Mkwawa
JF-Expert Member
- Jun 8, 2011
- 1,334
- 1,464
Naomba kujua anapoabudu mheshimiwa judge!
Utamwonea Judge bure. Niliwahi kuongea na Jaji mmoja amaye kwa sasa ni mwenyeki wa baraza la maadili Tanzania . Baada ya Maongezi ya Muda mrefu na kutaka kujua jinsi mahakama za Tanzania zinavyotoa haki. Mmoja wetu akataka kujua kama wanasiasa hasa ikulu inahusika na kutoa haki mahamani. Alikataa sana, ila alipobanwa na kupewa baadhi ya facts mojawapo ikiwa kesi ya marehemu Ukiwaona. Alikubali kuwa ikulu huwa inaingilia hukumu na kutoa maelekezo nini kifanyike kwa mtuhumiwa au kesi husika.
Ila alisema kuna baadhi ya Majaji shupavu hukataa, ila sio wengi kwani ajira iko mikononi mwa Raisi.