Mahakama yataka serikali kugharimia kesi za uchaguzi

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
Mahakama yataka serikali kugharimia kesi za uchaguzi Thursday, 16 December 2010 20:43

James Magai
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imeitaka serikali ibebe mzigo wa gharama zote za uendeshaji wa kesi za uchaguzi zilizofunguliwa katika vituo mbalimbali vya mahakama hiyo, kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 31 mwaka huu.

Mahakama pia imetoa angalizo kwa ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, akiwa mdau mkubwa katika kesi hizo kuwa lazima ijiandae na kuwezeshwa ili kuruhusu mashauri hayo, kuendelea na kumalizika kwa wakati bila kukwama.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Jaji Kiongozi Fakihi Jundu, alisema kufikia Desemba 10 mwaka huu jumla ya kesi 43 za kupinga matokeo ya ubunge, zilikuwa zimefunguliwa katika vituo 11 kati ya 13 vya Mahakama Kuu ya Tanzania

Uwingi wa kesi hizo za uchaguzi katika uchaguzi wa mwaka huu unaonekana kuwa mzigo mkubwa ambao serikali italazimika kuubeba kugharimia gharama za uendeshaji wake.
Jaji Jundu alisema katika kuyashughulikia mashauri hayo kwa wakati na kwa haki, inakadiriwa kuwa kiasi cha Sh.2.263 bilioni kitahitajika.

"Izingatiwe kuwa ili haki itendeke na ionekane kutendeka, jaji hatasikiliza kesi katika kituo chake cha kawaida cha kazi. Tutalazimika kuwasafirisha kutoka kituo kimoja kwenda kituo kingine," alisema Jaji Jundu
Alibainisha kuwa lengo la kuwahamisha majaji hao kwenda kusikiliza kesi hizo nje ya vituo vyao, ni kuruhusu haki kutendeka kwa kuondoa dhana kwamba jaji anaweza kuwa na mawasiliano na uhusiano na upande mmoja katika kesi hiyo.

"Kwa kuzingatia yote hayo, itagharimu kiasi cha Sh.52,644,000 kwa kila kesi. Hivyo tunahitaji kiasi cha Sh.2,263,692,000 kuendesha mashauri haya. Fedha hizi sisi hatuna na mzigo ambao serikali lazima iubebe,"alisema.
Jaji Jundu alisema tayari wameishaiandikia Hazina kueleza mahitaji ya fedha hizo na kwamba baada ya majaji kutoka likizo Februa mwakani na kama serikali itakuwa imeshatoa fedha hizo, kazi ya kusikiliza kesi hizo itaanza mara moja.

Alisema uendeshaji wa kesi hizo ni gharama kubwa lakini kwa kuwa serikali ya Tanzania inaamini katika demokrasia, haina budi kubeba mzigo huo kwa kuwa demokrasia ni gharama.
"Serikali lazima itoe hela kwa hili, haiwezi kuwepa isipotoa zitakwama, sisi tunatekeleza matakwa ya katiba," alisisitiza Jaji Jundu wajibu wa serikali kugharimia kesi hizo.
"Tunaiomba serikali kuiwezesha mahakama ili itemize jukumu hili muhimu katika kulinda heshima ya nchi yetu," alisisitiza.

Akizungumzia utaratibu wa uendeshaji wa kesi hizo, Jaji Jundu alisema kwa mujibu wa sheria ya Uchaguzi namba 1 ya mwaka 1985 kifungu cha 115 (2),mashauri hayo yanapaswa kuwa yamekamilika ndani ya kipindi cha miaka miwili tangu kufunguliwa.
Jaji Kiongozi alisema inakisiwa kuwa kila kesi itasikilizwa kwa muda wa siku zisizopungua 45 na kwamba kila kesi itakuwa na mashahidi 15.

Hata hivyo alisema kisheria iwapo muda huo utaisha kabla ya kesi hizo kumalizika, Waziri wa Katiba na Sheria kwa kujadiliana na Jaji Mkuu wataongeza muda wa miezi sita wa kusikiliza mashauri hayo.
Alisema kuwa kutokana na umuhimu wa kesi hizo za uchaguzi, mahakama imezipa kipaumbele na kwamba tayari wameshajipanga katika kuzishughulikia kikamilifu.

Akielezea jinsi mahakama ilivyojipanga kushughulikia kesi hizo alisema Septemba 17 kilifanyika kikao cha Majaji Wafawidhi katika Hoteli ya Kunduchi jijini Dar es Salaam ambapo walijadili sheria mbalimbali zinazohusu masuala ya uchaguzi.
 
"Izingatiwe kuwa ili haki itendeke na ionekane kutendeka, jaji hatasikiliza kesi katika kituo chake cha kawaida cha kazi. Tutalazimika kuwasafirisha kutoka kituo kimoja kwenda kituo kingine," alisema Jaji Jundu
Alibainisha kuwa lengo la kuwahamisha majaji hao kwenda kusikiliza kesi hizo nje ya vituo vyao, ni kuruhusu haki kutendeka kwa kuondoa dhana kwamba jaji anaweza kuwa na mawasiliano na uhusiano na upande mmoja katika kesi hiyo.
Hii ni hoja ya kuongeza matumizi serikalini...........................Hivi kama Jaji hawezi kuaminika kama akisikiliza kesi kwenye kituo chake cha kawaida huyo hafai kuwa Jaji.....................

Hoja hizi zinatumiwa na mahakama kwa sababu wanaona kesi tajwa sasa ni kivuno kwao.......................

Kwa ushauri wangu.............kuwatendea haki watanzania wote wenye kesi lukuki mahakamani majaji wastaafu waitwe ili waziendeshe hizi kesi..............lipo tatizo kubwa la msongamano wa kesi mahakamani na kuwaondoa majaji wengi kuzisikiliza kesi za uchaguzi kwa minajili ya kupata allawansi kutachangia kuzorota usikilizwaji wa kesi nyingi zilizopo na zinazokuja....................
 
Jaji Kiongozi atishia kurejesha kesi za uchaguzi bungeni Send to a friend
Monday, 16 January 2012 20:47
0digg

James Magai
JAJI Kiongozi, Fakihi Jundu amesema Mahakama imelemewa na mzigo wa kesi za uchaguzi ambazo imeshindwa kuziendesha kutokana na kupewa bajeti finyu na kusema kwamba ikiwa hadi kufikia Mei mwaka huu haitakuwa imepewa fedha ilizoomba, itarejesha kesi hizo bungeni.Amesema hadi sasa Serikali imetoa Sh300 milioni kati ya Sh2.3 bilioni zilizoombwa na mhimili huo wa dola na kuonya kuwa kama fedha hizo hazitapatikana watazirudisha kesi hizo bungeni. Mahakama Kuu imeshapokea kesi 43 zilizofunguliwa kupinga matokeo baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2010.

Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana baada ya kumwapisha, Batista John Mhelela kuwa Kaimu Msajili wa Mahakama Kuu Sumbawanga, Jaji Jundu alisema kwa sasa Mahakama inakabiliwa na hali ngumu ya fedha.

"Tayari muda wa kawaida umeshakwisha na tumeomba muda wa nyongeza wa miezi sita ambao nao unakwisha Mei mwaka huu. Kama fedha zitakuwa hazitapatikana baada ya muda huo, itabidi suala hilo tulirudishe bungeni," alisema.

Jaji Jundu alisema kama fedha hizo zingepatikana kwa wakati, hadi sasa kesi hizo zingekuwa zimeshamalizika na pengine zingekuwa katika hatua ya Mahakama ya Rufani, lakini mahakama imeshindwa kuziendesha kutokana na kukosa fedha."Katika siku za hivi karibuni, hali ya Mahakama imekuwa ni ngumu sana kiasi cha kushindwa kutekeleza majukumu yake yakiwemo mashauri mbalimbali. Kwa mfano, kesi za uchaguzi mahakama imeweza kusikiliza nne tu kati 43," alisema.

Jaji Jundu alisema baada ya Bajeti ya Serikali ya 2011/2012 kupitishwa, Mahakama iliahidiwa kupewa Sh20 bilioni kwa ajili ya shughuli zake zote (nje ya fedha za kesi za uchaguzi) lakini hadi sasa imepewa ni chini ya Sh5 bilioni.
Alisema kutokana na hali hiyo ngumu ya fedha, meshindwa kuendesha hata kesi za mauaji na kesi nyingine zenye upekee ambazo mashahidi wanalazimika kugharamiwa jambo ambalo linaweza kusababisha wananchi kuitupia lawama.

Jaji Jundu alitoa mfano wa Uganda akisema ni nchi inayothamini kesi za uchaguzi kwani mara ti baada ya uchaguzi wa mwaka jana, Mahakama ilipewa fedha za kutosha kuendesha kesi hizo hivyo uamuzi wake kutolewa kwa wakati.
"Nasi kama tungeweza kufanya hivyo sasa hivi kesi hizo zingekuwa Mahakama ya Rufani. Hivyo Serikali inabidi ione umuhimu wa kutupatia fedha hizo, vinginevyo itakuwa ni lawama tu," alisema Jaji Jundu.

Pia aliikosoa Sheria ya Mfuko wa Mahakama akisema ina upungufu ambao itabidi baadaye Bunge liuangalie..."Kama mnavyokumbuka, mwaka jana Bunge lilipitisha Sheria ya Mfuko wa Mahakama, tulitarajia kuwa hili lingetusaidia lakini sheria hiyo haisemi kuwa tutapewa asilimia ngapi ya bajeti hivyo hutegemea tu jinsi Serikali inavyopanga."
"Jaji Mkuu aliyepita (Augustino Ramadhani) alipendekeza Mfuko wa Mahakama utengewe asilimia mbili ingawa hata wabunge wengine walijaribu kutaka kuweka asilimia kadhaa lakini haikuwa hivyo."

Alitoa mfano wa Sheria ya Mfuko wa Mahakama Kenya, kwamba hata Katiba yao inataja mahakama itapewa asilimia mbili ya bajeti.

Hata hivyo, alipotakiwa kuzungumzia madai hayo ya Jaji Jundu Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, alisema: "Mambo yanayohusu Mahakama ni vyema wakatuandikia moja kwa moja, lakini mimi ninachojua ni kuwa tumetoa fedha nyingi zaidi ya hizo."

"Haiji kwa waziri kumjibu Jaji Kiongozi kwenye simu kwa sababu Mahakama wana utaratibu wao wa kufanya kazi. Naweza kusema hivyo kesho nikajikuta kwenye matatizo."

Kesi za uchaguzi
Akitoa taarifa Desemba 16, 2010, ya kesi za uchaguzi zilizofunguliwa, Jaji Jundu alisema jumla ya kesi 43 zilikuwa zimefunguliwa katika vituo 11 kati ya 13 vya Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga matokeo ya ubunge, katika majimbo mbalimbali.

Alitoa angalizo kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, akiitaka ijiandae na kuwezeshwa ili kuruhusu mashauri hayo kuendelea na kumalizika kwa wakati bila kukwama.

Alisema katika kuyashughulikia mashauri hayo kwa wakati na kwa haki, inakadiriwa kuwa kiasi cha Sh2.263 bilioni kitahitajika na kwamba kila kesi itagharimu kiasi cha Sh52,644,000, huku akisisitiza kuwa huo mzigo ni lazima ubebwe na Serikali.

Kwa wanaoombwa rushwaKatika hatua nyingine, Jaji Jundu ametoa wito kwa wananchi wanaoombwa rushwa na mahakimu kutoa taarifa kwa uongozi wa mahakama ili waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua.Alisema ni kweli kumekuwa na mahakimu na watumishi wa mahakama wasio waaminifu lakini pia akasema wapo wengine ambao ni waaminifu.

"Wito wangu ni kwamba kama mwananchi akiombwa rushwa aje azilete hizo fedha na kusema ameombwa na hakimu fulani na ni hizi hapa sasa nazipeleka ili tuweze kumkamata, maana malalamiko mengine huwa ni vigumu ushahidi kupatikana," alisema Jaji Jundu.


 
kuzirudisha hizi kesi kwa wabunge ambao baadhi yao ni washtakiwa ni kujikaanga kwa mafuta yetu wenyewe...............suala hili ni jaji Mkuu ajadiliane na Raisi na spika wa Bunge......................na maamuzi yafanyike bila ya zengwe lolote lile............
 
Back
Top Bottom