Gereza alikuwemo.. Kwa Kuzingatia Hati hiyo Hakuna Sehemu Inayoonyesha Kwamba Walikwepo Katika Germany za la Segerea.

Basi Mahakama inatilia Mashaka Ushahidi huo.. Shahidi huyo namba tatu alikabidhiwa Detention Register Ya Tazara alisema Jina lake halikwemo na Pia Jina la Mshitakiwa Namba tatu hakuwepo Katika Detention Register.

Kwa sababu Hiyo Mahakama Unapata Mashaka Kwamba Mshtakiwa namba tatu alikuwepo Kituo cha Polisi Tazara.. Na Shahidi Wa Pili alisema Kwamba Hapakuwa na Uwezekano Kwamba Msemwa alikuwa anafanya Kazi Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam.

Na Kwa Maelezo hayo alileta Vielelezo ambapo ni Dispatch, Hati ya Mashitaka na Vingine, Ukitazama Vielelezo Vyote hivyo Hakuna Uhusiano wa Moja kwa Moja Na Kesi iliyopo Mahakamani.. Na Kwamba Mahakama Inaona Kwamba Vielelezo hivi haiwezi Kuisaidia Mahakama.

Jaji: Ushahidi Unatolewa ni Kuhusu Tarehe 14 May 2020 Wakati Jambo Linalobishaniwa hapa ni 07 August 2020.. Labda kama Ingekuwa shahidi huyo Alikuwapo Oysterbay Siku ya Tarehe 07 August 2020, Katika Mazingira hayo Mahakama Inaona Value yake ni ziro na haiwezi KuSaidia Mahakama.

Jaji: Kwa Upande wa Mashtaka waliweza Kueleza Kwamba Shahidi Alikuwa ni Shahidi Mwenye Maslahi.. Kwamba Katika Ushahidi Wake ulikuwa wenye Kujikanganya, Hasa pale Aliposema Kwamba alimuelekeza DC Msemwa akachukue Fedha katika PPR yake Wakati Alisha Sema alipokamatwa hakuwa na Kitu chochote huko Mwanga.. Na hakutoa PPR yake hapa Mahakamani, na Hivyo ni Ushahidi Wenye Kujikanganya.. Mara ya Kwanza alisema Kwamba alitambua DC Msemwa Baada ya Kusoma Jina Lake Katika Uniform na alipoulizwa mara ya Pili alisema Kwamba alitambua anmab yake H4323

Alishindwa Kuoanisha Jina namba aliyo Sema Mara ya Pili, Kushindwa Kuonyesha Wajihi Wa DC Msemwa.. Alishindwa Kutoa Discription Nzuri ya Shahidi Huyo, Mwanzo alisema Kwamba ni Mweusi na Mnene na alipoulizwa tena akasema Kwamba anaweza Kuwa Mnene au Siyo Mnene.

Mahakama ya Rufaa Iliyoketi huko Arusha inasema Kwamba Siyo Kila Mkanganyiko unafanya Mahakama Isiamini Ushahidi Huo, Mahakama Inajiuliza Kwamba Je Mkanganyiko huo ni Mkanganyiko wa Kawaida ambao Mahakama Inapaswa Kuupuuza?

Mahakama Inaangaliwa Kuhusu Maelezo Yaliyotolewa, Katika Mazingira hayo Ukiangalia Contradiction ni Contradiction siyo Nyepesi kwa sababu hiyo Basi Mahakama inatilia Mashaka Ushahidi Wake.. Ni wazi Pia Ushahidi Unaotakiwa Kutengeneza Mashaka hautakiwi wenyewe Kutiliwa Mashaka.

Jaji: Wote waliokuja kuzungumza wamejichanganya.. Na Juu ya maslahi kwamba ni shahidi mwenye maslahi, Ni kweli amesema kwamba amekuwa haridhiki kuanzia Kesi mpaka Kwa Jaji mwenyewe. Mahakama inaona yeye ni Shahidi wa hisia ambaye amekuja mahakamani kutoa hisia zake.

Jaji: Mahakama Inaona Kwamba Kuhusiana na Ushahidi Alikuwepo Kituo cha Polisi Oysterbay wakati Mshtakiwa namba tatu alikuwa Tazara, Mahakama Inaona kwamba Ushahidi Ulioletwa na Upande wa Mashtaka haujaweza Kutikiswa. Na Kwa sababu Hiyo Pingamizi la Kwanza Kwamba Mshtakiwa hakuwepo Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam siyo la Msingi na Mahakama inatupilia Mbali.

Jaji: Kwa Maana hiyo sasa Kwamba Mshitakiwa namba tatu aliteswa na Alilazimishwa Kuweka Sahihi yake na Kwamba aliweka Sahihi yake baada ya ASP Jumanne Kumtishia Kwamba angeteswa kama alivyoteswa Moshi, Na Kwa namna ambayo alikuwa ametishwa hakupewa Kusaini.

Ikumbukwe Kwamba Maelezo Yanayibishaniwa no Yale Yaliyotolewa alipokuwa Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam, Upande wa Mashitaka unapaswa Kuthibitisha Kwamba Hapakwepo na Mateso, Na Kwa sababu Ya Upande Wa Mashitaka Ulikuwa Jukumu hilo.

Wao wanasema Mshitakiwa Namba tatu hakuteswa na Kwamba Wao Tarehe 08 August 2020 Walipo wa kabidhi Washitakiwa Mbweni hawakurudi tena, Na Kwa Mujibu ya Maelezo Yao, Maelezo ambayo anataka ni yale aliyotatoa akiwa Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam.

Jaji: Kwamba Mshitakiwa aliteswa Na Goodluck na Mahita kwa kuulizwa Maswali Juu ya Uhusiano Wake na Mshtakiwa Namba 4... Mshitakiwa anasema walimuuliza Maswali Mengi na walikuwa wanamrekodi na Baada ya hapo Walimpeleka Kituo cha Mbweni.

Kitu ambacho Upande wa Mashitaka Unapinga, Wakati wa Ushahidi Wake Hakusema Alivyoteswa na alivyotishwa akiwa Kituo cha Polisi Mbweni.. Kwa maelezo yake yeye Kwamba alifikishwa Mbweni akitokea Kituo cha Polisi Tazara.

Na Kwamba Siku ya Tarehe 10 Walimpeleka Kwenye Ofisi ya Upelelezi ambapo Jumanne na Goodluck Ndiyo walimtishia.. Na Kwamba alipokuwa amekaa aligeuka akamuona Goodluck akiwa na Pistol na Kumwambia Kwamba Asipo Saini watamfanya kama Moshi.

Jaji: Upande wa Utetezi hujaeleza Kwa Namna gani Upande wa Mashtaka Umeshindwa Kuthibitisha Kwamba hakuteswa.. Wakaomba Pia Mahakama Kujikimbusha PGO 353 (2) kwamba Mshitakiwa anatakiwa aku fikishwa kwa Daktari, hiyo ingeondoa Mashaka kama Mshtakiwa hajateswa Kwa Sababu hiyo Basi Upande wa Utetezi Wakaomba Mahakama Ione kwamba Mshitakiwa alitishwa, Mahakama inalo jukumu la Kuangalia Ushahidi Wa Mtu Mmoja Mmoja na Maelezo ya Mshtakiwa.

Kwa Ushahidi Wa Mshtakiwa namba tatu Kwamba alitshwa alipokuwa Kituo cha Polisi Mbweni na Kwamba Kama Asipo Saini Mateso ya Moshi yatajirudia, Kwa sababu hiyo Maelezo yanayopaswa Kutolewa yeye hayatambui.

Wakati anatoa Ushahidi Wake, Wakili Wa Serikali Alimuuliza ni Kweli Kwamba Yeye alitshwa Tarehe 08 August 2020, Akauliza Je Kama Adamoo alitolewa tarehe 09 August 2020.. Akasema hajui itakuwaje.

Jaji: Hoja za Mawakili Zina onyesha Kwamba Shahidi Aliteswa Tarehe 09 August 2020, Na Kwamba Hoja ya tatu Ya Maelezo Yaliandikwa Nje ya amuda wao Wameandika tarehe 09 August 2020, Ni wazi pale panapokiwa na Ushahidi Unapingana na Submission ni wazi Ushahidi unapaswa uaminike kwa sababu Submission ni Ufafanuzi wa Ushahidi, Katika Mazingira hayo Mahakama inarejea Maaamuzi yake wakati ina' resolve Mgogoro wa kwanza. Mahakama imeshindwa Ku' examine ni Tarehe gani Mshtakiwa aliteswa, Kwa sababu hiyo Basi Mahakama inabakia na Mkanganyiko.

Jaji: Na Kwa PGO ya 353 ya Kuhusu Kumpeleka Shahidi Kwa Daktari haiwezi Kusaidia Kwa sababu Mahakama ipo Kwemye Dilemma. Mahakama Inaona Sababu ya 2 ya Pingamizi Inaona Upande Wa Utetezi Umeshindwa Kujenga Vizuri na Kwa sababu hiyo Mahakama ina overule na Kutupa Pingamizi hilo.

Jaji: Nakuja sasa Kwenye Hoja za Kisheria Kwamba Maelezo yalichukuliwa Nje ya Muda.. Mahakama Inakubaliana Kwamba Mshtakiwa Alikamatwa Tarehe 05 August 2020 na Kwamba Maelezo Yalichukuliwa Tarehe 07 August 2020.

Mahakama Inarejea Sheria Kwamba Maelezo Yanatakiwa Kuchukuliwa ndani ya masaa Manne, Na Kwamba Kinyume na hapo panapaswa kuwa na Kibali Maalum, Ni kweli Maelezo hayo yameandikwa Nje ya Muda wa Zaidi ya Masaa 40.

Lakini Kifungu kichofuata kinasema Kwamba pale ambapo Mshitakiwa anakuwa amekamatwa na Taratibu Za Kiupelelezi zinaendelea basi Muda huo unapaswa uondolewe.

Kwa maelezo Kwamba Walikuwa na Moses Lijenje na Kwamba Haku kamatwa, Walitumia Siku iliyibakia ya a tarehe 05 August 2020 Walitumia Muda uliobakia Kumtafuta Moses Lijenje.. Na Kesho Yake waliendelea Kumtafuta sehemu Mbalimbali Kwa Kubase Kwenye Ushahidi Huo Wa Upande wa Mashitaka, Upande Wa Utetezi walieleza Kwamba Yapo Mapungufu Mengi yamaonekana.. Wanasema Maelezo hayo hayaonyeshi Kwamba palikuwa na Katazo Kutoka kwa DCI kuwa fanya Wasiandike maelezo hayo Hapo Moshi.

Kwamba Zoezi La Kumtafuta Lijenje Lilijawa na Mapungufu Mengi.. Wakaomba Mahakama Izingatie Hoja zao Kwa Kutumia Kesi zifuatazo, DPP Vs James, Massa we Vs JAMHURI, Aphonce Vs JAMHURI, Hamis Chuma Vs JAMHURI.

Jaji: Wakati Kifungu cha 50(2) kinasema Kwamba Muda hautohesabika kama Mshitakiwa atasafirishwa, Uzito wa Kesi yenyewe, Muda huo hautohesabika.. Kesi ya Mendez inasema kwamba Si Kila Kutofuatwa Kwa Sheria Kuna ondoa Uzito wa Ushahidi wenyewe.

Mahakama Imekwisha Kusema Kwamba Mara baada ya Washitakiwa Kukamatwa palikuwa na Taarifa Y a Kutokamatwa Kwa Moses Lijenje, Kwamba Walikamata Washitakiwa Wawili na Mmoja alikuwa ameshaondoka, Kwa namna hiyo basi Washitakiwa Walikuwa watatu na Mmoja aliweza Ku Dissappear.

Jaji: Kwa Askari Wanaojua kazi zao asingeweza Kurelax na Kukaa bila Kumtafuta Mshtakiwa Wa tatu.. Ni wazi Kwa Upande Wa Mashitaka Ushahidi Wao Hautakiwi Kutiliwa shaka.. Ni wazi Pia Upande Wa Utetezi Wameeleza Kwamba Kifungu 50(1) ni wazi ilitumgwa kwa uwezekano wa Kuondoshwa. kwa Kuteswa kwa Washtakiwa.. Katika hali hiyo ni wazi Kwamba, Kwa Hoja ya Upande wa Utetezi Ushahidi Unatolewa na Upande Wa Mashitaka Hakuna al Mashiko kwa Kutengeneza Mashaka.

Pamoja na Hoja zao hizo za Utetezi , lakini ni wazi Kwamba Ushahidi huo wa Mashitaka Umeletwa Kwa Uzito wake siyo wa Kupuuza, Mahakama unapokuwa inataka Kuyapa Uzito Maelezo Hayo Mahakama Inapaswa kungalia Mazingira yote. Kwa Maoni yangu hatua tuliyopo ni Hatua Ya Kupokea Maelezo Ya Onyo, Mahakama Haiwezi Kuzungumzia Uzito wake, Hoja ya Kwamba Mahakama Ione Uzito wa Maelezo Yenyewe Mahakama Inaona Imeletwa Kabla ya Wakati.

Kesi mbalimbali zinasisitiza Kwamba Yakiwepo Maelezo Ya Kutosha Yanayao Onyesha Kama a palikuwa na Sababu ya Kutosha Kuandaa Maelezo Basi Sababu hiyo inatosha Kupokea Maelezo Hayo, Maelezo ya a kwamba Shauri lilikuwa limegumguliwa Dar es Salaam basi palikuwa na Sababu ya Msingi Maelezo Kuyachukulia Dar es Salaam, Kuwasafirisha Washitakiwa Kutoka Sehemu Moja Kwenda Nyingine Mahakama Inamaoni Kwamba Kwa Namna Maelezo Yaliyotolewa, Mahakama Inaona Katika Mazingira haya ilikuwa ni sahihi itumike Kwa sababu hiyo Pingamizi la Tatu natupilia Mbali.

Jaji: Kuhusu Pingamizi la Nne kuhusu Verification, Katika Upande wa Utetezi Wameomba Mahakama Ione Umuhimu wa Verification, Kwamba Mahakama ilisema Kwamba Kutoa kuandika Sheria Kwa Usahihi ni Fatal. Hakuna Sehemu yoyote ambapo ASP Jumanne alikuwa akisahihisha Wakaomba Mahakama Ikatae Kielelezo Hicho, Suala Zima La Uhuru Wa mtu unapokuwa anachukiliwa Maelezo, Siyo lazima Ionyeshe Umeathirika Vipi.. Wakaomba Mahakama ikilatae Kielelezo hicho, Ni nakubaliana na Upande wa Utetezi Kwamba Mahakama Ilikuwa Inapokea Kielelezo Mara ya Kwanza.

Mahama Inaona Kwamba Katika Mazingira Fulani fulani Mahakama Ya Rufani imekuwa Ikilaumu kutokupolea Kielelezo, Basi Kwa Sababu hiyo Pingamizi hili pia naona halina Mashiko.

Jaji: Kwa Pingamizi la Tano pia Kuhusu Subsection na kunukuu Sheria ambayo haipo, Katika Kukosea kutaja Sheria, Hakufanyi Nyaraka Kukataliwa Mahakamani.

Katika Maamuzi Hayo nimezingatia Kesi ya JAMES NA SONGOROKA basi Kwa Namna hiyo pia natupilia Mbali Pingamizi hilo.


Jaji: Kwamba Kwa sasa Mahakama Ya Rufani imekuwa Unachukua Msimamo Tofauti, Kwamba Unapokuwa Umwrejea tofauti Sheria Kwamba Jambo hilo aliwezi Kupokelewa, Kesi Ya JAMES MWAMULE na SYKES Mahakama Inaona Kwamba Kurejea Kimakosa Kwenye Verification kumeathiri Haki ya Mshitakiwa kwa namna gani, Basi Kwa Sababu hiyo natupilia Mbali Pingamizi hilo.

Jaji: Kwamba Kwa sasa Mahakama Ya Rufani imekuwa Unachukua Msimamo Tofauti, Kwamba Unapokuwa Umwrejea tofauti Sheria Kwamba Jambo hilo aliwezi Kupokelewa, Kesi Ya JAMES MWAMULE na SYKES Mahakama Inaona Kwamba Kurejea Kimakosa Kwenye Verification kumeathiri Haki ya Mshitakiwa kwa namna gani, Basi Kwa Sababu hiyo natupilia Mbali Pingamizi hilo.


Jaji: Hoja ya Saba Ni kwamba Katika Kifungu cha 57 Mshitakiwa anapokuwa ameonyesha Kukiri anatakiwa kuonywa Upya, Na anapokuwa ameonywa basi Hapo Ndipo Maelezo Yanatakiwa Kuandikwa, Ni wazi Kwa Kungalia hilo aionyeshi Mshitakiwa Alihojiwa kwa Kufuata taratibu gani kati ya hizo 2.


Niseme Jambo hilo na Hoja hii Pamoja na Kwamba Ilikuwa a raised Mwanzo, Mawakili wamesema kwamba hawajazungumza.. Kwa Maana hiyo Mahakama inapata Benefit ya pekee kutoka kwa Upande wa Mashitaka.. Pamoja na Kwamba Hoja hiyo haijaelezwa na Upande Wa Utetezi lakini Mahakama ameona ni Vema Ipitie Hoja hiyo.

Kinachotakiwa ni Format tu na siyo Kifungu Kipi Kimetumika.. Kwa hiyo iwe Kwa Kifungu cha 51 au 57 kwa Kufuata Utaratibu huo Kama. Hakuna Maelezo Ya Mshtakiwa alivyoathirika.. Mahakama Inaona Hoja ya Saba haina Mashiko na naitupilia mbali.

Jaji: Hoja zote saba hazina mashiko na hasa kwenye kesi ndogo ushahidi ulioletwa na upande Wa mashtaka umeshindwa Kutingishwa... Kwa sababu hiyo Basi mapingamizi yote nayatupilia mbali..

NATOA AMRI!

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Utoe Amri tuweze Kurejeshewa Kielelezo Ambacho ni Dispatch..

Jaji: na Hivi Vingine?

Wakili Peter Kibatala: vibakie, kwa sababu Vinaweza Kutumika hata Mahakama ya Rufaa huko Mbeleni ila hiki Kinatumika na Ofisi.

Jaji: nimepokea Hoja, na kwamba vielelezo ambavyo vilitolewa kwenye kesi ndogo virudishwe kwa wenyewe na ninaelekeza maafisa wa Mahakama Kabla hawajarudisha watoe Copy NATOA AMRI Mawakili wa pande zote mbili wanakubaliana na Uamuzi Jaji kwa Kusimama na Kumuinamia kimasta zaidi.

Jaji: mara ya Mwisho tuliishia Kwenye ombi la Kutaka Kupokea Maelezo, Sasa Mahakama Inapokea Maelezo hayo NATOA AMRI Tuendelee na Shahidi.

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shahidi Wetu ASP Jumanne ameshindwa Kufika Mahakamani Pamoja na Kumpatia Taarifa Leo awe Maeneo Jirani.

Kibatala:
Mhe Jaji Shahidi alishaonywa na Kwamba Leo alikuwa awe hapa, Sisi wengine tulitakiwa tuwe Likizo lakini Kwa sababu ya Maslahi ya wateja Wetu Tumekubaliana Kuendesha Kesi wakati huu Wa Mahakama Inapokuwa Likizo, Tunaomba Kutoa Masikitiko yetu na Kesho akifika ajieleze.

Jaji: Nakubalina na wewe, Kesho aonyeshe Uungwana kwa Kuonyesha Uthibitisho Kwamba alikuwa anaumwa kabla ya kutoa Ushahidi Wake.

Jaji: Basi shauri linahairishwa mpaka kesho tarehe 15 December 2021, washtakiwa wataendelea kuwa rumande chini ya magereza mpaka kesho saa 3 asubuhi.

Jaji anatoka

Sheria zetu ni za kikoloni. Katika nchi zilizoendelea, recanting (retracting a statement by a defendant) au hata withdrawing a guilty plea sio big deal. Prosecutors wanapaswa kuwa na uwezo wa kuthibitisha mashitaka yao dhidi ya defendant hata bila confession ya defendant. Faida pekee ya defendant’s confession ni kuokoa muda wa mahakama na wa pande zote zinazohusika.

All in all, mawakili wanaounda jopo la defense wanapoteza muda mwingi kwenye POs ambazo zina zero-chance ya kufanikiwa (au hata zikifanikiwa, zina impact kiduchu sana kwenye kesi ya msingi). That’s nonsense. Wanapaswa watumie muda mwingi kunoa mikakati yao ya utetezi katika kesi ya msingi!
 
Sheria zetu ni za kikoloni. Katika nchi zilizoendelea, recanting (retracting a statement by a defendant) au hata withdrawing a guilty plea sio big deal. Prosecutors wanapaswa kuwa na uwezo wa kuthibitisha mashitaka yao dhidi ya defendant hata bila confession ya defendant. Faida pekee ya defendant’s confession ni kuokoa muda wa mahakama na wa pande zote zinazohusika.

All in all, mawakili wanaounda jopo la defense wanapoteza muda mwingi kwenye POs ambazo zina zero-chance ya kufanikiwa (au hata zikifanikiwa, zina impact kiduchu sana kwenye kesi ya msingi). That’s nonsense. Wanapaswa watumie muda mwingi kunoa mikakati yao ya utetezi katika kesi ya msingi!
Si ndio hivyo wanavyonoa?

Amandla...
 
..haya maamuzi ni MABAYA sana kwa upande wa washtakiwa.

..mimi sio mwanasheria, lakini ktk kusoma maamuzi ya leo, naona kama Jaji ameamua kwamba washtakiwa wana HATIA.

..hisia zangu ni kwamba, maamuzi ya mwisho ktk kesi hii yatafanana zaidi na maamuzi yaliyotolewa leo.

CC Nguruvi3
Mkuu Tuliambiwa 'Wenzie Mbowe'' wanatumikia kifungo tayari
Tuliambiwa 'mtuhumiwa' alikimbia huku rejea zikionyesha akiwa nchini
Tukasikia Jaji anatoa maoni na si kwa mujibu wa sheria . '' kwa maoni yangu'
Mahakama ilipowasihi waendesha mashata wakaweke uzuri mashataka yao
Jaji kiongozi akiapishwa '' kwamba hukumu zizingatie hali ya nchi '!

Kesi ya Mbowe pamoja na wengi kusema inatia doa Taifa na nchi kwa ujumla , kwa upande mwingine imesaidia sana na pengine kupitia kesi hii kuna kudhihiri kwa baadhi ya mambo

1. Kwamba, wasiojulikana wapo na wengine wamejulikana na haijulikani kwanini hawajulikani
2. Imetoa ushuhuda kwanini ilikuwa kupoteza muda kupeleka kesi za uchaguzi
3. Imeondoa shaka kuhusu 'Mhimili uliojichimbia chini zaidi' na hii mingine ikielea na kupepesuka

Kesi imeonyesha nafasi ya mahakama katika jamii na imeacha maswali mengi sana ikiwa kuna mahali mbadala pa kupata haki.

Imeonyesha matundu katika mhimili wa haki kuliko wakati mwingine wowote ule wa uhai wa Taifa.

Maana yake ni moja, haki isipopatikana mahakamani itapatikana wapi?

Wanaodhani tuna tatizo la Tume ya uchaguzi wafikirie tena.

Tatizo ni kubwa sana, kesi ya Mbowe iwafungue macho.
Mifumo ya Taasisi zetu haifanyi kazi kama ilivyotarajiwa.

Wanasaikolojia wanasema ukitaka kumshinda mpinzani wako kwanza mfanye dhalili ili kumuondolea ''confidence'' halafu mkabili. Mkuu unakumbuka ''probation' ?

Hakuna njia ya mkato, katiba mpya itakayojenga mifumo imara ya taasisi zetu ni jibu

Hii kesi iendelee inafunua macho , nadhani ni moja ya vitu muhimu sana vinavyolizindua Taifa
 
yaani Tanzania ni nchi ya amani sana. imagine, kesi ni ya upinzani, lakini wazungu ambao siku zote wamelalia upande wa upinzani, wanahudhuria kesi bila shida. sasa wewe nenda nchi za watu, kaonyeshe brassiness upande mmoja uone kama utakubaliwa na nchi hiyo. wajerumani na wazungu wengine wote wameonyesha kulalia upande mmoja bila hata aibu, hata kwa mambo ambayo yana ushahidi. hao mawakili wa serikali wanafanya kazi ngumu kwasababu wanashindana sio tu na mawakili wa mbowe, wanashindana na nchi za EU zote pia. na wanawashinda.
 
yaani Tanzania ni nchi ya amani sana. imagine, kesi ni ya upinzani, lakini wazungu ambao siku zote wamelalia upande wa upinzani, wanahudhuria kesi bila shida. sasa wewe nenda nchi za watu, kaonyeshe brassiness upande mmoja uone kama utakubaliwa na nchi hiyo. wajerumani na wazungu wengine wote wameonyesha kulalia upande mmoja bila hata aibu, hata kwa mambo ambayo yana ushahidi. hao mawakili wa serikali wanafanya kazi ngumu kwasababu wanashindana sio tu na mawakili wa mbowe, wanashindana na nchi za EU zote pia. na wanawashinda.

..Ujerumani wametupa fedha kuboresha mifumo yetu ya sheria. Pia wamekuwa wafadhili wakubwa wa kitivo cha sheria Udsm. Kwa hiyo lazima wafuatilie kinachoendelea.
 
Mkuu Tuliambiwa 'Wenzie Mbowe'' wanatumikia kifungo tayari
Tuliambiwa 'mtuhumiwa' alikimbia huku rejea zikionyesha akiwa nchini
Tukasikia Jaji anatoa maoni na si kwa mujibu wa sheria . '' kwa maoni yangu'
Mahakama ilipowasihi waendesha mashata wakaweke uzuri mashataka yao
Jaji kiongozi akiapishwa '' kwamba hukumu zizingatie hali ya nchi '!

Kesi ya Mbowe pamoja na wengi kusema inatia doa Taifa na nchi kwa ujumla , kwa upande mwingine imesaidia sana na pengine kupitia kesi hii kuna kudhihiri kwa baadhi ya mambo

1. Kwamba, wasiojulikana wapo na wengine wamejulikana na haijulikani kwanini hawajulikani
2. Imetoa ushuhuda kwanini ilikuwa kupoteza muda kupeleka kesi za uchaguzi
3. Imeondoa shaka kuhusu 'Mhimili uliojichimbia chini zaidi' na hii mingine ikielea na kupepesuka

Kesi imeonyesha nafasi ya mahakama katika jamii na imeacha maswali mengi sana ikiwa kuna mahali mbadala pa kupata haki.

Imeonyesha matundu katika mhimili wa haki kuliko wakati mwingine wowote ule wa uhai wa Taifa.

Maana yake ni moja, haki isipopatikana mahakamani itapatikana wapi?

Wanaodhani tuna tatizo la Tume ya uchaguzi wafikirie tena.

Tatizo ni kubwa sana, kesi ya Mbowe iwafungue macho.
Mifumo ya Taasisi zetu haifanyi kazi kama ilivyotarajiwa.

Wanasaikolojia wanasema ukitaka kumshinda mpinzani wako kwanza mfanye dhalili ili kumuondolea ''confidence'' halafu mkabili. Mkuu unakumbuka ''probation' ?

Hakuna njia ya mkato, katiba mpya itakayojenga mifumo imara ya taasisi zetu ni jibu

Hii kesi iendelee inafunua macho , nadhani ni moja ya vitu muhimu sana vinavyolizindua Taifa

Watu mna obsession na katiba mpya utadhani katiba mpya itakuwa na uwezo wa kujilinda yenyewe. Kama haki zilizomo kwenye katiba ya sasa hatuwezi kuzisimamia, kuna sababu gani ya kuamini kuwa tutaweza kuisimamia katiba mpya? FYI, zipo nchi zingine zilizoandika upya katiba zao, lakini shida zao zimebaki palepale!
 
yaani Tanzania ni nchi ya amani sana. imagine, kesi ni ya upinzani, lakini wazungu ambao siku zote wamelalia upande wa upinzani, wanahudhuria kesi bila shida. sasa wewe nenda nchi za watu, kaonyeshe brassiness upande mmoja uone kama utakubaliwa na nchi hiyo. wajerumani na wazungu wengine wote wameonyesha kulalia upande mmoja bila hata aibu, hata kwa mambo ambayo yana ushahidi. hao mawakili wa serikali wanafanya kazi ngumu kwasababu wanashindana sio tu na mawakili wa mbowe, wanashindana na nchi za EU zote pia. na wanawashinda.

You’re right, hiyo sio kazi ya diplomatic missions. Ni interference ya wazi kwenye internal affairs za host country!
 
yaani Tanzania ni nchi ya amani sana. imagine, kesi ni ya upinzani, lakini wazungu ambao siku zote wamelalia upande wa upinzani, wanahudhuria kesi bila shida. sasa wewe nenda nchi za watu, kaonyeshe brassiness upande mmoja uone kama utakubaliwa na nchi hiyo. wajerumani na wazungu wengine wote wameonyesha kulalia upande mmoja bila hata aibu, hata kwa mambo ambayo yana ushahidi. hao mawakili wa serikali wanafanya kazi ngumu kwasababu wanashindana sio tu na mawakili wa mbowe, wanashindana na nchi za EU zote pia. na wanawashinda.
Tanzania sio nchi ya amani..ni nchi ya watu waoga.tunaojiridhisha uoga wetu kwa kujificha kwenye kivuli cha amani..if you are in your right senses haya yote yanayoendelea kwa ujumla wake yanaonyesha ni watu waoga waliopumbazwa na siasa za ujamaa..kumbuka amani hupewi bali unaitafuta na haiji hadi kwa ncha ya upanga..amani huja baada ya kuushinda uoga.
 
Watu mna obsession na katiba mpya utadhani katiba mpya itakuwa na uwezo wa kujilinda yenyewe. Kama haki zilizomo kwenye katiba ya sasa hatuwezi kuzisimamia, kuna sababu gani ya kuamini kuwa tutaweza kuisimamia katiba mpya? FYI, zipo nchi zingine zilizoandika upya katiba zao, lakini shida zao zimebaki palepale!
Kwanza, nitajibu hoja zako kwa kuanzia na hii ya katiba iliyopo ya 1977.

Haki ndani ya katiba ya sasa haziwezi kusimamiwa ni hoja mfu potofu inayotumiwa na watu wasioweza kutazama mambo kwa upana wake.Ni hoja primitive na silaha rahisi kwa 'ignorant'

Katiba ya sasa ni sawa na mgonjwa aliyepo ''ICU'' kwamba mgonjwa hajiwezi wala kujitambua bado unamatumaini anaweza kwenda uani, kujiwekea Oxygen na hata kukusaidia wewe ulikwenda kumsalimu.

Nyerere alisema '' katiba inampa madaraka ya kuwa Dikteta''. Kwa bahati nzuri uadilifu na maadili ya viongozi waliomfuata yaliitetetea katiba. Miaka 5 iliyopita tumethibitisha alichosema Nyerere ni kweli. Katiba haikuweza kujitetea nani angeweza kuitumia kujitetea

Katiba Mpya si suluhisho la matatizo lakini ni hatua muhimu sana. Hakuna katiba iliyokamili duniani lakini zipo zilizo na hali nzuri. Kenya ya leo ni tofauti na sisi kwa haki na uwajibikaji

Kenya CJ anagombea hateuliwi na hafungwi na mtu. Yupo huru kutetea masilahi ya Umma

Majaji wana muda ili kuondoa conflict of interest. Kwamba hawategemewi kuwa katika bodi au taasisi nyingine na hilo linawaweka huru. Fuatilia yanayotokea Kenya

Katiba mpya si kwa ajili ya uchaguzi au tume, bali kurekebisha mifumo dhaifu iliyotakiwa kujisimamia na kusimamia umma zikiwemo taasisi kama Bunge na Mahakama

Vyombo kama DPP, DCI Takukuru ni vya umma kwa ajili ya Umma

Unakumbuka CAG na T 1.5? Kaondolewa na hakuna kilichotokea.
Takukuru ipo Ofisi ya Rais kisheria kabisa. Hadi leo ni malumbano ya T 1.5

Unakumbuka kesi ya Wakurugenzi kuwa wasimamizi wa chaguzi?

Mahakama ikaamua wasimamizi wanaapishwa na hivyo wanatenda haki. Think about that!

kwamba Mahakama ya Tanzania inaamini Mtanzania akila kiapo huyo ni muadilifu kabisa!!!
Hakuna Waziri au katibu mkuu au Mkurugenzi anayefanya ''uhalifu'', wameapa!

Bungeni kuna watu 19 wanalipwa pesa za umma. Ni kupitia mamlaka ya katiba, ipo sheria ya viongozi kutoshtakiwa kwa makosa akiwemo Rais, Waziri mkuu na Spika.
Katika mazingira haya nini unategemea katiba ya 1977 inaweza kufanya tofauti?

Hoja ni nyingi muhimu ni kuelewa katiba mpya inalenga kupunguza uozo iliyopo si kwamba ni mbovu bali ipo taabani.

Kinachoendelea mahakamani ni jambo la heri la kuwafumbua macho Watanzania.
Kuna mengi hawakujua lakini leo wanayaona na hili la kesi ya Mbowe ni jema

Kudhani ni kesi ya Mbowe ni kujidanganya! Yanayoendelea yatamkuta yoyote yule.


JokaKuu Alinda
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom