Mahakama yatoa Amri Askofu Mokiwa na Wenzake wakamatwe kwa kutotii mahakama!

mambo ya dini yana mahakama zake Mbinguni. hakuna mamlaka iliyojuu zaidi ya ile itokayo kwa Mungu. hata hivyo waumini tulishaambiwa tumdharau kikwete baada ya saa 48. hiyo ni uthibitisho tu kwamba kikwete anadharaulika.

dare for more?

Dini pia zinatuamuru kuheshimu mamlaka tulizoziweka hapa duniani!
 
Dini pia zinatuamuru kuheshimu mamlaka tulizoziweka hapa duniani!
Inapotokea sheria za mamlaka za duniani zinatofautiana na dini husika kama ya hili suala, tufuate sheria ipi? Maana kumsimika au kutomsimika Askofu au Shekhe si suala la Mahakama.
 
kama polisi watatimiza hiyo amri ya mahakama
CCM kwa heri more enemies

Kama kanisa linataka kuingilia mamlaka za kiserikali kwa kuwa tu wana chuki za kisiasa basi bila shaka watashughulikiwa kisiasa! Mnawapoteza kuwadanganya kwa hayo wayafanyayo. 9i busarakuwaeleza hawa viongozi wetu wa dini, wao ni kioocha jamii zetu, si busara kufanya mambo yatakayosababisha mgawanyiko kwenye nchi hii, wakidhani buasara itatumika huku sheria ikipindishwa kutokana na nafasi zao. Wajiangalie upya na wajitathmini juu ya umuhimu wao kwa nchi hii!
 
hivi kuna uingiliano gani hapa,kwani kutangazwa kwa askofu kunahitaji baraka za mahakama......haya mambo ya taratibu za dini na serikali mi sijui chochote,tujuzeni
 
Kwa kweli hii kali'
Serikali isiyo na dini inaingiliaje mambo ya dini?
Waumini wakianglikana hawana vyombo vyao vya kuwekeana mapingamizi mpaka washtaki mahakamani!

I am very proud to be a catholic!
 
Ya Mungu mpeni Mungu na ya Kaisari mpeni Kaisari. Mahakama zikianza kuchanganya shughuli za mahakama na mambo ya dini soon moto utawaka
 
Kwa kweli hii kali'
Serikali isiyo na dini inaingiliaje mambo ya dini?
Waumini wakianglikana hawana vyombo vyao vya kuwekeana mapingamizi mpaka washtaki mahakamani!

I am very proud to be a catholic!

kaunga,hongera kwa kuwa catholic,hawa utawahi kuwasikia wahakamani! Hongera.
 
hivi mahakama za tanzania mbona zinashangaza kiasi hicho, toka lini mahakama ikajihusisha na mambo ya uchunguzi na uendeshaji wa kesi! Mahakama inatakiwa kujiwekea mipaka ili hisijidhalilishe yenyewe mbele ya jamii maana ikifikia hatua jamii ikaiona kama chombo kisicho na maana na kama sehemu ya serikali kuu basi mahakama watakuwa wamejimaliza wenyewe na wala wasitafute mchawi.

Walizuia kusimikwa kwa askofu kwa sheria hipi?! Na makosa yaliyofunguliwa na nani?! Hivi serikali iliposema mahakama ya kadhi ifunguliwe nje ya utaratibu wa mahakama ya tanzania walikuwa na maana gani?! Kama mahakimu za arusha ni vichekesho hivi.

Hakuna katika list ya sheria za tanzania hata moja ambayo mahakama inataka kutumia katika hili swala labda kama wanataka kutumia kanuni za kanisa au biblia sasa sijui kama mahakama hawaoni mpaka hapo kwasababu gani?!

ukiona hivyo mkuu ujue kuna mkono wa serikari ya magamba nyuma ya jambo hili
 
kama kanisa linataka kuingilia mamlaka za kiserikali kwa kuwa tu wana chuki za kisiasa basi bila shaka watashughulikiwa kisiasa! Mnawapoteza kuwadanganya kwa hayo wayafanyayo. 9i busarakuwaeleza hawa viongozi wetu wa dini, wao ni kioocha jamii zetu, si busara kufanya mambo yatakayosababisha mgawanyiko kwenye nchi hii, wakidhani buasara itatumika huku sheria ikipindishwa kutokana na nafasi zao. Wajiangalie upya na wajitathmini juu ya umuhimu wao kwa nchi hii!

mkuu tambua kuwa dini ni imani na mtu asiyeridhika na mwenendo wa viongozi wake wa dini au matokeo yoyote huwa huru kujiondoa,kuanzisha kanisa linalokubaliana na msimamo wake,au kutafuta suluhu ndani ya taasisi za dini husika lkn si kjwenda mahakamani kwa kuwa suala hili si madai wala jinai.jambo hili linaonekana kuwa dogo lakini linaweza kuleta matatizo makubwa kama polisi wetu watatekeleza amri hii isiyo na mashiko.
 
Mahakama inatakiwa kuhandle hii isssue with care kwani inaweza kuchukua sura ya kidini na kuibua hisia mbaya miongoni mwa wananchi.
 
kaunga,hongera kwa kuwa catholic,hawa utawahi kuwasikia wahakamani! Hongera.

Teh teh teh teh Uko sahihi kabisa ebu julize mtu kama yule Padri karugendo angemaua kwenda mahakamani kwa issue zake amabzo hakubalini na msimamo wa kanisa. Lakini sio kwamba RC hakuna migogoro ni kwamba kuna stable organisation structure ya namna ya kufanya mambo. na kudeal na wakaidi.


Nadhani Kwa kwenda mahakamani hao waumini wangetengwa tu then kisheria kanisa likawaambia mahakama hao waleta kesi wameshatengwa kwa utaratibu halali na kanisa na haliwatambui kama waumini wake so hawana hoja. As simple as that.

Mahakama inatakiwa kuhandle hii isssue with care kwani inaweza kuchukua sura ya kidini na kuibua hisia mbaya miongoni mwa wananchi.

Mahakama inataiwa ifuate sheria tu sio kuhandle kwa carekwani kuna issue mahakama hazitakiwi kuzihandle kwa care??? Wananchi hatutakiwi kuwa na kasumba kuwa issue ya XXYZ mwenyeeiti wa cham HHHHH kudharau mahakama iwe handled tofauti na issue ya Mkulima BBB kudharau mahakama
 
Hii nimeipenda kwa sababu sasa watanzania wataona uwezo wa hawa mahakimu wetu wa kudesa maana swala lipo wazi kuwa ameapishwa kuwa Askofu wa ANGLIKANA TANZANIA na wala si DAYOSIS YA MOUNT KILIMANJARO. Hivyo ni vitu viwili tofauti.
Hata hivyo tutapata wasaa wa kuassess kauli ya Kova 'police' kuwa wao wapo kutekeleza amri ya mahakama, hivyo tunategemea kamamnda Kova atamkamata Askofu Mokiwa haraka iwezekanavyo na kumpeleka Arusha kama ilivyokuwa kwa Mh. Mbowe ili haki itendeke!
 
Mahakama ya kiraia ilipaswa kutopokea kesi hiyo. Ingeirudisha kwa kanisa na kushauri jambo hilo lishughulikiwe kufuatana na taratibu za kanisa husika. Naamini kanisa anglikana lina taratibu zake za kutatua migogoro. Wana mabaraza na bodi za ushauri katika provinsi zao na kanda
 
Mahakama ya kiraia ilipaswa kutopokea kesi hiyo. Ingeirudisha kwa kanisa na kushauri jambo hilo lishughulikiwe kufuatana na taratibu za kanisa husika. Naamini kanisa anglikana lina taratibu zake za kutatua migogoro. Wana mabaraza na bodi za ushauri katika provinsi zao na kanda

Ndivyo mahakama zilizostaarabika zinavyofanya, hii habari haingepokelewa mahakamani kiholela hivyo. Hakimu angekuwa na busara kidogo angewashauri hao waliokwenda mahakamani warudi huko huko wafuate taratibu za Kikanisa kwanza. Lakini kwa kuwa tuna mahakimu viangazi ndio hapo tunashuhudia mapuuzi kama haya.
 
Ananufaika kwa sababu Kikwete ni rais mdini na sera yake ni udini, kwanza mimi nashangaa hivi Arusha kuna mahakama toka lini?
Au ndio ile mahakama iliyosema Mbowe akamatwe kufika kule mahakamani wanamwambia hana kesi ya kujibu?
By the way kama nchi hii kuna mahakama kweli mbona serikali imeamriwa na mahakama imlipe Valambhia lakini mpaka leo hajarlpwa?

Hii mahakama inataka sifa; si ndiyo iliamuru mwenyekiti CDM akamatwe, sasa ni zamu ya askofu! Shame on the mahakama na hakimu mhusika!:lock1:
 
Back
Top Bottom