Sasa hivi CCM wanajua kuwa watu hawawataki, wanasoma magazeti, Jamii Forum na wanajua wakitoa mwanya tu wamekwisha na mwisho wao utakuwa mashakani hivyo tuna kazi ndugu zangu! Ila milango yote ikifungwa ni lazima kutatokea machafuko!!!God forbit.
[COLOR="#ffff00"]Tupate hukumu yenyewe kikamilifu; mimi sidhani kama majaji 7 wanaweza kutoa hukumu ya kijinga hivyo. Kuna conflict katika katiba maana upande mmoja inampa ,wananchi haki ya kuchaguliwa na upande mwingine inamnyang'anya haki hiyo kwa kumlazimisha kitu ambacho labda ni kinyume na matakwa yake (kujiunga na vyama vya siasa). Je conflict hiyo wameizungumziaje?[/COLOR]
Je wamesema mahakama kuu haikuwa na uwezo wa kusikiliza kesi inayohusu masuala ya katiba? na kama ni hivyo masuala hayo yapelekwe mahakama gani maana hatuna mahakama ya katiba! Huwezi kusema hayo yapelekwe bungeni maana uamuzi wa wabunge ndiyo ulileta conflict hiyo na hivyo mwananchi yeyote aliyekuwa -aggrived na maamuzi ya bunge hawezi tena kwenda bungeni- bali mahakamani.
Kuna ,mambo mengi yanayohitaji ufafanuzi katika hukumu hiyo.
Kama kweli mahakama imesema suala ni la kisiasa - je kesi ya kisiasa ipelekwe mahakama gani?
Ni hatari sana - watu wamepoteza imani na polisi, wamepoteza imani na mahakama hasa za chini na sasa wakipoteza imani na mahakama ya juu kabisa! itakuwa hatari zaidi ya kile mahakama ya rufaa ilichokiogopa - eti hakuna nchi inaongozwa na mtu huru/binafsi maana ni vizuri mtu binafsi akaingia kwa kupigiwa kura kuliko ukimzibia njia ya kura akaamua kuingia kwa njia ya mtutu! Tusijidanganye eti TZ hiyo haiwezekani, hata enzi za Obote hakuna aliyewazia hilo, enzi za Kenyatta na Moi hakuna akliwazia hilo - lakini yakatokea.!
Wagombea huru hata huko ilikoanzia hii democrasia tunayoiiga ni wachache sana tena kwenye ngazi ya UBUNGE tu. Sisi tunataka kuuparamia utaratibu huu kichwakichwa bila maandalizi yoyote, uelewa wa watu wetu bado mdogo. Mnataka kurudisha masultani, watemi na wafalme kwa mlango huu? Acheni hizo.
Tujipange vizuri kwanza kwenye mambo ya kuchagua na kuchaguliwa. Wagombea huru wabaki kwenye mambo ya uchumba tu kwanza. Hata kugombea uongozi YANGA ni lazima uwe MWANACHAMA!
Watawala wetu wakumbuke kitu kimoja kuwa hiyo ruling ya kupinga mgombea binafsi inaweza kuwa LEGAL but not LEGITEMATE!! Maana yake ni kwamba watu hawaikubali!!Si alishatamka waziri Marmo kwamba hakuna mgombea binafsi. CJ na jopo lake wamepiga mhuri tu amri ya waziri! LONG LIVE TANZANIA AND ITS POLITICS!!!!!!!
Wagombea huru hata huko ilikoanzia hii democrasia tunayoiiga ni wachache sana tena kwenye ngazi ya UBUNGE tu. Sisi tunataka kuuparamia utaratibu huu kichwakichwa bila maandalizi yoyote, uelewa wa watu wetu bado mdogo. Mnataka kurudisha masultani, watemi na wafalme kwa mlango huu? Acheni hizo.
Tujipange vizuri kwanza kwenye mambo ya kuchagua na kuchaguliwa. Wagombea huru wabaki kwenye mambo ya uchumba tu kwanza. Hata kugombea uongozi YANGA ni lazima uwe MWANACHAMA!
Unajua mwanakijiji, raha ya Tanzania ni kwamba Mahakama ni za serikali, jeshi la serikali, polisi wa serikali, bunge la serikali na hata katiba ni ya serikali. Majaji wote wameteuliwa na Rais, na Kikwete anajua wazi kwamba akisimama mgombea binafsi tu amekwisha. Unafikiri angekubali huo upuuzi wa mgombea binafsi? Atakuwa amewaagiza tu akina Augustino Ramadhani na washirika wake kwamba hii kesi iishie hapa.hakuna mahakama nyingine juu yake.. ndio uamuzi wa mwisho.. ila ningependa kupata details na reasoning yao. Inawezekana ameshinda kwenye hoja ya uwezo wa mahakama kutengua kipengele cha Katiba na siyo hoja ya wagombea binafsi au itarudishwa kesi mahakama Kuu.. kupitia tena.
Ebu niwaulizeni mnaotaka hii sheria ya mgombea binafsi...
Tuseme mathlan sheria hii ingepitishwa... Na wananchi elfu, laki au millioni uwezo wa kupiga kura wakiamua wao kujiandikisha kama wagombea Binafsi - itakuwaje?..
Maanake sheria mnayoitaka inaruhusu mgombea binafsi na sidhani kama kuna kiwango cha haki kwa idadi ya wagombea wala kukataza wengine wasifanye hivyo..Ni wapi kikomo wa hiyo haki ya mgombea binafsi kwa wananchi wake kwa sababu huwezi sema baadhi ya watu tu ndio wanaruhusiwa wengine wakae pembeni..Je, gharama zake pia zitachukuliwa na nani?..
Mzee Mwanakijiji,
Sijaisoma hukumu wala kuipata lakini kwa vyovyote vile issue itakuwa mahakama haiwezi kutengua kifungu cha katiba, bali inaweza kutengua sheria ambayo haiendani na katiba.
Unajua mwanakijiji, raha ya Tanzania ni kwamba Mahakama ni za serikali, jeshi la serikali, polisi wa serikali, bunge la serikali na hata katiba ni ya serikali. Majaji wote wameteuliwa na Rais, na Kikwete anajua wazi kwamba akisimama mgombea binafsi tu amekwisha. Unafikiri angekubali huo upuuzi wa mgombea binafsi? Atakuwa amewaagiza tu akina Augustino Ramadhani na washirika wake kwamba hii kesi iishie hapa.
Mgombea binafsi wa uraisi kwa sasa ni hatari zaidi. Atachunguzwa na nani kabla ya kuruhusiwa kugombea. Utambana vipi na kwa kanununi zipi? Kuna hatari kubwa ya mafisadi kujiunga na kuinunua nchi kwa bei poa na wakiipata hawahitaji zaidi ya kipindi kimoja kusaini mikataba mizito itayotufanya watumwa kwa miaka mingi. Kwa sasa tutaowapata ni vibaraka wa masultani na makabaila wakuu duniani ili wamilikishwe rasilimali zetu kwa kasi ya kutisha. Kama mwamkumbuka 'Jumanne' na kashfa ya OIC haiwi gumu kuelewa hili. Hata Nyerere aliwahi kueleza hofu yake juu ya mgombea binafsi asiye na chama. Ule msemo "Nionyeshe rafiki yako nitakuambia tabia yako" ndo unasaidia kuichambua tabia ya mgombea kwa kuzingatia tabia za chama kinachomfadhili.