Mahakama yasitisha kwa muda mchakato wa kuwapunguzia mshahara wabunge na kuwafutia baadhi ya posho

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,242
2,000
KENYA: Mahakama imezuia kwa muda mchakato wa kupunguza mishahara ya wabunge kutoka Kshs 710,00 hadi Kshs 621,250, mchakato huo pia ulilenga na kuwaondolea posho za kuhudhuria vikao vya bunge usafiri na magari

Tume ya Mishahara (SRC) ililenga kuokoa kiasi cha Kshs. bilioni nane kwenye gharama ya kuwalipa watumishi wa umma

Tume ya huduma za bunge umepata agizo la mahakama kusitisha utekelezaji wa mpango wa tume ya mishahara (SRC), Jaji George Odunga alikubaliana na tume ya PAC kuwa SRC haikuzingatia kupanda kwa gharama za maisha ilipopunguza mishahara yao

Kesi hiyo itasikilizwa tena January 26 mwakani

Hii inamaanisha kuwa wabunge watapokea kiasi kisichopungua Kshs milioni 1 mwezi Disemba na January na pia kupokea posho za usafiri, na Kshs 5,000 kama posho za kikao cha bunge au kamati pia kupata magari yasiyozidi thamani ya Kshs milioni 5 na kupata mkopo wa Kshs milioni 20 kwa ajili ya kununua nyumba

Bunge litakuwa na jukumu kubwa kuwachagua wajumbe wa tume ya mshahara mwaka ujao na suala la mishahara na posho zao zitachangia pakubwa watakaochaguliwa kwenye tume hiyo


 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom