Queen V
JF-Expert Member
- Jan 19, 2012
- 775
- 1,332
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa hati ya kumkamata msanii, Agnes Gerald maarufu kama Masogange kwa kushindwa kuhudhuria kwenye kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili.
Hati hiyo ilitolewa jana mbele ya Hakimu Mkazi mkuu, Wilbroad Mashauri, wakati kesi hiyo ilipotajwa.
Wakili wa Serikali, Adolf Mkini alidai mahakamani hapo kwamba upelelezi wa kesi hiyo upo hatua za mwisho, lakini mshtakiwa, wadhamini wake na wakili wake hawakufika hivyo wakili Nkini akaomba mahakama itoe hati ya kumkamata mshtakiwa huyo kwa sababu ni mara ya pili ameshindwa kufika mahakamani hapo.
Hakimu Mashauri alikubali maombi ya wakili wa Serikali na kutoa hati ya kumkamata mshtakiwa ambaye ni Masogange.
Msanii huyo aliwahi kuonywa akitakiwa aheshimu mahakama kutokana na kutokuwapo kwenye kesi yake ilipotajwa.
Katika kesi hiyo namba 77 ya mwaka 2017, Masogange anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14 mwaka huu, katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam, alitumia dawa za kulevya aina ya heroin(Diacety Imophine). Pia inadaiwa kati ya Februari 7 na 14, 2017 alitumia dawa za kulevya aina ya oxazepam.
Chanzo: Mtanzania
=====
Mfululizo wa kukamatwa, kesi, hukumu na kuachiwa huru kwa Agnes Masogange kwenye kesi ya Madawa ya kulevya
- Masogange akamatwa kwa tuhuma za kuhusika na Dawa za Kulevya
- Mwakyembe: Awamu iliyopita aliyetuwezesha kukamata 99% ya madawa ya kulevya aliishia jela
- Jeshi la polisi Tanzania laamua kumfuata Agness Masogange Afrika Kusini...!!
- Polisi aeleza alivyohangaika na Masogange
- Kamanda Sirro: Mbowe jisalimishe Polisi; Masogange, Chid Mapenzi, Wallis Nasher tumewakuta na madawa
Kupandishwa kizimbani na kusomewa shitaka
Yaliyojili wakati wa kesi ya Masogange
- Mwakyembe aagiza wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wakamatwe!
- Masogange awataja wamiliki wa mzigo aliokamatwa nao SA
- Hatimaye Masogange amtaja aliye mtuma mzigo wa dawa za kulevya
- Kumekucha Madawa ya Kulevya: Kina 'Masogange' wawataja waliowatuma!
- Mahakama yashindwa kusoma kesi ya Masogange; adaiwa kuwa mgonjwa
- Kumekucha Madawa ya Kulevya: Kina 'Masogange' wawataja waliowatuma!
- Dawa za Kulevya: Wema adai Makonda anatembea na Agnes Masogange ndio maana hakamatwi
- Kesi ya Masogange yakwama kusikilizwa tena
- Kisutu: Korti yakataa vielelezo vya ushahidi kesi ya Wema Sepetu. Masogange akutwa na kesi ya kujibu
- Muendelezo Vita Dawa ya Kulevya: Masogange apelekwa kwa Mkemia Mk
- Mahakama yakubali kuutumia mkojo wa Masogange, yasema fomu za mkemia zilifata sheria
- Sampuli ya mkojo wa Agness Masogange wakutwa na Heroin
Hukumu