Mahakama yatupilia mbali Kesi ya Mbowe ya Kikatiba dhidi ya IGP, DPP na Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,189
4,103
Leo Sept. 23, 2021 saa nane kamili mchana, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam itatoa uamuzi mdogo juu ya mapingamizi ya Serikali katika Kesi ya Kikatiba namba 21/2021 iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Chasema Freeman Mbowe dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, DPP na IGP.

Wakati anakabiliwa na Kesi ya Ugaidi, Mbowe alifungua kesi ya kikatiba Mahakama Kuu dhidi ya Serikali akipinga taratibu za kukamatwa na kushtakiwa kwake.

Miongoni mwa madai yake, Mbowe anapinga kushtakiwa kwa makosa ya ugaidi kimyakimya bila kumtaarifu kwanza kuhusu mashtaka hayo pamoja na maneno ya vitisho anayodai kupewa na polisi kabla ya mashtaka hayo.

Vilevile mwanasiasa huyo anelalamikiwa haki zake kukiukwa kwa ndugu na wakili wake kutokujulishwa na kupewa fursa ya kuwasilishwa.

Mbowe anadai wakati ameshikiliwa katika kituo cha Polisi Oysterbay alikuwa akipokea kauli za kejeli na vitisho kutoka kwa ofisa wa polisi.

Pamoja na mambo mengine, Mbowe katika hati ya kiapo chake kinachounga mkono madai yake anazitaja kauli hizo anazodai kuwa zilitolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni (RPC), aliyemtaja kwa jina Ramadhani Kingai kuwa:

“Wewe si unajifanya unaijua Katiba Mpya, safari hii huchomoki, tunakupiga kesi ya ugaidi”, inasomeka sehemu ya hati ya kiapo hicho cha Mbowe.

Mbowe alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Julai 26, 2021 na kusomewa mashtaka ya ugaidi kimyakimya katika kesi aliyoungianishwa na washtakiwa wengine waliokuwa wameshapandishwa kizimbani tangu mwaka 2020.

Alisomewa mashtaka hayo bila kuwepo mawakili, wanafamilia wala wanahabari kisha akapelewa rumande kwa kuwa mashtaka hayo hayana dhamana.

Kabla ya hatua hiyo Mbowe alishikiliwa na Jeshi la Polisi kwa siku tano tangu alipotiwa mbaroni Julai 21, 2021 usiku akiwa jijini Mwanza alikokwenda kwa maandalizi ya kongamano la kudai Katiba Mpya lililokuwa limeandaliwa na Baraza a Vijana wa Chadema (Bavicha).

Usiku huohuo alisafirishwa mpaka Dar es Salaam hadi nyumbani kwake ambako alifanyiwa upekuzi kisha akashikiliwa mahabusu ya Kituo cha Polisi Oysterbay hadi alipopandishwa kizimbani.

Wakati akiendelea na Kesi ya Ugaidi, Mbowe kupitia kwa wakili wake, Peter Kibatala alifungua kesi ya Kikatiba dhidi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) katika Mahakama Kuu, Masjala Kuu.

Katika kesi hiyo namba 21 ya mwaka 2021, Mbowe anadai kuwa mdaiwa wa kwanza (DPP) na wa pili (IGP) walikiuka haki zake za kikatiba kwa kumfungulia kesi nzito ya kikatiba bila kwanza kumtaarifu kwa maandishi na kumwezesha kuwasiliana na wakili wala ndugu zake.

Hivyo, anaiomba Mahakama Kuu itoe nafuu mbalimbali ambazo ni pamoja na masharti ya lazima ya vifungu namba 131 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) na Sheria ya Kudhibiti Uhalifu wa Kupanga na Uhujumu Uchumi, Sura ya 200.

Vifungu hivyo vinatoa sharti la lazima kwa ofisa wa polisi anayemshtaki mtuhumiwa na kwa mahakama ambako mtuhumiwa anashtakiwa kumjulisha mshtakiwa kwa maandishi kuwa atashtakiwa makosa husika, lakini pia vinampa fursa ya kuwasiliana na ndugu na wakili wake kuhusiana na mashtaka hayo.

Vilevile mahakama hiyo inaombwa itamke kuwa kifungu cha 29(1) cha sheria hiyo ya uhujumu uchumi kinachotoa sharti la lazima kwa ofisa wa polisi anayemshikilia mtuhumiwa mahabusu amfikishe katika Mahakama ya Wilaya au ya Hakimu Mkazi ndani ya saa 48, tangu kukamatwa kwake, kilikiukwa.

Mbowe pia anaiomba mahakama hiyo itamke kuwa DPP na AG walikiuka haki zake zinazotolewa na kulindwa chini ya masharti ya kifungu cha 29 (1) cha Sheria ya Uhujumu.

Anabainisha kuwa pamoja na mambo mengine, madai hayo yanalenge kuzuia matumizi mabaya ya madaraka dhidi ya mtuhumiwa katika Kituo cha Polisi ambako mtuhumiwa anakuwa amewekwa mahabusu baada ya kutiwa mbaroni.

Anadai kuwa alipokuwa akishikiliwa mahabusu aliwekwa katika mazingira yasiyofaa, ikiwemo kulala sakafuni (bila matandiko yoyote) kuanzia Julai 21 alipokamatwa jijini Mwanza mpaka Julai 26, 2021 alipopandishwa kizimbani.

Mbowe pia anaiomba mahakama itamke kuwa DPP na IGP pamoja na Mahakama ya Kisutu, ikitenda kwa amri ya DPP na AG, walikiuka haki zake zinazolindwa na masharti kifungu cha 29 (2) na (3) cha sheria ya uhujumu uchumi kwa kushindwa kumjulisha kwa maandishi kwamba atashtakiwa kwa mashtaka mazito chini ya Sheria ya Kuzuia Ugaidi na Sheria ya Uhujumu Uchumi.

Zaidi soma:

Thread 'Serikali yamwekea pingamizi Mbowe kesi aliyofungua dhidi ya DPP, AG na IGP' Serikali yamwekea pingamizi Mbowe kesi aliyofungua dhidi ya DPP, AG na IGP

=======

UPDATES;1715HRS

========

Dar es Salaam. Mahakama Kuu ya Tanzania imetupilia mbali kesi ya kikatiba ya mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, aliyekuwa akipinga namna alivyowekwa kizuizini na kulazwa sakafuni kwa siku tano bila kufikishwa mahakamani.

Mbowe alifungua kesi hiyo Julai 30, mwaka huu akilalamikia namna alivyotiwa mbaroni jijini Mwanza kuweka mahabusu ya polisi kwa siku tano bila kufikishwa mahakamani ndani ya saa 48 kama sheria inavyoelekeza.

Kiongozi huyo wa chama kikuu cha upinzania pia alikuwa akilalamika kiulazwa sakafuni bila matandiko uyoyote wakati akiwa mahabusu.

Katika kesi hiyo namba 21 ya 2021, Mbowe alikuwa akipinga kufikishwa mahakamani bila kuwajulisha mawakili wake au ndugu zake na kabla ya kujulishwa kwa maandishi kuhsu mashtaka yaliyokuwa yakimkabili.

Katika kesi hiyo aliyoifungua dhidi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Mbowe alikuwa pia akipinga kusomewa mashtaka ya ugaidi yanayomkabilia bila kuwa na wakili wala kupewa hati ya mashtaka.

Mbowe alikuwa akidai utaratibu huo ulikiuka haki zake za kikatiba, huku akiiomba mahakama hiyo itamke kuwa haki zake zilikiukwa.

Uamuzi wa kuitupa kesi hiyo umetolewa leo Alhamisi Septemba 23 na Jaji John Mgetta aliyesikikiza pingamizi hilo la Serikali kwa niaba ya jopo la majaji watatu waliokua wamepangwa kusikiliza kesi hiyo, akiwemo Jaji Leila Mgonya na Jaji Stephen Magoiga.

Majaji hao wamekubaliana na pingamizi la Serikali lililokuwa na hoja nne lililotaka kesi hiyo isisikilizwe kwa madai ya kuwa na kasoro nyingi za kisheria.

Mahakama Kuu imekataa hoja tatu za pingamizi la Serikali na kubaliana na hoja moja tu ya pingamizi la Serikali iliyodai kuwa Mbowe hakutumia njia nyingine zilizopo kutafuta haki anazodai kabla ya kufungua kesi ya kikatiba.

Mahakama imekubaliana na Serikali kupitia jopo la mawakili wa Serikali lililoongozwa na Wakili wa Serikali Hangi Chang'a kuwa kwa kuwa kuna kesi ya jinai dhidi yake (Mbowe), basi madai yake alipaswa kuyaibua katika Mahakama hiyo kwanza kabla ya kufungua kesi ya kikatiba.

"Kwa hiyo nakubaliana na pingamizi hili la wajibu maombi kwamba hii ni hoja ya kisheria na kama alivyoeleza Wakili Mkuu wa Serikali, Mussa Mbura katika hoja za maandishi, Mahakama inayosikilizwa kesi yake (Mbowe) ya uhujumu uchumi ndiyo mahakama sahihi. Hivyo alipaswa kutoa madai yake huko kwanza," amesema Jaji Mgetta.

Chanzo: Mwananchi online
 
La muhimu ni kujua ni vipi maamuzi hayo yataathiri kesi inayoendelea mahakama ya uhujumu uchumi na ugaidi.
 
La muhimu ni kujua ni vipi maamuzi hayo yataathiri kesi inayoendelea mahakama ya uhujumu uchumi na ugaidi.
Hakuna Mahakama ya Uhujumu Uchumi na Ugaidi katika Mfumo wa Mahaka ya Tanzania. Bali kuna Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uchumi, High Court, Division of Corruption and Economic Crimes
 
Hakuna Mahakama ya Uhujumu Uchumi na Ugaidi katika Mfumo wa Mahaka ya Tanzania. Bali kuna Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uchumi, High Court, Division of Corruption and Economic Crimes
Asante kwa masahihisho. Kwa kweli nilikuwa silijui hilo
 
Muhimu sana kuwa na uhuru kamili na demokrasia. Kujaribu kuminya uhuru na demokrasia kupitia sheria kandamizi haihalalilishi dhulma na ukandamizwaji. Dunia inaona na kuelewa hilo
 
Updates
Nini tafsiri ya Hukumu Hii ya Kutupiliwa mbali kesi hii kwa sababu za " Kiufundi / Kitaaluma". Je aliyefungua kesi wanahaki ila kuna masuala ya kiufundi ndiyo yanakwamisha?

ALICHOKISEMA WAKILI KIBATALA BAADA YA MAHAKAMA KUKATAA MAOMBI YA MBOWE LEO
Source : watetezi tv


.................................................................

Hapo awali asubuhi 23 Sept.2021


Hapa ni pia zile kanuni za PGO zitaangaziwa

Soma hapa PGO (kanuni za utendaji wa polisi) Tanzania | Swahili Times

3 days ago — Police General Orders (PGO) ni nini? Ni kanuni za mwongozo wa utendaji kazi wa Jeshi na Polisi. Ofisa yeyote wa polisi anapotekeleza....


Pia wiki 3 zilizopita kesi hii ya pingamizi tarehe 30 August 2021

KESI YA MBOWE DHIDI YA DPP, IGP NA MWANASHERIA MKUU YATAJWA MAHAKAMA KUU
 
Muhimu sana kuwa na uhuru kamili na demokrasia. Kujaribu kuminya uhuru na demokrasia kupitia sheria kandamizi haihalalilishi dhulma na ukandamizwaji. Dunia inaona na kuelewa hilo
Dunia gani inayoona? inaona wapi na kwa kioo gani? Marekani au Uingereza au Afghanistan?

Endesheni siasa bila kutegemea vigeugeu Uingereza,Marekani,bara la Ulaya au mababa wa kambo, mabeberu kusaidia kuleta mabadiliko.
Tuna muda mrefu wa kusubiri mabadiliko hayo kabla mageuzi kufika Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mahakama Kuu Tanzania, leo, imeifuta kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Freeman Mbowe, kupinga utaratibu uliotumika kumkamata, kumuweka kizuizini na kumfungulia kesi ya ugaidi. Jaji John Mgetta, amesema Mbowe anaweza kupeleka malalamiko yake mahakama ya uhujumu uchumi. https://t.co/fLro42csiu
IMG_20210923_153020.jpg
 
Tusaidie sababu za kuifuta ili habari yako ikamilike. Vinginevyo imekaa kishabiki kuliko kihabari.
Mahakama Kuu Tanzania, leo, imeifuta kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Freeman Mbowe, kupinga utaratibu uliotumika kumkamata, kumuweka kizuizini na kumfungulia kesi ya ugaidi. Jaji John Mgetta, amesema Mbowe anaweza kupeleka malalamiko yake mahakama ya uhujumu uchumi. https://t.co/fLro42csiu
View attachment 1949601
 
Back
Top Bottom