Mahakama yatupilia mbali kesi ya Dk. Mahanga dhidi ya Msemakweli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahakama yatupilia mbali kesi ya Dk. Mahanga dhidi ya Msemakweli

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Bujibuji, Oct 16, 2012.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Oct 16, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,157
  Trophy Points: 280
  Mahakama ya Wilaya ya Ilala, imefuta kesi ya madai iliyofunguliwa na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga, dhidi ya mwandishi wa kitabu cha ‘Orodha ya Mafisadi wa Elimu’, Kainerugaba Msemakweli.

  Katika kesi hiyo, Dk. Mahanga ambaye pia ni Mbunge wa Segerea (CCM), alikuwa akiiomba mahakama imwamuru Msemakweli amlipe fidia ya Sh. bilioni tatu kwa madai ya kumtaja katika kitabu hicho kuwamo kati ya mafisadi wa elimu.

  Kesi hiyo ilifutwa Septemba 17, mwaka huu, na Hakimu aliyekuwa akiisikiliza, Wilbaforce Luhwago.

  Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Joyce Minde, aliliambia NIPASHE ofisini kwake jana kuwa baada ya kesi hiyo kufutwa, limebaki jalada la gharama za kesi.

  Alisema shauri hilo litaenda mahakamani hapo Oktoba 31, mwaka huu, ili kuanza kusikilizwa, ambapo gharama za kesi zinazotakiwa kulipwa zitatajwa.

  Kesi hiyo ilihamishwa kwa Hakimu Luhwago baada ya Hakimu, ambaye awali ilikuwa mbele yake, Esther Mwakalinga, kujitoa kwa maelezo kwamba, ana maslahi na Dk. Mahanga, hivyo anahofia kutotenda haki.

  Kesi hiyo namba 25/2010 ilifunguliwa na Dk. Mahanga Machi 3, mwaka juzi.

  Msemakweli aliwahi kuiomba mahakama itupilie mbali kesi hiyo kwa madai kwamba, ilikuwa ikimpotezea muda wake kwa kuwa Dk. Mahanga kipindi hicho alikuwa hafiki mahakamani.

  Dk. Mahanga katika kesi hiyo alikuwa akitaka alipwa kiasi hicho cha fedha kwa madai kuwa katika toleo la kwanza la kitabu hicho, Msemakweli aliandika kwenye kurasa ya 11, 12, 13 na 14, na kumtaja kuwamo kati ya mafisadi wa elimu.

  Pia Dk. Mahanga, alikuwa anataka malipo hayo yasiwe chini ya Sh. milioni 500 pamoja na Sh. milioni 267 alizodai kuwa Msemakweli alijipatia baada ya kuuza nakala 89,000 za kitabu hicho.
   
 2. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280
  Kwahiyo kwa Lugha nyingine ni kwamba Mahakama imejiridhisha alichokisema Msemakweli ni kweli tupu.
   
 3. Scolari

  Scolari JF-Expert Member

  #3
  Oct 16, 2012
  Joined: Aug 4, 2008
  Messages: 273
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa hali hii Mahanga lazima aombe radhi taifa kwa kudanganya yeye ni DAKTARI.

  Wako wengi lakini sio yeye peke yake.
   
 4. S

  Sambwisi Senior Member

  #4
  Oct 16, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 166
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Tungeweza kupata nakala ya hukumu tutajua, sababu kama ni kwa Dk. Mahanga (Mdai) kutoenda mahakamani au vinginevyo. Kama ni kwa Mdai kutokwenda mahakamani hapo tujadili, ni kwa nini afungue kesi na asihudhurie mahakama? Mwishowe tunaweza kuamua alichoandika Msemakweli ni KWELI, KWELI TUPU!
   
Loading...