Mahakama yatoa Amri Askofu Mokiwa na Wenzake wakamatwe kwa kutotii mahakama!

Wiki iliyopita mahakama mkoani Arusha ilitoa amri kuzuia kusimikwa kwa askofu mmojawapo wa kanisa la anglikana mkoani humo kufuatia kesi iliyofunguliwa na waumini watatu wa kanisa hilo. Licha ya amri hiyo HALALI ya mahakama jana askofu huyo amesimikwa hadharani katika sherehe iliyohudhuliwa na askofu mkuu wa kanisa hilo Valentino mokiwa. Najiuliza maswali, je kanisa liko juu ya sheria kiasi cha kutotii amri ya mahakama?Je tutarajie hakimu atoe hati ya kukamatwa askofu mokiwa na wenzake kwa kukiuka amri halali ya mahakama? Je mahakama itamzuia askofu huyo kutimiza majukumu yake ya kichungaji???? Je si kwamba kitendo hicho kimeidhalilisha mahakama na kuishushia hadhi mbele ya jamii na kuonekana amri yake si lolote si chochote? Yote haya ni maswali yanayohitaji majibu.
Jifunze kuandika heading,au unadhani unaandikia magazeti ya udaku! kuhudhulia kusimikwa kwa huyo askofu hakumfanyi mokia kuwa amedharau mahakama
 
Migogoro yote ya Kanisa anglicana dayosisi ya Mt. kilimanjaro inatookeaga St. james parishi. Na waanzilishi ni haohao. Nadahnia wanaitaji maombi zaidi.

Hujui usemalo; na sikal usikialo lazima uliamini. Saint James imehusika vipi? Unawajua vizuri hao waumini walioanzisha hilo zogo? Watu watatu, tena waumini wa kawaida unawajumuishaji na Kanisa zima?
 
Wiki iliyopita mahakama mkoani Arusha ilitoa amri kuzuia kusimikwa kwa askofu mmojawapo wa kanisa la anglikana mkoani humo kufuatia kesi iliyofunguliwa na waumini watatu wa kanisa hilo.

Licha ya amri hiyo
HALALI ya mahakama jana askofu huyo amesimikwa hadharani katika sherehe iliyohudhuliwa na askofu mkuu wa kanisa hilo Valentino mokiwa. Najiuliza maswali, je kanisa liko juu ya sheria kiasi cha kutotii amri ya mahakama?

Je tutarajie hakimu atoe hati ya kukamatwa askofu mokiwa na wenzake kwa kukiuka amri halali ya mahakama?

Je mahakama itamzuia askofu huyo kutimiza majukumu yake ya kichungaji???? Je si kwamba kitendo hicho kimeidhalilisha mahakama na kuishushia hadhi mbele ya jamii na kuonekana amri yake si lolote si chochote? Yote haya ni maswali yanayohitaji majibu.
Peleka kwenye Jukwaa la Sheria (The Law Forum)
 
Kwa hiyo mahakama na hakimu wamechemka kutoa amri ya Dr. Mokiwa kukamatwa? Kama mahakama ilizuia askofu wa Kilimanjaro asisimikwe na aliyesimikwa ni kwa Tanzania hapo tatizo liko wapi? Itabidi mahakama iifute hiyo hati ya kukamatwa kwa Dr. Mokiwa kwa kukiuka amri ya mahakama la sivyo tutadhani kuna mkono wa mtu hapo? Huyo Dr. Mokiwa si ndiye aliyetoa saa 48 kwa Kikwete kuwataja wauza unga alipochemsha kwa kuwasema maaskofu wanajihusisha na madawa yakulevya?

Tiba

Hapo ndo kwenye tatizo na ndio tunadhani kuwa nyuma ya uamuzi huo kuna mambo ya siasa. Askofu wa Dayosisi ya Mount Kilimanjaro hajasimikwa bado, Jaji kwa ukihiyo wake na kuchukulia mambo kijuu-juu au kwa kutekeleza matakwa ama ya kisasa au mengineyo kakurupuka ati Askofu wa Dayosisi ya Mount Kilimanjaro kasimikwa!

Akofu Mokiwa alikuwa very clear jana kuwa Tunamsimika Askofu wa Kanisa Anglikana Tanzania, Jumapili ijayo (bila shaka kwa kuzingatia amri ya mahakama na ahadi ya kutoa uamuzi leo). Nadhani tunaelekea kwenye mgogoro mwingine wa Kisheria . Je mahakama haiwezi kudaiwa fidia kwa kupotosha hukumu kwa makusudi?
 
Huyu Valentino Mokiwa si ndiye aliyempa Kikwete saa 48 kutaja vioangozi wa dini wanaojihusisha na madawa ya kulevya!

Sasa hapo ndiyo atamtambua Kikwete na semena elekezi yake.
 
Kiswahili kina pekechuliwa, hii kusimikwa imetokana na neno kusimika? Kama kwenye "dudu" inavyo simika? Mnashangaza!
Dada unapepo baya linakusumbua wewe! Unawaza "dudu" huo kichwani kwako maana ndio imekupapia hata kazi hapa JF. Kweli Sheikh Yahya alisema wote mna mapepo!
 
Wewe mleta mada una matatizo,kivipi?heading ya thread yako ina tofauti kubwa na main body (presentation) unayotuletea,hatupo kuongelea speculations humu ndani,una jambo toa data,unauliza sema naomba kusaidiwa vinginevyo rudi kwa Nauye...unajidharaulisha mkuu!
 
Mahakama ilitoa amri ya kusimikwa kwa Askofu wa Dayosisi ya Kilimanjaro, alichofanya Askofu Mokiwa na wenzake ni kumsimika Askofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania lakini hajasimikwa kuwa Askofu wa Dayosisi ya Kilimanjaro!! Kesi ikiisha kama atashinda basi atasimikwa kuwa Askofu wa Anglikana Dayosisi ya Kilimanjaro. Kwa sasa anabaki kuwa na cheo cha uaskofu bila kuwa na Dayaosisi kama vile kina Askofu Donald Mtetemela, Askofu John Ramadhani n.k.
Hivi haya mambo gani! Mambo ya DINI tangu lini mahakama ikahusikana nayo? Kwani mambo ya CANON LAW yamo kwenye sheria zetu za nchi hii? Mimi naona kama bahadhi ya madhehebu yamegeuzwa kama kitega uchumi/biashara, kwa nini tushangae wakati Jakaya aliposema bahadhi ya wakuu wa DINI ni Kingpin wa madawa ya kulevya - haya mambo ya Maaskofu kuamua kufikishana mahakamani si jambo la KAWAIDA hata kidogo, kuna KITU.
 
Mimi nadhani yote ni mazuri tu haya na viongozi wa Kanisa waonje mgongano wao na wanasiasa; wamekuwa wakikumbatiana sana hadi wengine wamejisahau. Lakini ni nzuri pia kwa sababu inazidi kuwaonesha wananchi maana ya double standard hasa litakapotokea kwa viongozi wa CCM na serikali hasa wale wa ngazi za juu.

Mzee Mwanakijiji, hivi kuna sheria ya nchi inayoipa mahakama nguvu ya kuamua migogoro ya ki imani?
 
mambo ya dini yana mahakama zake Mbinguni. hakuna mamlaka iliyojuu zaidi ya ile itokayo kwa Mungu. hata hivyo waumini tulishaambiwa tumdharau kikwete baada ya saa 48. hiyo ni uthibitisho tu kwamba kikwete anadharaulika.

dare for more?

du...sikuwezi kaka kwa makombora yako!

maana hata signature yako.....bifu bifu tu!
 
Mahakama ilitoa amri ya kusimikwa kwa Askofu wa Dayosisi ya Kilimanjaro, alichofanya Askofu Mokiwa na wenzake ni kumsimika Askofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania lakini hajasimikwa kuwa Askofu wa Dayosisi ya Kilimanjaro!! Kesi ikiisha kama atashinda basi atasimikwa kuwa Askofu wa Anglikana Dayosisi ya Kilimanjaro. Kwa sasa anabaki kuwa na cheo cha uaskofu bila kuwa na Dayaosisi kama vile kina Askofu Donald Mtetemela, Askofu John Ramadhani n.k.

kwangu mimi yote haya ni ya kidunia na kanisa la anglicana linazidi kutibitisha udhaifu wao wa kufanya mambo yao hadi kwenda mahakamani ambapo hakuna undani wa neno la mungu kama kanisa lenyewe

If i was Mokiwa, ningeacha kazi ya utumishi kwani kwenda mahakama hata FIFA wanakufungia ijekua nyumba ya Mungu?
 
Kwa hiyo mahakama na hakimu wamechemka kutoa amri ya Dr. Mokiwa kukamatwa? Kama mahakama ilizuia askofu wa Kilimanjaro asisimikwe na aliyesimikwa ni kwa Tanzania hapo tatizo liko wapi? Itabidi mahakama iifute hiyo hati ya kukamatwa kwa Dr. Mokiwa kwa kukiuka amri ya mahakama la sivyo tutadhani kuna mkono wa mtu hapo? Huyo Dr. Mokiwa si ndiye aliyetoa saa 48 kwa Kikwete kuwataja wauza unga alipochemsha kwa kuwasema maaskofu wanajihusisha na madawa yakulevya? Tiba
Mahakama ikikosea inafanywaje. "Hakuna mtu aliye juu ya sheria".
 
Back
Top Bottom