Mahakama yasimamisha uuzaji samaki wa Magufuli-wizi mtupu

May 4, 2009
34
1
Mahakama yasimamisha uuzaji samaki wa Magufuli




Na Mwandishi wetu






email.png








Magufuli.jpg

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, John Pombe Magufuli.



Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam, jana ilisimamisha zoezi la uuzaji wa tani 296 za samaki aina ya johari kutokana na ukiukwaji taratibu za kisheria.
Mkurugenzi wa Yono Auction Mart, Staney Kevela, alisema zoezi hilo ambalo lilikuwa lifanyike jana saa 10:00 jioni, lilisitishwa baada ya kupata amri ya Hakimu wa Mahakama ya Kisutu, Addy Lyamuya.
Kevela alisema kutokana samaki hao kuwa ni kidhibiti, ilikuwa ni sharti lazima Hakimu au karani awepo kwenye zoezi hilo.
Alisema hatima ya kuuzwa samaki hao, sasa itatolewa leo na Hakimu huyo baada ya kukutana na kamati iliyoundwa kwa lengo la kusimamia uuzaji wa samaki.
Kevela alisema leo 2:30 asubuhi, wanatarajia kukaa pamoja na Hakimu Lyamuya kwa maelekezo zaidi.
Hata hivyo, baadhi ya wanunuzi waliofika kwenye mnada huo uliopangwa kufanyika Bahari Food, walisema zoezi hilo halifanywi kwa uwazi.
Mmoja wa wateja hao, Ayoub Kibau, alisema hajaridhishwa na utaratibu wa zaoezi nzima kutokana na uwazi haupo.
Mnada huo pia ulishindwa kufanyika Jumamosi wiki iliyopita kutokana na bei kubwa iliyopangwa na serikali.




CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom