Mahakama yatoa hati ya kumkamata Zacharia Hans Poppe, kuunganishwa kesi ya utakatishaji fedha

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,179
2,940
Leo April 30, 2018 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa amri kwamba mwenyekiti wa usajili wa Simba SC, Zacharia Hans Poppe na Franklin Lauwo wakamatwe na wafikishwe mahakamani kuunganishwa katika kesi inayomkabili Rais wa Klabu hiyo, Evans Aveva na Makamu wake Kaburu.

Amri hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba baada ya Wakili wa TAKUKURU, Leonard Swai kubadilisha hati ya mashtaka na kuwaongeza watuhumiwa hao.

Swai amedai amewatafuta washtakiwa hao toka mwezi wa tatu bila mafanikio na kuomba hati ya kuwakamata washtakiwa hao ambao hawakuepo mahakamani.

Washtakiwa hao wameongezwa katika kesi ya utakatishaji fedha na kugushi inayomkabili Rais wa Simba, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ .

images (26).jpeg
 
Hivi "utakatishaji fedha" ndio nini?wajuzi tusaidieni maana hata sielewi hawa jamaa walifanyeje?
 
Utakatishaji fedha au Money laundering kwa kifupi ni kuchukua mapato yatokanayo na biashara haramu kama uuzaji wa dawa za kulevya, Silaha ama kusafirisha binadamu nk na kuyaingiza mapato hayo kwenye mfumo halali wa uchumi wa nchi kwa kufanya biashara halali
 
Hivi "utakatishaji fedha" ndio nini?wajuzi tusaidieni maana hata sielewi hawa jamaa walifanyeje?
Unapata fedha Haramu (mfano za kupora benki, madawa ya kulevya, dili serikalini n.k) halafu unatumia Miradi halali (mfano unaanzisha biashara ya night club, kiwanda) kupumbaza Umma wasijue hela umetoa wapi.

Hiyo ndiyo kutakatisha fedha
 
Kuna siku Elungata alisha wahi kusema kitu kama hicho hapa jf, sijui kama atakuwa anakumbuka,

Jamaa ndiyo aliye toa milion 30, kwenye uchanguzi wa mwaka 2015 kwenye mkutano wa CDM na wadau sijui ulifanyika ukumbi gani vile wa kuomba msaada wa hela kumalizia kampeni za uchanguzi mkuu..

Anatafutwa kwa mlango wa nyuma usio wa kisiasa patamu hapo....
 
Back
Top Bottom