Mahakama yataka kesi ya aliyekuwa Mhasibu Mkuu Takukuru itendewe haki

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
1.jpg

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema haki itendeke katika kesi ya kumiliki mali ya zaidi ya Sh3.6 bilioni kinyume na kipato halali inayomkabili aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru),Godfrey GugaI na wenzake wawili kwa kuwa washtakiwa hao hawana dhamana.

Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ameeleza hayo leo Oktoba 21, 2019 wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi lakini upande wa mashtaka kupitia Wakili wa Jamhuri, Sylvia Mitanto kudai kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi lakini mawakili wanaosimamia kesi hiyo hawapo wapo mahakama ya mafisadi.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Simba alisema hajafurahi kuona kesi hiyo inaahirishwa kwani lazima waitendee haki kwa sababu mashtaka yanayowakabili washtakiwa hayana dhamana.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 28 mwaka huu kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.

-Mpekuzi-
 
Sitoi kejeli.hakimu hapaswi kuonesha huruma mahakamani anapaswa kutoa maamuzi ya kisheria au kwasababu ni mawakili wa serikali wanakuja na hoja za kijinga mahakamani.ndio maana nasema hakimu analialia.sidhani kama huu upuuzi ungefanywa na mawakili wanaotetea wapinzani hakimu angekuja na malalamiko namna hii.
Hakimu anamuonea huruma mshitakiwa kuendelea kusota mahabusu We unakejeli
 
Afuate sheria.aache kulialia au kiti hakimtoshi analinda tumbo?
Hakimu yuko vizuri na anaweza kuifuta kesi kwa kile kifungu ambacho kina apply kwenye mazingira ambapo upande wa mashtaka una sua sua kuleta ushahidi. Lakini akiwachia watashikwa kwa kifungu hicho nao TAKUKURU watawakamata tena mlangoni na kusababisha kesi ianze upya.

Ila unapoona visingizio wanavyotoa upande wa mashtaka, ujue hawana ushahidi kwa hiyo wanaishia kumuacha mtuhumiwa asiye rumande bila dhamana.
 
Back
Top Bottom