Mahakama yataka Chenge akamatwe, Kikwete ambeba!

Raj Patel Jr. Mkuu kiswahili hukjiwezi... Mahabusu inaweza kumweka mtu kabla ya Hukumu hivyo sii wote waliopo mahabusu are gulity..Ukikosa bond unakaa mahabusu hadi kesi yako itakapomalizika, hivyo mtuhumiwa (suspect) is not a freeman. Hatakiwi kugombea uchaguzi.
 
f.png
 
Hii ni aibu na fegheha kwa Wananchi wa nchi hii kuwaachia makuwadi wa Mafisadi kuendelea kukomba hazina ya taifa kwa njia za ujanja ujanja. Jakaya tunakusubiri muda bado tunao.
 
Hivi hajakamatwa bado? ama kwa vile ni Fisadi nyangumi? ina maana huko aliko hamna polisi? ama huwa hawawasiliani kwahiyo inasubiliwa atakaye tumwa toka dar kwenda huko ndo amkamate?
 
Chenge mwenyekiti wa kamati ya maadili ya ccm.
Hakuna haja ya kujiuliza chama cha ccm ni cha mfumo gani. Ukimtizama tu Chenge basi unapata sura halisi ya chama. Hili ni tunda linalofanana na mti lilikotundwa!
 
Hapa kweli huyo hakimu lazima ahamishwe hii wiki hamalizi!!!


Jamaa kamfagilia mbaya sana kule sasa sijui itakuwaje!!!
 
Mahakama yaagiza Chenge akamatwe Monday, 27 September 2010 20:00

chengecrop.jpg
Mbunge wa Jimbo la Bariadi Magharibi Andrew Chenge

Ummy Muya
MGOMBEA urais wa Muungano, Jakaya Kikwete jana alimnadi bila mbwembwe Andrew Chenge jimboni kwake Bariadi Magharibi, huku Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kinondoni ikitoa ruhusa ya kukamatwa kwa mwanasheria huyo mkuu wa zamani kwa kushindwa kufika kortini.

Chenge anakabiliwa na mashtaka mawili ya kuendesha gari kizembe na kusababisha vifo vya watu wawili-Victoria George na Betrice Costantine- na shtaka jingine la kuendesha gari bila ya bima, lakini jana hakuwepo mahakamani.

Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Kwey Rusema hakuwepo mahakamani jana kutokana na kuhudhuria semina ya kikazi, lakini hakimu aliyemshikia shauri hilo, Sundi Fimbo alitoa kibali cha kukamatwa kwa waziri huyo wa zamani wa Afrika Mashariki kutokana na kutofika mahakamani bila ya kutoa taarifa.

Kabla ya kutoa kibali hicho, Hakimu Fimbo alihoji sababu za mshtakiwa kutofika mahakamani na akajibiwa na Simon Mponda, wakili anayemtetea Chenge, kuwa mteja wake yupo kwenye msafara wa Kikwete ambaye jana alikuwa na mkutano wa kampeni kwenye Jimbo la Bariadi Magharibi.

Lakini jibu la wakili huyo likakumbana na kauli kali kutoka kwa hakimu.

“Wewe haupaswi kutoa taarifa ya kutofika mahakamani mshtakiwa. Masuala hayo hufanywa na mshtakiwa mwenyewe ama wadhamini wake, nafikiri unafahamu hilo,” alisema Hakimu Fimbo.

“Kutokana na mshtakiwa kutofuata taratibu za kisheria, ninatoa kibali cha kumkamata,” alisema Fimbo.
Chenge alitakiwa kuanza kujitetea jana baada ya mahakama kumuona kuwa ana kesi ya kujibu katika mashtaka hayo matatu yanayomkabili ya kugonga pikipiki ya matairi matatu, maarufu kama Bajaj na kusababisha vifo hivyo.
Kutokuwepo kwake kulimfanya Hakimu Fimbo kuahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 5.

Wakati mahakama ikitoa kibali hicho, Ibrahim Bakari Bariadi anaripoti kutoka Bariadi kuwa Kikwete alimtambulisha Chenge na kumnadi kuwa anafaa katika mkutano wa hadhara ambao CCM ilisomba wanachama 223 kutoka UDP.

Kikwete alikuwa akihutubia maelfu ya wakazi wa jimbo hilo waliojitokeza kwenye Uwanja wa CCM Bariadi Magharibi ambako pia alipokea kadi mbili kutoka kwa watu waliojitambulisha kuwa wanatokea CUF na wameamua kujiunga na CCM.
Mmoja wa waliorudisha fomu alisema kuwa wameamua kumkacha kiongozi wa UDOP, John Mimosa Cheyo kwa madai kuwa hana mfumo wa utawala na hawakubaliana na mwenendo mzima wa chama ambao walisema haufanani na CCM.

Mbali na zoezi hilo, Kikwete alimnadi mgombea ubunge wa jimbo hilo, Chenge lakini haikuwa kwa mbwembwe zaidi kama zinavyofanyika kwa wagombea wengine.

"Chenge mnamfahamu, anawapenda, mpeni kura," alisema Kikwete kwa kifupi.

Mgombea aliwasalimia wananchi kwa Kisukuma na baadaye kumwomba Kikwete kusaidia kutatua matatizo ya maji ikiwa ni pamoja na kuchimba visima, ujenzi wa malambo na kuvuta maji kutoka Ziwa Victoria.

Hata hivyo, Kikwete aliwataka wananchi wa Bariadi kutambika, kusali ndipo wapate maji na vile vile kuchimba visima virefu.
Alisema kuwa amelipokea ombi la kuunganisha maji kutoka Ziwa Victoria.

Kwa upande wa barabara, alisema kuwa serikali imetenga Sh2.5 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Bariadi hadi Lamadi na zile za kutoka Bariadi-Maswa na ile ya Bariadi Mwigumbi.

Katika hatua nyingine, Kikwete amesema serikali imetoa jumla ya Sh21 bilioni kwa ajili ya kulipa fidia wakulima kutokana na kuporomoka kwa bei ya mazao katika soko la dunia.

"Serikali ililitambua tatizo la kuporomoka kwa soko la dunia, sasa ilichofanya ni kutoa fidia ili waendelee kujikwamua kutokana na mdororo huo na lengo hasa ni kuwawezesha kufanya kazi zao," alisema.

chanzo: Mahakama yaagiza Chenge akamatwe
 
Back
Top Bottom