Mahakama yatupilia mbali Kesi ya Mbowe ya Kikatiba dhidi ya IGP, DPP na Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Toka kizazi cha majaji tajika kama Jaji Lugakingira,Jaji Kati,Jaji Mapigano,Jaji Mwalusanya,Jaji Chipeta na wengine wa aina hiyo waliokuwa real bold spirted judges,kwa sasa tuna kizazi cha majaji wasiojielewa na wasiomjua nguvu waliyonayo katika kusimamia Uhuru wa muhimili wa mahakama katika kutenda haki. Inasikitisha.
Akhsante mkuu@Kamugumya kwa kumuorodhesha mzee wangu kuwa mmojawapo ya majaji bora watenda haki kuwahi kutokea.
Mungu akubariki.
 
kwahiyo mwawakili wa serikali wamewashinda mawakili wasomi na hoja zao zenye nguvu na mashiko? kwanza hao mawakili wasomi wamewahi fanikisha kushinda kesi ipi ya ugaidi na uhujumu uchumi mbona wamekuzwa sana tofauti na uhalisia.
 
Sijawahi kusifia hizo mahakama za ccm. Sabaya hata asingepelekwa mahakamani, bado haiondoi ukweli kuwa alikuwa ni agent wa kutekeleza maovu ya yule kiongozi dhalimu aliyeko motoni muda huu.
Dhalimu kwa mujibu wa nani?

Motoni kwa mujibu wa nani?

Unafikri huo moto ni wa Lisu na Amsterdam?
 
Nani alisema mahakama iko vizuri? Hiyo mahakama ndio iliagizwa aina ya hukumu ya kutoa. Usidhani hatujui ni kipi kilikuwa kinaongelewa.
Mkuu umeshawachangia mawakili wetu kupitia miamala?
 
Kumbe mahakama haijakataa hoja za Mbowe ila imeelekeza kwamba, kwa kuwa kesi ya msingi iko mahakama kuu, kitengo cha Uhujumu uchumi, basi huko ndiko mahali sahihi kupeleka madai yake...

On the other hand, kama Jaji angekubaliana na hoja za mleta pingamizi (ambazo obviously ziko sahihi), maana yake alikuwa anaifuta kabisa kesi ya Msingi iliyoko mahakama kuu kitengo cha makosa ya uhujumu uchumi...!

Ndiyo maana, Jamhuri wiki hii yote imesimama kuendelea na usikilizaji wa shauri hili ili kupima na kujadiliana namna ya kulimaliza pingamizi hilo...
Utayasikia machadema yakimsifu kibatala kama hayana akili wakati maji yamemfika shingoni. Wanaogopa kesi ya msingi hadi wanajamba na kuharisha kwa sababu uko ushahidi wa kutosha mbowe kufanya ugaidi. Eti laki sita inaweza fanya ugaidi? Wanauliza.. kinachoangaliwa ni nia. Kwani laki sita haitoshi kulipua kituo cha mafuta?
Uliberali wanaopigania leo hakuna 🙄. Eti ukionyesha kuna kosa kwenye kukamatwa basi jaji anakuachia kesi ya msingi!! 🚶🚶🚶
 
Dhalimu kwa mujibu wa matendo yake. Motoni kwa mujibu biblia kuhusu watu waovu. Huo moto sifikiri ni wa Amsterdam na Lisu, bali ni wa Mungu.
limu kwa mujibu wa nani?

Motoni kwa mujibu wa nani?

Unafikri huo moto ni wa Lisu na Amsterdam?
 
Akili za mawakili wa Mbowe kama za BAVICHA!

Kulalamika kwingi, vipingamizi Vingi, maneno mengi, LAKINI hayana msingi, yanakosa logic, yanajikita kwenye vitu vidovidogo na kushindwa kuaddress core issues!
Kweli kabisa bwa sheeee
 
Leo Sept. 23, 2021 saa nane kamili mchana, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam itatoa uamuzi mdogo juu ya mapingamizi ya Serikali katika Kesi ya Kikatiba namba 21/2021 iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Chasema Freeman Mbowe dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, DPP na IGP.

Wakati anakabiliwa na Kesi ya Ugaidi, Mbowe alifungua kesi ya kikatiba Mahakama Kuu dhidi ya Serikali akipinga taratibu za kukamatwa na kushtakiwa kwake.

Miongoni mwa madai yake, Mbowe anapinga kushtakiwa kwa makosa ya ugaidi kimyakimya bila kumtaarifu kwanza kuhusu mashtaka hayo pamoja na maneno ya vitisho anayodai kupewa na polisi kabla ya mashtaka hayo.

Vilevile mwanasiasa huyo anelalamikiwa haki zake kukiukwa kwa ndugu na wakili wake kutokujulishwa na kupewa fursa ya kuwasilishwa.

Mbowe anadai wakati ameshikiliwa katika kituo cha Polisi Oysterbay alikuwa akipokea kauli za kejeli na vitisho kutoka kwa ofisa wa polisi.

Pamoja na mambo mengine, Mbowe katika hati ya kiapo chake kinachounga mkono madai yake anazitaja kauli hizo anazodai kuwa zilitolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni (RPC), aliyemtaja kwa jina Ramadhani Kingai kuwa:

“Wewe si unajifanya unaijua Katiba Mpya, safari hii huchomoki, tunakupiga kesi ya ugaidi”, inasomeka sehemu ya hati ya kiapo hicho cha Mbowe.

Mbowe alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Julai 26, 2021 na kusomewa mashtaka ya ugaidi kimyakimya katika kesi aliyoungianishwa na washtakiwa wengine waliokuwa wameshapandishwa kizimbani tangu mwaka 2020.

Alisomewa mashtaka hayo bila kuwepo mawakili, wanafamilia wala wanahabari kisha akapelewa rumande kwa kuwa mashtaka hayo hayana dhamana.

Kabla ya hatua hiyo Mbowe alishikiliwa na Jeshi la Polisi kwa siku tano tangu alipotiwa mbaroni Julai 21, 2021 usiku akiwa jijini Mwanza alikokwenda kwa maandalizi ya kongamano la kudai Katiba Mpya lililokuwa limeandaliwa na Baraza a Vijana wa Chadema (Bavicha).

Usiku huohuo alisafirishwa mpaka Dar es Salaam hadi nyumbani kwake ambako alifanyiwa upekuzi kisha akashikiliwa mahabusu ya Kituo cha Polisi Oysterbay hadi alipopandishwa kizimbani.

Wakati akiendelea na Kesi ya Ugaidi, Mbowe kupitia kwa wakili wake, Peter Kibatala alifungua kesi ya Kikatiba dhidi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) katika Mahakama Kuu, Masjala Kuu.

Katika kesi hiyo namba 21 ya mwaka 2021, Mbowe anadai kuwa mdaiwa wa kwanza (DPP) na wa pili (IGP) walikiuka haki zake za kikatiba kwa kumfungulia kesi nzito ya kikatiba bila kwanza kumtaarifu kwa maandishi na kumwezesha kuwasiliana na wakili wala ndugu zake.

Hivyo, anaiomba Mahakama Kuu itoe nafuu mbalimbali ambazo ni pamoja na masharti ya lazima ya vifungu namba 131 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) na Sheria ya Kudhibiti Uhalifu wa Kupanga na Uhujumu Uchumi, Sura ya 200.

Vifungu hivyo vinatoa sharti la lazima kwa ofisa wa polisi anayemshtaki mtuhumiwa na kwa mahakama ambako mtuhumiwa anashtakiwa kumjulisha mshtakiwa kwa maandishi kuwa atashtakiwa makosa husika, lakini pia vinampa fursa ya kuwasiliana na ndugu na wakili wake kuhusiana na mashtaka hayo.

Vilevile mahakama hiyo inaombwa itamke kuwa kifungu cha 29(1) cha sheria hiyo ya uhujumu uchumi kinachotoa sharti la lazima kwa ofisa wa polisi anayemshikilia mtuhumiwa mahabusu amfikishe katika Mahakama ya Wilaya au ya Hakimu Mkazi ndani ya saa 48, tangu kukamatwa kwake, kilikiukwa.

Mbowe pia anaiomba mahakama hiyo itamke kuwa DPP na AG walikiuka haki zake zinazotolewa na kulindwa chini ya masharti ya kifungu cha 29 (1) cha Sheria ya Uhujumu.

Anabainisha kuwa pamoja na mambo mengine, madai hayo yanalenge kuzuia matumizi mabaya ya madaraka dhidi ya mtuhumiwa katika Kituo cha Polisi ambako mtuhumiwa anakuwa amewekwa mahabusu baada ya kutiwa mbaroni.

Anadai kuwa alipokuwa akishikiliwa mahabusu aliwekwa katika mazingira yasiyofaa, ikiwemo kulala sakafuni (bila matandiko yoyote) kuanzia Julai 21 alipokamatwa jijini Mwanza mpaka Julai 26, 2021 alipopandishwa kizimbani.

Mbowe pia anaiomba mahakama itamke kuwa DPP na IGP pamoja na Mahakama ya Kisutu, ikitenda kwa amri ya DPP na AG, walikiuka haki zake zinazolindwa na masharti kifungu cha 29 (2) na (3) cha sheria ya uhujumu uchumi kwa kushindwa kumjulisha kwa maandishi kwamba atashtakiwa kwa mashtaka mazito chini ya Sheria ya Kuzuia Ugaidi na Sheria ya Uhujumu Uchumi.

Zaidi soma:

Thread 'Serikali yamwekea pingamizi Mbowe kesi aliyofungua dhidi ya DPP, AG na IGP' Serikali yamwekea pingamizi Mbowe kesi aliyofungua dhidi ya DPP, AG na IGP

=======

UPDATES;1715HRS

========

Dar es Salaam. Mahakama Kuu ya Tanzania imetupilia mbali kesi ya kikatiba ya mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, aliyekuwa akipinga namna alivyowekwa kizuizini na kulazwa sakafuni kwa siku tano bila kufikishwa mahakamani.

Mbowe alifungua kesi hiyo Julai 30, mwaka huu akilalamikia namna alivyotiwa mbaroni jijini Mwanza kuweka mahabusu ya polisi kwa siku tano bila kufikishwa mahakamani ndani ya saa 48 kama sheria inavyoelekeza.

Kiongozi huyo wa chama kikuu cha upinzania pia alikuwa akilalamika kiulazwa sakafuni bila matandiko uyoyote wakati akiwa mahabusu.

Katika kesi hiyo namba 21 ya 2021, Mbowe alikuwa akipinga kufikishwa mahakamani bila kuwajulisha mawakili wake au ndugu zake na kabla ya kujulishwa kwa maandishi kuhsu mashtaka yaliyokuwa yakimkabili.

Katika kesi hiyo aliyoifungua dhidi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Mbowe alikuwa pia akipinga kusomewa mashtaka ya ugaidi yanayomkabilia bila kuwa na wakili wala kupewa hati ya mashtaka.

Mbowe alikuwa akidai utaratibu huo ulikiuka haki zake za kikatiba, huku akiiomba mahakama hiyo itamke kuwa haki zake zilikiukwa.

Uamuzi wa kuitupa kesi hiyo umetolewa leo Alhamisi Septemba 23 na Jaji John Mgetta aliyesikikiza pingamizi hilo la Serikali kwa niaba ya jopo la majaji watatu waliokua wamepangwa kusikiliza kesi hiyo, akiwemo Jaji Leila Mgonya na Jaji Stephen Magoiga.

Majaji hao wamekubaliana na pingamizi la Serikali lililokuwa na hoja nne lililotaka kesi hiyo isisikilizwe kwa madai ya kuwa na kasoro nyingi za kisheria.

Mahakama Kuu imekataa hoja tatu za pingamizi la Serikali na kubaliana na hoja moja tu ya pingamizi la Serikali iliyodai kuwa Mbowe hakutumia njia nyingine zilizopo kutafuta haki anazodai kabla ya kufungua kesi ya kikatiba.

Mahakama imekubaliana na Serikali kupitia jopo la mawakili wa Serikali lililoongozwa na Wakili wa Serikali Hangi Chang'a kuwa kwa kuwa kuna kesi ya jinai dhidi yake (Mbowe), basi madai yake alipaswa kuyaibua katika Mahakama hiyo kwanza kabla ya kufungua kesi ya kikatiba.

"Kwa hiyo nakubaliana na pingamizi hili la wajibu maombi kwamba hii ni hoja ya kisheria na kama alivyoeleza Wakili Mkuu wa Serikali, Mussa Mbura katika hoja za maandishi, Mahakama inayosikilizwa kesi yake (Mbowe) ya uhujumu uchumi ndiyo mahakama sahihi. Hivyo alipaswa kutoa madai yake huko kwanza," amesema Jaji Mgetta.

Chanzo: Mwananchi online

Katika uendeshaji nchi ambako kuna mhimili uliojichimbia zaidi hatuna cha kujivunia kutokea mahakamani kiwe +ve au -ve.

Majaji ni wateuliwa wa ule mhimili na wakapewa bakshish za kutokulipa kodi kama wale vigogo bila kuyasahau maelekezo kutoka juu.

Hadi tutakapokuwa na katiba mpya, mahakamani tunakwenda kuwaumbua tu kama alichofanya Adamoo au yaliyowakuta Kingai au yule bwana Mahita.

Iko wazi kuwa hata Hangaya anajua Mbowe si gaidi.
 
Back
Top Bottom