Mahakama yatoa Amri Askofu Mokiwa na Wenzake wakamatwe kwa kutotii mahakama! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahakama yatoa Amri Askofu Mokiwa na Wenzake wakamatwe kwa kutotii mahakama!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by samirnasri, Jun 13, 2011.

 1. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Wiki iliyopita mahakama mkoani Arusha ilitoa amri kuzuia kusimikwa kwa askofu mmojawapo wa kanisa la anglikana mkoani humo kufuatia kesi iliyofunguliwa na waumini watatu wa kanisa hilo.

  Licha ya amri hiyo
  HALALI ya mahakama jana askofu huyo amesimikwa hadharani katika sherehe iliyohudhuliwa na askofu mkuu wa kanisa hilo Valentino mokiwa. Najiuliza maswali, je kanisa liko juu ya sheria kiasi cha kutotii amri ya mahakama?

  Je tutarajie hakimu atoe hati ya kukamatwa askofu mokiwa na wenzake kwa kukiuka amri halali ya mahakama?

  Je mahakama itamzuia askofu huyo kutimiza majukumu yake ya kichungaji???? Je si kwamba kitendo hicho kimeidhalilisha mahakama na kuishushia hadhi mbele ya jamii na kuonekana amri yake si lolote si chochote? Yote haya ni maswali yanayohitaji majibu.
   
 2. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,438
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mahakama ilitoa amri ya kusimikwa kwa Askofu wa Dayosisi ya Kilimanjaro, alichofanya Askofu Mokiwa na wenzake ni kumsimika Askofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania lakini hajasimikwa kuwa Askofu wa Dayosisi ya Kilimanjaro!! Kesi ikiisha kama atashinda basi atasimikwa kuwa Askofu wa Anglikana Dayosisi ya Kilimanjaro. Kwa sasa anabaki kuwa na cheo cha uaskofu bila kuwa na Dayaosisi kama vile kina Askofu Donald Mtetemela, Askofu John Ramadhani n.k.
   
 3. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  mambo ya dini yana mahakama zake Mbinguni. hakuna mamlaka iliyojuu zaidi ya ile itokayo kwa Mungu. hata hivyo waumini tulishaambiwa tumdharau kikwete baada ya saa 48. hiyo ni uthibitisho tu kwamba kikwete anadharaulika.

  dare for more?
   
 4. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #4
  Jun 13, 2011
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  sasa ni wazi, amri ya kumkamata Mokiwa na Askofu Hotay imetolewa tayari na polisi wanahaha kila upande kuwatafuta.
   
 5. Yousuph .M.

  Yousuph .M. Senior Member

  #5
  Jun 13, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naona muingiliano hapa mkuu,
  Kikwete ameingiaje ktk hili, au ndiye aliyetoa agizo la kusitisha usimikwaji wa huyo askofu? Anafaidikaje yeye kama Kikwete ktk hili?
  Nahisi ukakasi.
   
 6. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #6
  Jun 13, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280
  Ananufaika kwa sababu Kikwete ni rais mdini na sera yake ni udini, kwanza mimi nashangaa hivi Arusha kuna mahakama toka lini?
  Au ndio ile mahakama iliyosema Mbowe akamatwe kufika kule mahakamani wanamwambia hana kesi ya kujibu?
  By the way kama nchi hii kuna mahakama kweli mbona serikali imeamriwa na mahakama imlipe Valambhia lakini mpaka leo hajarlpwa?
   
 7. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #7
  Jun 13, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,422
  Likes Received: 393
  Trophy Points: 180
  Wakuu nimepata hii habari kutoka Radio One breaking news kwamba Askofu Dr. Mokiwa kukamatwa kwa amri ya mahakama ya Arusha. Ni kwa nini? inauhusiano na kesi ya akinaMbowe?
   
 8. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #8
  Jun 13, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,422
  Likes Received: 393
  Trophy Points: 180
  Tena mahakama yenyewe ni ya Arusha!
   
 9. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #9
  Jun 13, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,422
  Likes Received: 393
  Trophy Points: 180
  Sijui watutumiwa dege la jeshi tena au?
   
 10. m

  mob JF-Expert Member

  #10
  Jun 13, 2011
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,027
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  kama ni kuwakamata lazima busara itumike vingine watu wanaweza wakachukua kama ni ishu ya udini ndani yake.na pia nadhani watu wanajua madhara ya udini
   
 11. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #11
  Jun 13, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  Askofu Dr Mokiwa ni mkuu wa kanisa la Anglican Tanzania sidhani kama kuna uhusiano na kesi ya akina Mbowe.


  Jana Askofu Dr Mokiwa alishiriki kumweka wakfu Askofu wa Anglikana jimbo la Arusha.Upo mgogoro wa uchaguzi wa Askofu jimbo la Arusha nadhani kulikuwa na amri ya mahakama kuzuia kusimikwa Askofu alieshinda uchaguzi.Askofu Dr Mokiwa bila kujali amri ya mahakama waliendelea na zoezi la kumsimika Askofu anayelalamikiwa.
   
 12. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #12
  Jun 13, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Hivi Mahakama za Tanzania mbona zinashangaza kiasi hicho, toka lini mahakama ikajihusisha na mambo ya uchunguzi na uendeshaji wa kesi! Mahakama inatakiwa kujiwekea mipaka ili hisijidhalilishe yenyewe mbele ya jamii maana ikifikia hatua jamii ikaiona kama chombo kisicho na maana na kama sehemu ya serikali kuu basi mahakama watakuwa wamejimaliza wenyewe na wala wasitafute mchawi.

  Walizuia kusimikwa kwa Askofu kwa sheria hipi?! na makosa yaliyofunguliwa na nani?! Hivi serikali iliposema Mahakama ya kadhi ifunguliwe nje ya utaratibu wa mahakama ya Tanzania walikuwa na maana gani?! kama mahakimu za Arusha ni vichekesho hivi.

  Hakuna katika list ya sheria za Tanzania hata moja ambayo mahakama inataka kutumia katika hili swala labda kama wanataka kutumia kanuni za kanisa au Biblia sasa sijui kama mahakama hawaoni mpaka hapo kwasababu gani?!
   
 13. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #13
  Jun 13, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Waangalikana nao. Mambo yenu ya uaskofu mpaka mahakamani?
   
 14. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #14
  Jun 13, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280

  Wamchukue na ndege ya jeshi kama alivyofanyiwa Mbowe.
   
 15. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #15
  Jun 13, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  1.Mtoa mada naomba unijuze dini ya serikali ni ipi?
  2.Mtu akiwa askofu hashitakiwi?
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Jun 13, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mimi nadhani yote ni mazuri tu haya na viongozi wa Kanisa waonje mgongano wao na wanasiasa; wamekuwa wakikumbatiana sana hadi wengine wamejisahau. Lakini ni nzuri pia kwa sababu inazidi kuwaonesha wananchi maana ya double standard hasa litakapotokea kwa viongozi wa CCM na serikali hasa wale wa ngazi za juu.
   
 17. N

  Nguto JF-Expert Member

  #17
  Jun 13, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,653
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Mbona kichwa cha habari tofauti na habari yako uliyoileta hapa?
   
 18. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #18
  Jun 13, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  MATUMIZI YA AKILI YANATAKIWA KWANI .....THE LAW IS BLIND,SO ARE THE LAWYERS.... watatekelza kitu ambacho kitaibua kubwa kuliko cha mwanzo
   
 19. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #19
  Jun 13, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mbona haya ni masuala ya DINI?
  modS' Please take this OUT of here.
  Now now...
   
 20. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #20
  Jun 13, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kwa mwendo huu tusio na imani tunaamini kanisa sasa hivi ni moja ya ujasilia mali
   
Loading...