Mahakama katika mji wa Toronto nchini Canada imetoa hukumu ya kihistoria ambayo huenda
ikazusha mjadala mkubwa kuhusiana na biashara kongwe kuliko zote duniani, "biashara ya ukahaba".
Hukumu hiyo imetolewa baada ya makahaba kuifungulia kesi serikali ya nchi hiyo wakitaka biashara
yao ihalalishwe na kuzuia ubaguzi dhidi yao. Mahakama katika hukumu yake imesema kuwa makahaba
wanastahili kupata ulinzi kikatiba, hawastahili kubaguliwa, na kwamba biashara yao ni halali-wanastahili
ulinzi toka serikalini na kwamba wanapaswa kulipa kodi kama wafanyabiashara wengine.Hata hivyo serikali
imepewa muda wa kukata rufaa kabla ya utekelezaji wa hukumu hiyo. Hukumu hii imekuja wakati ambapo
mkuu wa kanisa katoliki duniani Pope Benedict wa XVi akiendelea na ziara yake huko America. Kanisa hilo
limekuwa mstari wa mbele kuipinga biashara hiyo. (Source-Aljazeera). Je ndiyo tuseme ule upepo wa kuruhusu
vitendo vya ukahaba na ushoga umeanza kuvuma?